Uchaguzi 2020 Je, lengo la watawala kukifanya chama cha NCCR Mageuzi kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya mwaka 2020 litafanikiwa?

Kuna idadi ya kura na wabunge inayokifanya chama kuunda kambi ya upinzani bungeni.

Sidhani kama Nccr mageuzi wataweza kuqualify!
 
wananchi wengi wapi? Chedema imetukatisha tamaa kabisa, hata hao NCCR mageuzi ndiyo wale wale tu sasa hivi tumurudi chama kimoja. Siasa za Tanzania haziaminiki tena
 
Basi kumbe we ni wa juzi. Waulize wazee wako mrema alikuwaje enzi zile. Kisha waulize walikuwa wanamjua freeman mbowe.
Mbowe kafahamika baada ya operation sangara 2009. Katika uchaguzi wa 2005 mbowe alipata kura laki sita tu nchini nzima.

Ndio maana akakimbilia bungeni tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu kwanza ccm yenyewe haina mvuto, bali mvuto wake unapatikana kupitia vyombo vya dola, je itawezaje kuwapa mvuto hao NCCR? CCM hiyo hiyo walitaka kumpa mvuto Lipumba, saa hii wameishia kuipotezea mvuto CUF, wameona ngoja wajaribu kwa Mbatia kupitia NCCR. Tatizo ambalo ccm hailijui ni kuwa mapenzi ya shuruti hayawezekani tena kwa kizazi hiki. Ni kweli mwenyekiti wa ccm kwa kupitia madaraka yake ya urais, anaweza kutumia madaraka yake vibaya kuipa viti kadhaa NCCR, lakini hakuna uwezekano wowote wa kuifanya iwe chama kinachokubalika.

Halafu ccm ni kama inataka kuvipumbaza vyama vya upinzani vijione vyenyewe nafasi yao ni kuwa vyama vya upinzani tu. Hapo wanataka kujiweka kwenye mazingira mazuri kuwa wao ni washindi, ila ushindani upo kwenye kuwa chama kikuu cha upinzani! Hiyo NCCR inajua fika hata kukiwa na tume huru ya uchaguzi haina uhakika wa kupata hata viti kumi vya ubunge, hivyo imeona bora ijinyenyekeze kwa ccm, kwani inajua rais ana uwezo wa kuchezea uchaguzi na kuwahonga vita kadhaa.
 
wananchi wengi wapi? Chedema imetukatisha tamaa kabisa, hata hao NCCR mageuzi ndiyo wale wale tu sasa hivi tumurudi chama kimoja. Siasa za Tanzania haziaminiki tena
Wewe huwajui wananchi wengi waliokonga nyoyo za chama cha Chadema ni wepi?

Hebu fanya analysis hapa JF pekee, utakuta kuwa wafuasi wa CCM wanafanya kuhesabika........

Wakati majority wanaiunga mkono kwa dhati chama cha Chadema
 
Hapo kwenye red, kama viongozi wa chadema wanahama kwa kupewa MAELEKEZO na sisiemu, basi hicho khakikua chama cha upinzani bali sisiemu C.

Wataacha kuhama mbele ya hongo na hatari ya kupotezwa na kundi la watu wasiojulikana? Udhaifu wa mtu binafsi usiuambatanishe na chama.
 
Kuna idadi ya kura na wabunge inayokifanya chama kuunda kambi ya upinzani bungeni.

Sidhani kama Nccr mageuzi wataweza kuqualify!
Kupitia dola ya ccm lolote linawezekana, fikiria ccm wanaweza kukimbia na masanduku ya kura then wanayarudisha yakiwa na kura za ccm, sasa kipi kinashindikana bwashee??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tindo
Naunga mkono yale uliyoyasema kwa asilimia 100...........

Kilichobaki kwa CCM hivi sasa ni ku-abuse power anakokufanya Mwenyekiti wake kwa kuvitumia vyombo vya dola, utadhani ni mali yake binafsi!
 
Wataacha kuhama mbele ya hongo na hatari ya kupotezwa na kundi la watu wasiojulikana? Udhaifu wa mtu binafsi usiuambatanishe na chama.
Kwa nini mnakuwa na wanachama wanaohongeka? Vetting yenu ina mapungufu...na vetting hii inafanywa na viongozi hivyo udhaifu wa viongozi ni udhaifu wa chama.
 
