Je kwa Uzembe huu wa madaktari ulivosabababisha kumpoteza mdogo wangu,nilikosea kuwaacha ningechukua hatua??,(ukweli)

Je kwa Uzembe huu wa madaktari ulivosabababisha kumpoteza mdogo wangu,nilikosea kuwaacha ningechukua hatua??,(ukweli)

NITAKUKAMATA TU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2021
Posts
347
Reaction score
432
Habari wana jamvi,leo nimekuja na thread hii. hili pengn kama kuna mtu,anaweza kujikuta katika hali kama hii,pengine wawe waangalifu .
Ep1
Mimi ni mzaliwa wa pili katika familia yetu ,familia yetu ilikuwa ya watoto sita .mama yetu alifariki tukiwa bado wadogo .tukabaki na baba ambaye alikuwa akai nyumbn kutokana na shughuli ,baba yetu alikuwa anakaa wilaya nyingine tofauti na tulipokuwa tunakaa,sisi,hivyo muda wa kuja nyumbn ilikuwa ni jumamosi na jumapili kila week,kaka yetu yeye aliondoka nyumbn kwetu kikazi,kwenda mkoa mwingine ,kipindi hicho mimi bado nilikuwa nakaa nyumbn kwetu sababu ya kuangalia wadogo zangu 4 ,ambao walibaki nyumbani,iyo ni kutokana na ukoo kukaa. baada ya msiba wa mama na kuona wadogo zangu ni wadogo na pia wanamasomo ,baba na kaka wako mbali kikazi hivo mimi nibaki nyumbn ili kuwangalia.
Kipindi huu hicho nilikuwa nafanya kazi katika sheli moja maarufu ya mafuta,

(Kisa)Basi siku moja nilikuwa off kazini.hivo nilienda mchana kazini kupiga story na wafanyakazi wenzangu,hilipofika Mida ya saa 10 niliondoka kulejea nyumbn,nilipofika nyumbn sikukuta mtu.basi nilichukua vifaa vya michezo na. Kuelekea uwanjani kucheza mpira, uwanja ulikuwa wa shule moja ya wasichana jirani na makazi yetu .hivo nilikuwa naenda mara zote ninapokuwa offkazin,
Basi nilipofika uwanjani niliwakuta wadogo zangu wawili .wa pili na wa tatu kutoka mwisho hila wa mwisho aliekuwa na miaka 16 alikuwa hayupo,na aliekuwa ananifatia alikuwa anashughuli zake hivo sikuwa na wasiwasi nae,mdogo wetu uyo wa mwisho wakati anazaliwa ,alikuwa na dalili zote za sickle cell(siko seli).hivo toka mdogo alikuwa anapitia mara kwa mara maumivu makali ya mifupa Asa mikono na miguu, pia kuishiwa damu mara kwa mara,hivyo ilisababisha ukuwaje wake uwe dhoofu,,hilikuwa ni mara 2 adi 3 kwa mwezi lazima tumpeleke hospital kutokana na kuishiwa damu ,na maumivu ayo ya mifupa ya mikono na miguu.alikuwa akianza kupata maumivu ayo ya mifupa, kama ni mguu usiku, atataka uhu bebe mguu uwe umeunyanyua juu ,ndio anapata unafuu kidogo au mkono,baada ya siku 2 adi 3 alikuwa ndio anapata unafuu lakini kama ulikuwa ni mguu.akianza kutembea baada ya kutoka kitandani ,anakuwa anachechemea mpaka siku kidogo tena ndio anakuwa na hali ya kawaida.

Nitaendelea.....

Asanteni.
 
EP 2
INAENDELEA.............
basi akiisha toka katika maumivu ayo ya mifupa ya mikono na miguu baada ya siku 2 adi 3 kuwa sawa,ilitufanya tumuangalie,kwa umakini na kuwa karibu nae ,basi nilivyo fika uwanjani nikakuta hayupo niliwauliza ,wadogo zangu niliowakuta lpale,wakaniambia kwamba mdogo wetu uyo ameenda na watoto wenzake wa hapo mtaani kucheza mechi ya mpira wa makaratasi (sembu) .na watoto wa mtaa wa jirani ambapo ni mbugani kulikuwa na mashamba ya mpunga ,basi sikupata wasiwasi baada ya kujua wapi alipoenda,
Nilijiandaa na kutaka kuanza mazoezi hapo uwanjani,
Mara ghafla walikuja watoto 2 wa jirani yetu kunifata hapo uwanjani ,wakaniita nikatoka na kwenda kuwasikiliza sababu nilikuwa nawajua na uwa ni marafiki wa wadogo zangu,
Nilipofika waliniambia kwamba niwah nyumbn ,mdogo wangu kuvunjika mguu, nilishangaa sana ,nikawauliza kavunjika mguu kwa sababu gani, wakasema walikuwa wanacheza sasa mdogo wangu alipotaka kupiga mpira,mtoto mwingn aliekuwa timu pinzan alimrukia na miguu yote ,hivyo alipopiga akakuta miguu ya mtoto uyo na kuvunjika,nilipatwa na wasiwasi mkubwa na kuchanganyikiwa kwa muda,basi bila kusubiri ,niliwaambia wachukue vitu vyangu nilipokuwa nimeviweka ,mimi nilitoka kwa haraka kuwahi nyumbn kumuona mdogo wangu,wakati nakimbia yan akilini nilikuwa nawajua jinsi gani ana mahumivu,basi kwasababu hilikuwa ni jirani niliwahi kufika ,nilikuta majirani wengi wameshafika nyumbn ,niliingia moja kwa moja mpaka ndani kwenye chumba chao walichokuwa wanalala,
Nilimkuta alikuwa ameshaletwa na mtoto wa jirani yetu aliekuwa ni rafiki yake ,alimbeba mgongo mpaka pale nyumbn, alikuwa amevunjika chini kidogo ya ugoko,,(ukitoka kwenye ankle juu kidogo yan katikati ya ankle na ugoko)basi bila kuchelewa nilivunja kibubu changu ambacho nilikuwa naifazi pesa cash,hili niwah kumpeleka hospitali,nilitoka mpaka barabarani na kuchukua boda ,kuelekea hospitali,
Hospitali ya kwanza nilipenda hilikuwa ni ya kanisa la aic ,ambalo niliona lilikuwa jirani kwa yeye kupata hudumu ya haraka ,
Baada ya kumfikisha hapo hilikuwa majira ya saa 11 kuelekea 12
Basi madaktari walimpokea na kumuangalia ,wakasema awataweza kumtibu sababu wao awana mashine ya xray,hivyo niende hosptal kubwa ,ambayo ilikuwa ni ya serikali

ITAENDELEA

ASANTENI....
 
Back
Top Bottom