Ukiangalia mwenendo wa viongozi wa Chadema hivi sasa wanaohama chama hicho kuhamia NCCR Mageuzi utagundua wazi kuwa chama tawala kina mkakati wa wazi wa kukifanya chama cha NCCR Mageuzi kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya mwaka 2020
Tamko la kiongozi wa NCCR Mageuzi, James Mbatia la hivi karibuni linalithibitisha hili, pale alipotamka kuwa chama chake cha NCCR Mageuzi ndicho kinachotegemewa kuwa chama kikuu cha upinzani nchini baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
Huo ndiyo mkakati wao watawala wetu wa CCM wa "kukiwezesha" chama cha NCCR Mageuzi kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya mwaka 2020
Hata ukiangalia viongozi wanaohama Chadema hivi sasa, wengi wao wanahamia chama cha NCCR Mageuzi, ikionekana wazi, hayo ni "maelekezo maalum" kutoka kwa chama tawala
Kulithibitisha hilo tumejionea namna wabunge wawili wa kuchaguliwa, akina Antony Komu na mwenzie Selasini, wakisema wazi kuwa wanahamia chama cha NCCR Mageuzi.
Si hao tu, hivi majuzi tumeshuhudia pia wabunge wengine wawili wa viti maalum wa Chadema, Suzane Masele na mwenzie Joyce Sokombi, nao wakifuata nyayo hizo hizo za kuhamia chama cha NCCR Mageuzi
Swali langu ni je watawala hawa wa CCM wataweza kuufanikisha mkakati wao huo?
Nauliza swali hili, kwa kuwa najua kuwa mioyoni mwa watanzania mamilioni tegemeo lao kubwa lipo kwa chama cha Chadema, kuwa ndiyo chama pekee cha upinzani nchini, cha kuwakomboa kutoka kwenye mikono ya chama tawala.
Je watawala wetu wataweza kugeuza mapenzi ya mamilioni hao wa kitanzania kwa chama chao cha Chadema na waweze kukipenda chama cha NCCR Mageuzi kwa matakwa ya watawala hao?