figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,132
- 64,416
Nathani BASATA hawapewi ruzuku na Serikali. Wanaishi kwa Jasho la Wasanii kwa kuwapiga faini kisha wanalipana Posho.
Sababu za BASATA kupiga watu fani huwa hazieleweki. Wakikuona umepata hela, wanasubiri ukohoe.
Godfrey Tumaini (Dudubaya) hatishwi na na kufungiwa. Alikaa bila nyimbo zake kupigwa tamgu 2006 lakini hadi leo yupo.
Huyo Mzanzibari wenu akishatoka kwenye madaraka alojipachika, sudubaya atazidi kutamba..
Jana Waziri wa Sanaa Paul Makonda, alisema anashangaa mtu anaimba sijui Linda mgongo wako na bado anazidi kuitwa kuimba kwenye majukwaa.
Baada ya Makonda Jana kuongea. Leo BASATA wamwmfungia dudubaya wakati akijiandaa na mazoezi ya kwenda kwenye show ya miaka 30 ya bongo Fleva huko Zanzibar
MARA VAAP! BASATA HAWA HAPA
YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA)
TAARIFA KWA UMMA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linatoa taarifa kwa umma kuhusu maamuzi yaliyotolewa dhidi ya Godfrey Tumaini (Dudubaya) msanii, pamoja na Mratibu Mkuu wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Flava.
1. Godfrey Tumaini (Dudubaya)
Mnamo tarehe 19 Septemba, 2026 katika Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Flava lililofanyika katika Viwanja vya General Tyre, jijini Arusha Msanii husika wakati akitumbuiza hakuzingatia Mwongozo wa maadili katika kazi za sanaa. Aidha katika tukio hilo msanii alitenda kosa ambalo linavunja heshima ya msikilizaji au mtazamaji, kinyume na Kanuni ya 20(a) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, Tangazo la Serikali Na. 137 la tarehe 22 Mei 2026.
Baraza limefanya tathmini ya utetezi wake na limejiridhisha kuwa alitenda kosa hilo kwa makusudi. Vilevile imefahamika kuwa amekuwa na desturi ya kukiuka taratibu zinazosimamia uendeshaji wa matamasha ya sanaa hapa nchini kwa makosa yanayojirudiarudia. Hivyo, kwa mujibu wa Kanuni ya 45 imeamuliwa:-
a) Kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ya BASATA katika uendeshaji wa Sanaa hapa nchini;
b) Kulipa faini ya shilingi Milioni Tatu (Tsh 3,000,000) ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya uamuzi huu;
c) Kutojihusisha na shughuli za Sanaa kwa namna yoyote ile kuanzia Tarehe ya uamuzi huu hadi pale atakapotekeleza maamuzi haya.
2. Mratibu Mkuu wa Tamasha la miaka 30 ya Bongo Flava
Mnamo tarehe 19 Septemba, 2026 katika Tamasha la Miaka 30 ya BongoFlava lililofanyika katika Viwanja vya General Tyre, jijini Arusha, Mratibu husika ameendelea kumtumia msanii Godfrey Tumaini (Dudubaya) kutumbuiza jukwaani na kufanya kosa la kimaadili kwa kutamka maneno ambayo ni kinyume na Kanuni ya 20(a) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, Tangazo la Serikali Na. 137 la tarehe 22 Mei 2026
Baraza limefanya tathmini ya utetezi wake na limejiridhisha kuwa kosa hilo lilitendeka wakati msanii husika akitumbuiza jukwaani katika tamasha hilo chini ya usimamizi wake. Aidha, mratibu husika anatakiwa kuhakikisha kuwa Jukwaa la miaka 30 ya Bongoflava linatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo ili kuepuka changamoto za kimaadili kwa watumbuizaji anaowatumia. Hivyo, kwa mujibu wa Kanuni ya 45 imeamuliwa:-
a) kuzingatia Kanuni na Miongozo ya BASATA katika uendeshaji wa matukio ya Sanaa hapa nchini;

BASATA inatoa Rai kwa Wasanii na Wadau wa Sanaa kuhakikisha wanazingatia Sheria, Kanuni, Miongozo na Maadili ya Mtanzania wanapotekeleza kazi zao za Sanaa.