Je Liverpool ni bora ulaya??

Je Liverpool ni bora ulaya??

Joined
Dec 28, 2016
Posts
50
Reaction score
52
Jana ulikuwa ni usiku wa Ulaya ambapo Liverpool walipepetana na Tottenham ambapo Liverpool walifanikiwa kutwaa ubingwa kwa kuibamiza Tottenham magoli mawili kwa nunge, Salah katika dakika ya kwanza na sekunde 48 na Divok Origi katika dakika za lala salama, unakuwa ubingwa wa 6 katika michuano ya Ulaya ,wapo katika nafasi ya 3 nyuma ys Ac Mila(7) na Real Madrid(13)

Mchezo haukuwa na kasi sana, hii ilichangiwa na goli la mapema la Salah, Liverpool waliamua kuupoteza mchezo na kubaki compact at the back,hii iliwafanya Tottenham kunyimwa clear cut chances za kufunga katika dakika 75 za mchezo, Liverpool walisimama imara kwenye kuzuia kuhakikisha hawapati goli

Mpaka kufikia hatua ya fainali, Liverpool walipitia kwenye mikono ya mabingwa ya Ujerumani, Ureno na Hispania,hii yote inaonyesha ni jinsi gani walivyo na team imara

Pia kwenye league hawakuwa vibaya, wamepambana na kupata pointi 97,walistahili ubingwa, katika michezo 38 wamepoteza mechi 1 tu,jambo linaonyesha ni namna gani wamekuwa team imara zaidi ndani na nje ya Uingereza

Je kubeba taji la Ulaya kutafungua milango zaidi ya kunyakua makombe zaidi??

Je ni sehemu gani ya Liverpool ina mapungufu, je ni mambo gani Liverpool wafanye ili kuendelea kubaki kwenye ubora wao au kuimarika zaidi??

Je nini hatima ya Tottenham,wataweza kuingia kwenye fainali nyingine ya Ulaya hivi karibuni??

Karibuni kwa mjadala
 
Ni kweli kwa England Liverpool na Man city ni timu zenye vikosi vikubwa na vizuri kwasasa.

Ila sijui ni kwangu tu au VP...naona fainali ya UEFA ya mwaka haikuwa na ladha ile tuliyoizoea zinapoingia fainali baadhi ya timu zingine kubwa.

Hata ile ya Liver na R.Madrid mwaka Jana ilikuwa nzuri.

Hii ya Jana imepoa sana.
 
Ni kweli kabisa mkuu. Jana hata mimi sikuenjoy kabisa ile mechi.. yaani ilikuwa utadhani mechi ya ligi, ambayo timu zote hazina cha kupoteza kwa wakati huo.

Goli la mapema liliua ubora wa mechi, lilifanya Liverpool warudi nyuma kulinda goli lao...wakati huohuo Tottenham hawakuwa uhatari wowote dakika nyingi za mchezo...actually mechi haikuwa na mvuto sana

Hata fainali ya last season baada ya Salah kuumia ilikuwa mbovu, iligeuka ya upande mmoja
 
Mkuu liverpool haina kikosi kikubwa bali ina kikosi kilicho bora
 
Just imagine mkuu na vuta kumbukumbu miaka ya nyuma...lbd fainali iwe ni Real Madrid na Juventus au Barcelona na Bayern...unafikiri ingekuwa vile?

England wana mpira wao flan ambao ukiuzoea unakinaisha.
 
Mkuu liverpool haina kikosi kikubwa bali ina kikosi kilicho bora
Ndio...na nimesema ni kikubwa kwsbb ya aina ya wachezaji waliokuwa nje Jana. Shakiri, Keita, Chamberlain, Sturridge n.k
 
Kwaulaya best teams ni man city na Liverpool, wale giants buyern Munich,Real Madrid,Barcelona wapo kwenye kipindi cha mpito baada ya kuwa namisimu kadhaa bora ila now wameshuka,japo juventus anaweza kuingia kwa city naliver
 
Upana wa kikosi sio wingi wa wachezaji kwenye benchi bali ni wingi wa chezaji wazuri. Fikilia pale VVD ange umia nani angeenda kuziba nafasi yake kiasi Cha kwamba tusimiss kama alivyo toka Boby na Origi akaziba nafasi yake vizuri. Kiwazie kikosi kipana na chenye ubora cha cty ukiacha kipa ni eneo gan aina replecement nzuri.
 
Liverpool ni timu bora Ulaya,ndio maana wako nafasi ya 3,wampe muda klopp,msimu wa tatu mfululizo anashiriki fainali zinazoandaliwa na UEFA,SI JAMBO DOGO
 
Msimu uliopita pia walicheza final, figisu za Ramos ndio ziliwazingua
 
Mkuu liverpool haina kikosi kikubwa bali ina kikosi kilicho bora
Nafikiri hii ni moja ya weakness kubwa ya Liverpool, kikosi chao bora hakifanyiwi rotation ipasavyo hasa front three..wanahitaji attacker mwingine mwenye uwezo mkubwa, pia wanahitaji kiungo mwingine mshambuliaji, japo watakuwa na Chamberlain ambaye amepona majeraha yake

Pia hawana namba mbili kama back up ya TAA, hawana pia strong back up ya Andy Robertson
 
Kwaulaya best teams ni man city na Liverpool, wale giants buyern Munich,Real Madrid,Barcelona wapo kwenye kipindi cha mpito baada ya kuwa namisimu kadhaa bora ila now wameshuka,japo juventus anaweza kuingia kwa city naliver
Sanasana Liverpool na Manchester City, hawa Juventus nao wapo kwenye wakati mgumu sana, team ina wazee wengi ambao hawawezi kuhimili kasi ya vijana, refer mechi vs Ajax zilivyokuwa

Alafu mabeki wao wote wazuri umri umekwenda,siku hizi wanafanya makosa mengi sana

Forward wao ni mandzukic ambayo silaha yake ni kichwa na umri wake pia umesogea

Na haina pia kiungo mshambuliaji wa kuongeza creativity mbele
 
Yeah nikweli mkuu
 
Back
Top Bottom