SAUTI YAKO
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 2,944
- 2,032
Ninaandika haya sio kwa kuponda stlye zetu za kila mwaka za watu kujipanga na likatokea neno labda miaka 60 ya uhuru nadhani vitu hivyo zama hizi za tekenolojia tungeviweka pembeni na tutoe nafasi kwa watanzania wavumbuzi kwenye sherehe hizi kwani itatusaidia kuchochea ukuaji wa tekenojia hapa kwetu na kututangaza Duniani.
Mimi nashauri miaka ijayo siku kama hii walau pale katikati ya uwanja tutangaze utalii wetu kwa kuwaleta twiga,simba,chui na wanyama wengine mara moja moja kwenye matukio kama haya,nadhani kwanza itavutia watanzania wengi kuja kushuhudia maadhimisho hayo lakini kipaumbele cha kwanza kuwe kuonyesha vitu vilivyogunduliwa au kutengenezwa hapa nchini katika zama hizi za sayansi.Nawatakia watanzania wote sikukuu njema na tuendelee kuchukua taadhari kwa mvua zinazoendelea