Ccm ni mafiiHivi karibuni kumezuka trend ya waandishi na Youtube duniani kote kwenda maeneo ya wahadzabe na kuwashangaa na kuwachukua video kuonesha maisha yao ikiwemo Ulaji wa nyani, uzamani wao, lugha yao isiyotamkika wala kuandikika na vingine vingi ambavyo kwa dunia ya leo ni aibu au ni kushangaa!
View attachment 3455013
Pia kumeibuka video youtube youtuber wakitania Tanzania kuwa sisi bado tunaishi maisha ya nyani au ya wanyama kwa uzamani
Swali langu:
Je, ni kitu cha kujivunia au ni Kitu cha aibu?
Mkuu nadhani ungejibu mbele ya camera usingeongea huu utoporoWameshawahi kukuomba kuwa wanataka wainuliwe? Kuinuliwa ni kufanyaje?
Acha shobo na maisha ya watu.
Mkuu nadhani ungejibu mbele ya camera usingeongea huu utoporoWameshawahi kukuomba kuwa wanataka wainuliwe? Kuinuliwa ni kufanyaje?
Acha shobo na maisha ya watu.
Nimaisha ya aina hyo ndio yalitufanya tutawaliwe tusiweze kupambana na maadui….Alafu wakishabadilika we utanufaika na nini?
Waache waishi maisha yao. Unataka waanze kuimba "No reform No election" ambayo imeshafeli kama mfanyavyo? 😂😂
Acha ujuaji na kuingilia maisha ya watu wengine.
??Kila siku humu JF na kwenye Mitandao ya kijamii mbalimbali lazima utakutana na nyuzi za kuwalaumu waafrika kukumbatia Uzungu na kuziacha Mila na utamaduni wao wa asili !
Hicho wanachokifanya waadzabe ndiyo Mila na desturi zao;Hao waadzabe hawajaanza Leo Wala Juzi kufanya hicho wanachokifanya,Kwa bahati mbaya au nzuri kwasababu ya ukuaji wa Teknolojia wewe ndo umewafahamu Leo!
Hao Waadzabe ni Jamii ya kipekee sana miongoni mwa Jamii chache zilizobaki bara la Afrika wakiwa na utamaduni wao wa asili !
Nyama,mizizi na matunda ndiyo vyakula vyao vya miaka yote kwasababu wao ni Jamii inayoishi ikitegemea uwindaji pekee,wao hawafugi Wala hawalimi,ndiyo maana unaona wanakula nyama muda wote!
Wanakula nyani Kwa sana kwasababu analipwa na wao,pia upatikanaji wake ni rahisi nadhani kuliko wanayama wengine!
Lugha Yao imekuwa kivutio Kwa mataifa mengi ulimwenguni,hivyo lugha Yao wanaelewana wao,suala la kundikika sidhani kama nila umuhimu,Nchi inatumia Kiswahili siyo lugha ya Kihadzabe !
Hiyo nyama ambayo wewe Leo ukiwaona wanakula ya kuchoma na kutokosa kwenye masufuria,ni baada ya kupewa elimu namna ya kupika na kuchoma nyama!
Mwaka 2005 nikiwa ninafanya kazi kama kibarua kwenye taasisi fulani tuliwapelekea nguo tukiwa na Askari wa Manyara National park wakiwa wamewabebea nyati kama 5 ili kuwashawishi kushiriki kwenye Uchaguzi mkuu wa mwaka huo,walikuwa sehemu moja inaitwa Yaeda Chini, jamaa walikuwa wanakula nyama mbichi,nilikuwa nina rafiki yangu muhadzabe ila yeye alikuwa amesoma nilienda naye huko maporini Kwa wazee wake,aisee nilikaribishwa na nyama mbichi ya mnyama pori sikula hata kidogo na jamaa alinielewa,wao wanapiga tena fresh kabisa na hawaweki hata chumvi na bado inalika vizuri tu!
Angalau Sasa unaweza kuwaona kwenye Mitandao wanachemsha na kuchoma nyama!,tena siku hizi naona hata utumbo wanapika unaiva wanakula,kati ya vitu ambavyo wao wanasema hawawezi kuchoma au kupika ni Utumbo,walikuwa wanakula mbichi tangu enzi hizo na unashuka freshi,ila nowadays naona wanachemsha!,nadhani wanaendelea kuelimika !
Watalii wanamiminika huko kama mvua kila mwaka kwenda kuwatazama,serikali inaingiza fedha nyingi sana kupitia wahadzabe!
HaipoShida Iko wapi bro?View attachment 3455057
Fanya research huwezi kua unakula nyama mbichi na nyani uishi miaka mingiNadhani umri wao wa kuishi unaweza kuwa around 98 au 100
Akili yako ndo inawaza hivo….Waafrika bado tunataka kila kitu kiwe kwa standard ya wazungu.
Wazungu wao hawatujali sisi, lakini sisi macho naakili zote tuna taka approval za wazungu.
Hatuna standard zetu tuna copy na kufuaya mikumbo.
PointlessAcha waishi ivo tena Serikali iendelee kuwapa Ulinzi na Kuwafanyia Close supervision Ili wasitoke kwenye hio Culture Kwasababu tayari hao ni iconic
Turejee duniani Kuna Makabira yako isolated hao wahzabe Bado sana Kuna watu wanaitwa Sentinels wapo India uko Kwa kweli wao hata Vacine hawana na wanaishi maisha ya Kijima haswa na Serikali imeamua kabisa kuwa hairuhusu intruders yoyote kuchangamana nao mana ukipeleka magonjwa haya ya duniani utawaua ivo hawako accessible kabisa
Na Serikali imeamua Kufunga Icho kisiwa na kuamua kuwaacha hapo bila interaction yoyote na intruders
Hao sio wa kwanza duniani hii kuishi Vile, Kuna Communities zipo isolated kabisa na watu na zinaishi Kijima kuliko hao wahzabe wasome watu wanaitwa SentinelsKwan kuna sehemu nimesema wahamishwe
Ujinga ulisomea wap ww
Nadhani naww akili yako iko KM1000 nyuma…Kwamba maisha yao, aibu unaona wewe ? Nadhani cha muhimu ni kutokuogopa watu wanakuonaje au kukufikiliaje; hapo utaishi maisha bora.., ila tukija kwenye maisha ya hawa cha kujiuliza je wanaishi maisha sustainable ? Au wewe unawaona wajinga na wachafu wakati wewe unayejisaidia na uchafu wako kwenda ziwani ili baada ya muda unaunywa (shit where you eat); Sewage yako ni non existent.., au wale wanaoishi kwa kuvuta hewa ya carbondioxide kutokana na traffic kuchafua mazingira hence magonjwa yasiyoisha...
To each their Own...
Wewe unafikiri ni mapato kiasi Gani Serikali inapata kwenye utalii wa wale jamaa? Unajua ni wageni wangapi wanamiminika kwenda kuwaona tena kwa kulipia?Pointless
Iwalinde kwa pesa ya nani??
Yaani wengine wakatwe kodi ili kulinda wala nyani??
Ni wajibu wa kila raia kulipa kodi afu ndo udai ulinzi