screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,857
- 15,866
Habari wadau, tuna kampuni yetu ya mambo ya Media ambayo iko Mkoa mmoja hapa Tanzania, tuliplan kufungua gazeti ambalo litakuwa linadeal na kuandika habari zinazohusu maendeleo na fursa za mkoa husika, kuna mtu yuko Dar tulimuagiza atusaidie kusajili, tatizo likawa jina, wamekataa jina tulilosuggest pamoja na kwamba halijawahi kutumika, wanasema hawakubali majina ya mkoa au wilaya, sasa tumeshindwa kuelewa hii sheria imeanza sikuhizi au vipi, maana kuna magazeti tunayajua yanatumia majina ya mkoa e.g Arusha Times, Kigoma Yetu. Pia kuna yanayotumia hata jina la nchi e.g Tanzania Daima, Mtanzania. Naomba nieleweshwe ili tujiridhishe kabla hatujaamua kufikiria jina jingine