Je, Makonda ni asset au liability kwa CCM?

Je, Makonda ni asset au liability kwa CCM?

Missile of the Nation

Bandiko#1 umechambua vizuri tu, niweke senti sumuni. Jibu la swali DAB ni Liability kubwa.

1. Kampeni ya ''vyeti fake''. lilikufa baada ya watu kuhoji vyeti vya Makonda. Hakuna aliyeweza kuendelea na zoezi kwasababu ilikuwa 'uonevu' kwa kuchagua wakati. Magufuli aka feli kwasababu ya Makonda. Liability

2. Makonda aliendesha kampeni zisizo na kichwa wala miguu. Zoezi la majina ya wauza madawa limekwisha bila ya mtu yoyote kufunguliwa mashtaka, ilikuwa uonevu uliopaka uchafu serikali ya Magufuli. Liability

3. Makonda akaanzisha zoezi la la kupima tezi dume lililofeli kabla ya kuanza. JPM akaonekanawa ajabu. Liability

4. Makonda akaleta zoezi la watoto wasio na baba bila hata kujua suala hilo ni ''social na si political' zoezi likafeli, Magufuli akabeba msalaba kwasababu ni kijana wake. Liability

5. Makonda alivamia vituo vya TV . Magufuli akamlinda bila kutathmini akaubeba uozo wake Liability

6. Tuhuma za Viroba coco beach anahusishwa na kutuhumiwa kutokuwepo Dar es Salaam siku ya Tundu Lissu
Si Makonda ndiye aliyewezesha kupatikana kwa Roma Mkatoliki!

Makonda hajakanusha wala kwenda mahakamani. Tuhuma '' zilitoa mashaka' alitumwa- Liability

7. Majuzi tu kaendesha kampeni za chama na kuitia Serikali hasara ya V8 10 katika ajali.
Watu wanamuuliza Mh Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM , kulikoni? Rais SSH anabeba 'msalaba' - Liability

Orodha ni ndefu, hakuna shaka SSH anamrudisha serikali kiaina.

Baada ya ku test kina cha maji ameona kuna uwezekano, nakuhakikishia hii ni njia ya kumrudisha Serikalini.
Ni karata mbovu sana anacheza Rais na itamgharimu kisiasa, at any moment Makonda ni Liability

Makonda hana charisma, influence au political persuasion. Nguvu yake ni ''Bullying'

Mikutano yake inakuwa organized kwa fear ndio maana uliona magari 10 ya serikali yakipata ajali.
Think about this, hivi DMO (Daktari wa Mkoa) anawajibikaje kwa mwenezi wa chama? ni bullying tu.

Kauli yake wakati wa kupokea ndege ''kuna wapuuzi wanataka kumtenga mama na Magufuli' ilikuwa ushahidi wa ''bullying' lakini pia Rais SSH aliona ni Liability kwasababu Magufuli ha-fit katika 4Rs!

Huwezi kumhusisha Magufuli halafu ukabaki na 4Rs , DAB anataka hilo liwe Mwenyekiti anajitenga naye.

Kibaya, Rais SSH amempleka Arusha, tukijua wakati wa Msiba wa Mzee Reginald Mengi Makonda alitoa kauli ya kuudhi kuhusu Kaskazini hadi Bushiru Ally akaomba Msamaha. Pia alikuwa 'mpambe ' wa JPM aliyechukia kanda hiyo. Nina uhakika hata pata ushirikiano kutoka kanda ya Kaskazini.

Mh Rais, SSH kwanini wasaidizi wako hawakuliona hili? huyu kijana ni Liability, 'will drag you down'

JokaKuu Tindo Pascal Mayalla Mag3
 
Wadau nimekuwa napitia matukio mbalimbali ya Bw Bashite ya Siku za nyuma. Miongoni mwa Matukio yalionisikitisha ni pamoja na haya Mawili aliyoyafanya kwa WAZEE wetu VIONGOZI wakubwa Walioitumikia nchi hii na CHAMA cha CCM ambacho leo kinamlea Bw. Bashite.