Kwa kiasi ccm wamefanikiwa kuwagawa wapinzani maana hata ACT wanaona Membe ndo chaguo sahihi.Lakini tujue tu kuwa hakuna mtu anayeweza kuchagua NCCR-Mageuzi kama sio Mwanachama.Labda mtu achague ACT wazalendo kwa kuwafuata Zitto na Maalim seif.Lakini Mbatia kwanza vijana wengi hawamfahamu.Pia NCCR hawana watu wa maana wa kuwasimamisha.Hebu fikiria hao wamama wakina sokombi na masele wasimame jukwaani kuomba ubunge, nakwambia wakipata kura 552 washukuru Mungu.
Chadema bado kuna vijana wengi wanaoweza kunadika na bado ndio chama kinachopendwa zaidi Tanzania.NCcR watagawiwa majimbo na Ccm bure tu kwa kushirikiana na polisi na tume ya uchaguzi.

Kwa nini vyama hivi vinavyosapoti CCM visiungane ili tuwe na vyama viwili au vitatu tu ndio kila mtanzania achague hapo.Sasaivi eti TLP wamemchagua magufuli kwaninu kusifanyike binding ili TLP imezwe na CCM kisha TLP tukifute?Nadhani US kuwa na vyama 2 vya maana wanamaarifa kuliko sisi wenye marundo ya vyama yasiyoeleweka.Kuna chama kinaitwa SA,CHAUMA,DP,UPDP ACT vyote hivi ni trash tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu nenda pia mitaani kwa wapiga kura wenyewe sio wa keyboard na wenye id zaidi ya tano humu uone uhalisia.

yaani wewe na wenzio mna id karibu sita kila mmoja alafu unajivunia mko wengi? Aibu!
 
Kwa nini mnakuwa na wanachama wanaohongeka? Vetting yenu ina mapungufu...na vetting hii inafanywa na viongozi hivyo udhaifu wa viongozi ni udhaifu wa chama.

Unapokuwa na watu zaidi ya 1,000 usitegemee wote kuwa na roho za kishujaa. Sio kila mtu anaweza kusimama imara mbele ya kundi la watu wasiojulikana. Wengine uongozi kwao ni ajira, anapoona akiingia kwenye uchaguzi hata akishinda hatangazwi, ni kwanini asihamie mahali alipoahidiwa kuendelea kuwa kwenye uongozi ili alishe familia yake? Mbona hiyo ni saikolojia ya kawaida sana?
 
Hivi ACT WAZALENDO imesahaulika kama inaweza pindua meli katika bandari ya Zanzibar na kufanya matakwa ya hao Nccr na washirika wake wakaangukia pua?.
 
Kwenye Uchaguzi fake uliojaa wizi, vitisho na ulaghai LITAFANIKIWA. Kwenye Uchaguzi huru na wa haki msaliti Mbatia hataambua kitu.
Hivi huko NCCR Mageuzi kumetokea nini sasa?Wamegeuza Sera,malengo,katiba,au?Mbona ghafla bin vuuu wimbo wa mapambio ya wanaCCM umekuwa ni NCCR Mageuzi?Ajabu na KUB wamemteua ni Mbatia,je CCM ndicho humchagua KUB?
Maswali ni mengi ila hakuna wa kutujibu.
 
CCM wanamjua Mbatia kwamba hana msimamo hivyo sidhani kama watampa hiyo fursa!

Hawataki kumpa hiyo nafasi, bali wanamtumia ili kuwabeba kwenye mazingira ambayo wamejiandaa kufanya hujuma kwenye uchaguzi. Wameshampotezea mvuto Lipumba na CUF, hivyo wameona bora wamtumie Mbatia aliyekuwa Ukawa, wakiamini wataipotezea mvuto cdm. Hata huyo Mbatia wataangalia mazingira ya uchaguzi, wakiona hana mvuto waliotegemea yeye na chama chake watampotezea, na Mbatia atapewa nafasi yoyote huko mbeleni kama kifuta jasho.

Mtindo huo huo wa kuwatumia wapinzani wanaofahamika pia ulifanyika uchaguzi uliopita kwa chama cha ACT. Bahati mbaya wananchi wanajitambua hivyo ACT haikupata kura tarajiwa. Alivyoingia Magufuli Zito alitaka kujipendekeza lakini Magufuli akawa hataki chain ya Kikwete. Ndio maana Zito hawaivi na Magufuli baada ya kupandishiwa vioo. Hiyo ACT iliundwa na kina JK, Membe, Mwigulu nk kama backup ya ccm. Iwapo Magufuli angekuwa anataka kufanya kazi na kundi la Kikwete, hii ofa aliyopewa Mbatia, angepewa Zito na ACT yake. Nadhani umesikia Membe anaweza kugombea ACT, hiyo sio bahati mbaya, yeye ndio kinara, lakini ile movie ya Lowassa na cdm 2015, ni kama imeharibu mkakati mzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…