Je, Makardinali ni raia wa Vatican?

Kama katiba ya kwao inaruhusu mwananchi wa nchi nyingine kupiga kura kumchagua rais wao, wewe unahangaika nini? Kwani Tanzania inakataza mtanzania kupiga kura nchi nyingine?
 
Hapa inaongelewa nchi ya Vatican sio Italy. Kwa raia wengine ili uingie Vatican lazima kwanza upate visa ya Italy

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Kumbuka na weka akilini kuwa Nchi Lazima iwe huru,iwe na Watu ,Mipaka inayotambulika kimataifa na Mamlaka kamili kumbuka Mamlaka kamili ikiwemo Majeshi kwa maana vyombo vya ulinzi na Usalama .Hivyo jua mambo ya Uraia yambo chini ya vyombo vya Ulinzi na Usalama kitu ambacho VATCAN haina Inategemea Italy hivyo hao Makadinali wanapewa Diplomatic visa kwenda Vatcan na kaguzi zote zinashughulikiwa na Serikali ya Italy hivyo tulia kimya.Kumbuka kuwa kule Watu hawazaliani hivyo pale ni mambo ya Imani tu.Nchi wasiozaliana hawezi kuishi miaka yote hiyo ingeshakwisha.
 
Uongo wa mchana. Alikuwa Katibu Mkuu. Waziri lazima awe Kardinali
 
Sio lazima awe Dar. Hata Rugambwa I alianzia huko Bukoba, Dar alienda baadae.
 
SIo raia wa Vatican. Ni wapumbavu tu wanaotunga conspiracy theories za kijinga. Jamani muwe ata mnaskiliza radio Maria, au source za kikatoliki, sio wasabato au watu wa propaganda.
tupe darasa kidogo kwahiyo ni mabalozi wa vatican tanzania au imekakaje apo
 
Sio lazima awe Dar. Hata Rugambwa I alianzia huko Bukoba, Dar alienda baadae.
Yes sio lazima dar. Ila kuna sababu ya hawa kuwa Dar. Sasa hivi mambo yameenda tofauti kabisa na matarajio? Ingawa inawezekana kukawa na makadinali zaidi ya mmoja. Ni uamuzi wa askofu mkuu wa Roma
 
tupe darasa kidogo kwahiyo ni mabalozi wa vatican tanzania au imekakaje apo
Hawana cha ubalozi, ni hivi cardinal ni cheo ceremonial, kazi kubwa ni kuchagua papa ajaye. Mabalozi wapo ata Tanzania kuna balozi wa Vatican maana ni taifa lile. So suala la kardinali kuwa raia wa Vatican ni uzushi tu.
 
Kwa hiyo Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ana uraia wa nchi mbili tayari?
Vipi, na yeye mnataka kumtengenezea zengwe kama mlivyofanya awamu iliyopita kwa Askofu Kakobe na Askofu Niwemugizi! Kisa tu amewakosoa kwenye mkataba wa bandari?
 
Hawana cha ubalozi, ni hivi cardinal ni cheo ceremonial, kazi kubwa ni kuchagua papa ajaye. Mabalozi wapo ata Tanzania kuna balozi wa Vatican maana ni taifa lile. So suala la kardinali kuwa raia wa Vatican ni uzushi tu.
sawasawa hapo nimekupata
 
Kuna makardinali wa aina tatu na wana kazi tofauti kulingana na muundo wa uongozi pale Roma.

Aina za makardinali ni:
1. Kardinali Askofu
2. Kardinali Shemasi
3. Kardinali Padri
 
Katiba ya Tanzania hairuhusu uraia wa nchi mbili, ila katika hili Kanisa Katoliki lipo juu ya Katiba.
huu upumbavu mnakuwa mnadanganyana wapi hasa? alafu unaaminije jambo kizembezembe tu, eti wana uraia wa nchi mbili , nani kasema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…