Je, kwanini tumekataliwa kutumia jina la mkoa kwenye biashara?

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
Habari wadau, tuna kampuni yetu ya mambo ya Media ambayo iko Mkoa mmoja hapa Tanzania, tuliplan kufungua gazeti ambalo litakuwa linadeal na kuandika habari zinazohusu maendeleo na fursa za mkoa husika, kuna mtu yuko Dar tulimuagiza atusaidie kusajili, tatizo likawa jina, wamekataa jina tulilosuggest pamoja na kwamba halijawahi kutumika, wanasema hawakubali majina ya mkoa au wilaya, sasa tumeshindwa kuelewa hii sheria imeanza sikuhizi au vipi, maana kuna magazeti tunayajua yanatumia majina ya mkoa e.g Arusha Times, Kigoma Yetu. Pia kuna yanayotumia hata jina la nchi e.g Tanzania Daima, Mtanzania. Naomba nieleweshwe ili tujiridhishe kabla hatujaamua kufikiria jina jingine
 
Ukitumia jina la mkoa unaleta ubaguz wa kikanda

OK, na vipi kwa hao walioruhusiwa kuyatumia hao Arusha Times na Kigoma Yetu? Na je kuhusu wanaosajili mfano timu ya mpira na kuiita 'Mbeya City' wanatofauti gani na sisi?
 
Not sure why but the logic suggest the reasons is to avoid a public corporation look alike!, ukianzisha The Darisalama Media Company, wana Daisalama watandhani hiyo ndio kampuni yao ya media hivyo utagain more favorable advantage!.

Pasco

Ebu mleta mada ajaribu kueleza vema zaidi, ni aina gani ya biashara wanayotaka kuanzisha.
 
Ebu mleta mada ajaribu kueleza vema zaidi, ni aina gani ya biashara wanayotaka kuanzisha.

kasema gazeti tena unaulizia biashara mkuu

MIMI CHA KUMSHAURI AENDE MWENYEWE MAMBO YA KUMTUMIA MTU YALISHAPITWA NA WAKATI na kuna kupotoshana sometimes na mara nyingi kumtumia mtu hawezi kuwa mdadisi kama wewe mwenyewe
 
Kuna mdau wamekujibu vizuri hapo juu kwamba ni vema ukaenda wewe mwenyewe pale Maelezo ukaonana na Msajili wa Magazeti. Binafsi, sioni tatizo la jina la mkoa kutumika. Tatizo linaweza kuwa kwenye jina la kabila kwa mfano; Wakurya, Chagga Times, Makonde News, na kadhalika. Lakini jina la Mkoa sioni kama hilo ni tatizo kwa sababu yapo magazeti mengi yenye majina ya aina hiyo. Ebu tembelea ofisi za MAELEZO, inawezekana huyo uliyemwagiza hajafika au kaona usumbufu wa hapa na pale kwa sababu kuna mlolongo kidogo! Kwa zama hizi za Rais Magufuli utafanikiwa.
 
Manyerere Jackton
THE RICHARDS
Pasco

Nawashukuru sana kwa maoni yenu, nimefanikiwa kuongea direct na msajili kwa njia ya simu kaniambia haina tatizo, otherwise jina liwe limeshatumiwa na mtu mwingine!
 
Last edited by a moderator:
Manyerere Jackton
THE RICHARDS
Pasco

Nawashukuru sana kwa maoni yenu, nimefanikiwa kuongea direct na msajili kwa njia ya simu kaniambia haina tatizo, otherwise jina liwe limeshatumiwa na mtu mwingine!

Safi kabisa. Wakati mwingine uwe unawasiliana na wahusika moja kwa moja, maana wanaoagizwa mara kadhaa huwa hawafiki na kwa sababu hiyo hutoa majibu yasiyo kweli. Hongera na karibu kwenye shughuli hii inayohitaji ujasiri.
 
Asante sana mkuu
 
kabisa pia hawawi makini maana hana uhitaji congrats mkuu mafanikio mema
 
Hilo jina sio "KILIMANJARO" ? maana kuna mtoto wa mwana mfalme alisema watu waishio kule ni wezi. Kwa hiyo sishangai kama litakuwa limekataliwa. Halafu kama kuna ARUSHA TIMES kwanini neno lingine la mkoa likataliwe? Huyo jamaa yako amekuongopea tu sidhani kama kuna sheria kama hiyo.
 
hahaha hapana mkuu sio Kilimanjaro, thanks kwa comment yako
 
Asante mkuu

pamoja mkuu Na kukushauri zaidi anza kuulizia bei za kuprint masoko katika hizi hatua za awali TEMBELEA TOVUT ZAO WANAOPRINT kama huzijui angalia kwenye magazeti na fanya mawasiliano nao MAGAZETI MENGI YAMESAJIRIWA NA KUISHIA KAPUNI TATIZO PRIO INFORMATION HAMNA NA KUFANYA KITU KWA KUIGA SIO PASSION
Kuna mdau hapo
inaonekana yupo katika industry hiyo anza mawasiliano nae as starting point au omba wengine humu waliopo sekta hiyo
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…