Uchaguzi 2020 Je, lengo la watawala kukifanya chama cha NCCR Mageuzi kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya mwaka 2020 litafanikiwa?

Uchaguzi 2020 Je, lengo la watawala kukifanya chama cha NCCR Mageuzi kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya mwaka 2020 litafanikiwa?

CCM haijawahi kutaka upinzani wa kweli nchi hii ndio maana inajaribu kuuwa vyama vya upinzani kwa kutumia dola au kutengeneza mfano wa chama cha upinzani ambacho ni jina tu upinzani ila matendo yake yawe ccm ili watawala walale usingizi
Mbatia amuulize Lipumba CUF 2020 haiwezi pata hata diwani mmoja, 2016 Lipumba alikuwa anashinda Ikulu kama kwake.
 
Dawa ya hawa CCM ni ndogo sana, ni kuikataa Tume yake hii ya uchaguzi, ambao muundo wake ni wa hivyo kupita kiasi.. ushahidi ni chaguzi ndogo zote zimeleta mauaji na fujo za ajabu...

Leo kada wa chama mtiifu wa CCM eti ndiye awe msimamizi Mkuu wa uchaguzi? hata ningekuwa mimi nitasikiliza chama changu kinanitaka nifanye nini.

Hizi tuhuma za CCM kutaka kuitengeneza NCCR kuwa chama kikuu cha upinzani ki kubwa mno, lazima zifanyiwe kazi kabla ya uchaguzi Mkuu mwezi October.
 
jme
Ni kweli kabisa ukisemacho, ni lazima pia watanzania tujiulize hivi hiki chama cha NCCR Mageuzi si ndicho kilikuwa chama kikuu cha upinzani nchini baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995?

Nini kilitokea baada ya hapo?

Ni kusambaratishwa kwa chama hiko kwa "usimamizi" wa karibu wa chama tawala
NCCR walichangia sana kukua kwa demokrasia lakini chadema wamefifisha kabisa. Hatuwezi kuendelea na chadema kama chama kikuu vinginevyo upinzani utafutika kabisa.Kurudi kwa NCCR kutafufua ustawi wa demokrasia. Karibu sana Mbatia mtoto wa MAMA TANZANIA, ufufue matumaini yetu wanamageuzi
 
Ukiangalia mwenendo wa viongozi wa Chadema hivi sasa wanaohama chama hicho kuhamia NCCR Mageuzi utagundua wazi kuwa chama tawala kina mkakati wa wazi wa kukifanya chama cha NCCR Mageuzi kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya mwaka 2020

Tamko la kiongozi wa NCCR Mageuzi, James Mbatia la hivi karibuni linalithibitisha hili, pale alipotamka kuwa chama chake cha NCCR Mageuzi ndicho kinachotegemewa kuwa chama kikuu cha upinzani nchini baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
Kwanza,
NCCR - MAGEUZI ina mizizi ya CCM. Kama unabisha angalia waasisi wake. Wengi walikuwa ni watu wa system na walienda huko kwa minajili ya kuu-control upinzani ili usiwe kikwazo kwa chama tawala. Na kwa yanayoendelea bado nina mashaka sana kama NCCR - MAGEUZI wanamaanisha kuwa wapinzani wa kweli kama wanavyojitanabaisha
 
Hawa wanasiasa hawajifunzi jamani?ccm wamechoka na propesa na sasa wamehamia kwa mbatia! Mbatia ameshindwa kabisa kupata leaf kutokana na yaliyomsibu propesa??? Ajabu!
Ccm wanachotaka ni divide and rule sawa na mambo yaliyofanywa na makaburu wa Africa ya kusini-kumwambia kila moja “wewe ni bora kuliko Yule” hivyo kwamba kila moja anadhani yeye ni rafiki wa kaburu kwa hiyo atahurumiwa kumbe yote ni uwongo!
Mwulizeni Mrema alichofanyiwa katika local government election 2Alilia kuwa walimwibia hata Kijiji chake kimoja cha Kiraracha. Just imagine that!!!
Mwambieni Mbatia you are in for a surprise!!!!!!’
Hahaha and Hahaha!!!!!!!
 
NCCR inajitambulisha wapi? Kwanza wana watu? Sanasana akihirumiwa Mbatia atapewa kiti chake kimoja bungeni. Na siri yake ya kuwahadaa wafuasi wake ndiyo hiyo. Anataka wafanye kazi bure ili yeye apatiwe kiti chake. Mchezo mchafu huo!!
 
Mkuu Upinzani wote huwa tunajitahidi sana kujipa moyo, lakini huku kwenye ngome yenu Kilimanjaro sisi tunao ishi huku tuna tahadharisha ngome inashambuliwa sana nafikiri kuliko Mbeya,

CCM wanaweza kuikomboa muda wowote, Njooni muongeze nguvu Askari wa akiba tunazidiwa nguvu.
 
Ukiangalia mwenendo wa viongozi wa Chadema hivi sasa wanaohama chama hicho kuhamia NCCR Mageuzi utagundua wazi kuwa chama tawala kina mkakati wa wazi wa kukifanya chama cha NCCR Mageuzi kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya mwaka 2020

Tamko la kiongozi wa NCCR Mageuzi, James Mbatia la hivi karibuni linalithibitisha hili, pale alipotamka kuwa chama chake cha NCCR Mageuzi ndicho kinachotegemewa kuwa chama kikuu cha upinzani nchini baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020

Huo ndiyo mkakati wao watawala wetu wa CCM wa "kukiwezesha" chama cha NCCR Mageuzi kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya mwaka 2020

Hata ukiangalia viongozi wanaohama Chadema hivi sasa, wengi wao wanahamia chama cha NCCR Mageuzi, ikionekana wazi, hayo ni "maelekezo maalum" kutoka kwa chama tawala

Kulithibitisha hilo tumejionea namna wabunge wawili wa kuchaguliwa, akina Antony Komu na mwenzie Selasini, wakisema wazi kuwa wanahamia chama cha NCCR Mageuzi.

Si hao tu, hivi majuzi tumeshuhudia pia wabunge wengine wawili wa viti maalum wa Chadema, Suzane Masele na mwenzie Joyce Sokombi, nao wakifuata nyayo hizo hizo za kuhamia chama cha NCCR Mageuzi

Swali langu ni je watawala hawa wa CCM wataweza kuufanikisha mkakati wao huo?

Nauliza swali hili, kwa kuwa najua kuwa mioyoni mwa watanzania mamilioni tegemeo lao kubwa lipo kwa chama cha Chadema, kuwa ndiyo chama pekee cha upinzani nchini, cha kuwakomboa kutoka kwenye mikono ya chama tawala.

Je watawala wetu wataweza kugeuza mapenzi ya mamilioni hao wa kitanzania kwa chama chao cha Chadema na wawalizimishe kukipenda chama cha NCCR Mageuzi kwa matakwa ya watawala hao?
Wanajilisha upepo...
NCCR ikijitahidi sana kwenye ubunge ni wabunge 1 na labda wa kuteuliwa 2
 
Back
Top Bottom