Je, kwa takwimu hizi, Ki Aziz ni mchezaji mzuri au wa kawaida?

Okay! Kwenye kundi walilokuwemo, pamoja na Simba, aliisaidia timu yake kushika nafasi ya ngapi? Na Simba walishika nafasi ya ngapi?
Huyu si ndiyo alimgeuza geuza Inonga kama chapati,kisha akalitungua lile shati Manula
 
Mkuu nahisi utakuwa umeanza kushabikia mpira kipindi hiki cha mayele. Haya mambo kwenye mpira yapo. Hakuna timu ambayo imekuwa bora miaka yote hata ungeenda ulaya.
Mwaka umekuwa mzuri kwenu mtachukua vikombe lakini siyo kwamba mtakuwa bora miaka yote. Kuna mwaka mtayumba wengine nao watachukua.Na huo ndiyo mpira.
 
Ndugu ligi ya bongo ni kitu kingine kabisa! Mtu anaweza akaja mzuri lakini mkajikuta mnamsitishia mkataba
 
Mwaka mzuri aujitokezi kwa kupiga ramli au kwa bahati nasibu mkuu, mwaka mzuri utakuja kama umesajili vizuri na kama umeinvest vya kutosha kwenye jambo husika, Unachokuwa umepanda ndo utavuna ichoicho usitegemee kupanda bangi ukategemea kuvuna mahindi, ukisajili ovyo basi usitegemee miujiza au mazoea ndo yakubebe, kuwa na heshima na waliokuzidi ubora mambo ya chuki, dharau na roho za korosho yatazidi kukuongezea stress tu na wala auwezi kuwapunguzia wala kuwaongezea chochote zaidi ya kuumia tu
 
kesho saa 9:10 Alfajiri ngoja tuwatetemeshe halafu ndio mtaelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…