Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Katika miaka ya hivi karibuni, tumezidi kushuhudia ongezeko kubwa la matatizo ya kiafya kwa watoto na vijana. Kuanzia mwaka 2000 hadi sasa, imekuwa kawaida kusikia watoto na vijana wakikumbwa na magonjwa ya uzazi, matatizo ya afya ya akili, matatizo ya kimwili kama vile unene kupindukia, na hata utegemezi wa dawa za kulevya ili kuhimili maisha ya kila siku.
Kwa mfano, mtoto wa kike ambaye bado yupo Sekondari anaweza kuishi na ugonjwa kama Polycystic Ovary Syndrome (PCOS) bila hata kuelewa chanzo chake. Wengine wanakumbwa na changamoto ya ugumba, pamoja na matatizo ya homoni. Wapo watoto wana matatizo ya mfumo wa upumuaji, kiasi kwamba akikimbia dakika 10 pekee mtoto anahema utadhani amekimbia riadha kilomita 42.
Aidha, kuna ongezeko la matatizo ya mfumo wa mkojo (UTI) kwa watoto wa kike, ambayo zamani yalikuwa nadra sana. Vijana wa kiume nao wanapitia magumu kweli – wengi wao wanapigwa na msongo wa mawazo, hali yao ya kujiamini kupungua, na matatizo ya kisaikolojia ambayo hayakuwahi kuonekana kwa wingi kipindi cha nyuma.
Katika kipindi cha vizazi kama Baby Boomers, Generation X (Gen X), pamoja na Millennials (Gen Y) kulikuwa na kiasi kidogo sana cha haya matatizo, ila kuanzia Generation Z (Gen Z) na hiki kizazi cha Generation Alpha kwa hakika kizazi cha Generation Beta kitakuwa ni majanga juu ya majanga.
Wazazi na walezi wengi tunapaswa kujiuliza maswali magumu:
Je kuna nini tofauti kati ya kizazi cha sasa na kile cha miaka ya 1960 hadi 1990?, ni kipi Baby Boomers, Generation X (Gen X) walikifanya mpaka kukawa hakuna kesi na takwimu nyingi za watu wenye matatizo namna hii?
Zamani, ilikuwa nadra sana kusikia mtoto anaumwa magonjwa kama haya. Ilikuwa ni kitu cha ajabu ukisikia mtoto wa fulani anachoma sindano kila mwezi kwa sababu ana hormonal imbalance.
Watoto walikuwa na nguvu, afya nzuri na walikuwa na matumaini makubwa ya maisha. Leo hii, tunashuhudia kizazi kilichojaa hofu, magonjwa, na kutegemea madawa kwa maisha yao ya kila siku. Kuna vijana bila kutumia Ibuprofen, naproxen, diclofenac, etoricoxib, indomethacin pamoja na aspirin maisha yao yatakuwa magumu sana.
Je, ni mabadiliko ya kimazingira? Je, vyakula tunavyokula leo vina athari kiasi gani? Au ni teknolojia, mitindo ya maisha, na msukumo wa kijamii unaochangia haya yote? Je, jamii yetu ina nafasi gani katika kuzuia au kutibu matatizo haya?
Ningependa kusikia kutoka kwako. Je, una maoni gani kuhusu ongezeko hili la matatizo ya kiafya kwa watoto na vijana wa sasa? Je, ni jambo la kawaida kutokana na maendeleo ya dunia au ni tatizo linalopaswa kushughulikiwa kwa dharura?