Kila siku humu JF na kwenye Mitandao ya kijamii mbalimbali lazima utakutana na nyuzi za kuwalaumu waafrika kukumbatia Uzungu na kuziacha Mila na utamaduni wao wa asili !
Hicho wanachokifanya waadzabe ndiyo Mila na desturi zao;Hao waadzabe hawajaanza Leo Wala Juzi kufanya hicho wanachokifanya,Kwa bahati mbaya au nzuri kwasababu ya ukuaji wa Teknolojia wewe ndo umewafahamu Leo!
Hao Waadzabe ni Jamii ya kipekee sana miongoni mwa Jamii chache zilizobaki bara la Afrika wakiwa na utamaduni wao wa asili !
Nyama,mizizi na matunda ndiyo vyakula vyao vya miaka yote kwasababu wao ni Jamii inayoishi ikitegemea uwindaji pekee,wao hawafugi Wala hawalimi,ndiyo maana unaona wanakula nyama muda wote!
Wanakula nyani Kwa sana kwasababu analipwa na wao,pia upatikanaji wake ni rahisi nadhani kuliko wanayama wengine!
Lugha Yao imekuwa kivutio Kwa mataifa mengi ulimwenguni,hivyo lugha Yao wanaelewana wao,suala la kundikika sidhani kama nila umuhimu,Nchi inatumia Kiswahili siyo lugha ya Kihadzabe !
Hiyo nyama ambayo wewe Leo ukiwaona wanakula ya kuchoma na kutokosa kwenye masufuria,ni baada ya kupewa elimu namna ya kupika na kuchoma nyama!
Mwaka 2005 nikiwa ninafanya kazi kama kibarua kwenye taasisi fulani tuliwapelekea nguo tukiwa na Askari wa Manyara National park wakiwa wamewabebea nyati kama 5 ili kuwashawishi kushiriki kwenye Uchaguzi mkuu wa mwaka huo,walikuwa sehemu moja inaitwa Yaeda Chini, jamaa walikuwa wanakula nyama mbichi,nilikuwa nina rafiki yangu muhadzabe ila yeye alikuwa amesoma nilienda naye huko maporini Kwa wazee wake,aisee nilikaribishwa na nyama mbichi ya mnyama pori sikula hata kidogo na jamaa alinielewa,wao wanapiga tena fresh kabisa na hawaweki hata chumvi na bado inalika vizuri tu!
Angalau Sasa unaweza kuwaona kwenye Mitandao wanachemsha na kuchoma nyama!,tena siku hizi naona hata utumbo wanapika unaiva wanakula,kati ya vitu ambavyo wao wanasema hawawezi kuchoma au kupika ni Utumbo,walikuwa wanakula mbichi tangu enzi hizo na unashuka freshi,ila nowadays naona wanachemsha!,nadhani wanaendelea kuelimika !
Watalii wanamiminika huko kama mvua kila mwaka kwenda kuwatazama,serikali inaingiza fedha nyingi sana kupitia wahadzabe!