Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,809
- 6,948
Nina maswali kadhaa ambayo kutokana na umuhimu na uzito wake nimelazimika kuyauliza katika uzi mpya badala ya kutumia nyuzi za kesi hiyo zilizopo sasa.
Siku ya leo wakati Ramadhan Kingai alipoenda mahakamani, alizungumza na kujadiliana na Tundu Lissu na kumwambia maneno ambayo Lissu alikuja kuyatamka mahakamani mbele ya Majaji.
Lissu katika maelezo yake alisema alikutana na Kingai katika chumba au eneo lile lile la mahakama ambapo kesi ilikuwa inasikilizwa. Nadhani hii kauli ilikuwa na umuhimu wa kipekee ndiyo maana aliitamka. Maana moja wapo ni kuwa hawakukutana gizani au nyuma ya pazia. Narudia, hii ni kauli muhimu sana.
Swali langu ni je, wahudhuriaji mahakamani walikuwa bado hawajaruhusiwa kuingia? Vipi waandishi wa habari?
Nilisikia kuna mtu aliripoti mitandaoni kuwa Kingai alifika mahakamani na mapolisi wengi sana na kuwa Lissu alizuiwa kujadiliana na Kingai akiwa na wanasheria wake, pia akasema umeme ulikatika watu wakawa gizani, kwa hiyo ni wazi kuna watu walishuhudia tukio zima la majadiliano ya Lissu na Kingai.
Moja ya picha muhimu ambazo zingebeba taswira nzima ya kumbukumbu ya kesi hii ni picha ya Lissu akijadiliana na Kingai, Wambura au Mkunda kama "mshitakiwa na shahidi wake".
Picha hiyo tumeikosa mpaka sasa.