Tukio la kwanza ambalo ningependa kujua ni:

1. Kwanini Bw. Bashite alimpiga Mzee WARIOBA Waziri Mkuu Mstaafu?
2. Kwanini Bw. Bashite alimdhalilisha Mzee LOWASSA Waziri Mkuu Mstaafu kuwa Katelekeza Mtoto kumbe sio kweli?
 
Wakati Mzee Warioba anapigwa, his body guard (mlinzi wake) alikuwa wapi?
 
1713852003014.png


Makonda ana laana ya asili. Kumpiga baba yako hata uende wapi hutoboi.
 
Hajawahi mpiga. Walimtoa nje mzee, alikua analeta vurugu tu pale.
Ila simkubali kabisa makonda.
Nimekujibu maana umeua thread kwa kusema kitu kisicho kua na fact.
 
Katika maamuzi ya hovyo ambayo CCM wamewahi kuyafanya ni kumrudisha huyu kijana katika nafasi kubwa sana ndani ya chama.

Pengine ni katika hali ya kutapatapa kisiasa kwa rais Samia na Pengine kwa sababu ya urafiki wake na Makonda uliomsukuma Rais atumie nguvu na ushawishi wake kumrudisha Makonda katika ulingo wa kisiasa.

Inafahamika vizuri kuwa Tangu Makonda apendekeze kwa wakubwa wa CCM na watawala katika bunge la katiba kuwa Wamfanye Samia kuwa mgombea mwenza wa mgombea uraisi wa mwaka 2015, nadhani Samia amekuwa akiamini kuwa sababu mojawapo ya nyota yake ya kisiasa kung'aa ni pendekezo la Makonda. Hivyo kutoka katika uvungu wa moyo wake amekuwa akidhani kuwa ana deni kwa huyo kijana.

Hata hivyo Samia asichokifahamu, au pengine anakifahamu lakini ameamua kufumba macho kwa sababu ya kumpenda Makonda ni kwamba, Katika watu waliomharibia magufuli na kuiba mtaji mkubwa wa kisiasa wa Magufuli ni huyu Makonda. Makonda alifanya mambo ya ajabu mno na Magufuli alitumia mtaji wake binafsi wa kisiasa kumlinda na kumkingia kifua huyu kijana. Hii ilipelekea watu kuanza kumchukia Magufuli na kumsema vibaya sana. Umaarufu wa Magufuli umeongezeka zaidi baada ya kifo chake kuliko wakati wa uhai wake hasa kipindi Makonda anafanya mambo ya ajabuajabu.

1. Tukio la Jaribio la Mauaji ya Lissu.
Tundu Lissu amekuwa akimtuhumu Makonda katika jaribio la mauaji dhidi yake, hizi ni allegations nzito sana. Haipaswi hata kidogo kwa Chama kikubwa tena kinachoendesha serikali kumpa mtu kama Makonda dhamana kubwa katika chama chao wakati ana tuhuma nzito kama hizo. Hii inatoa taswira kuwa chama cha CCM nacho kinalinda uhalifu, na kinaunga mkono kilichomkuta Lissu. Otherwise badala ya kumuweka huyu Makonda katika uchunguzi, chenyewe kinamfanya kuwa msemaji wake.

2. Tuhuma za kudhulumu nyumba ya GSM
Pia kuna tuhuma, zimetolewa na Lissu kuwa Makonda amewahi kutumia jina la Rais (Magufuli) ili kufanya utapeli. Mtu aliyetumia nafasi yake ya mkuu wa mkoa na ukaribu na raisi kudhulumu, utampaje mtu kama huyo nafasi kubwa katika chama?. Unampa mtu kama huyu kukisemea chama ili akisemee nini haswa?. Ni dhahiri vetting ya CCM ni ya hovyo au haijielewi kuwa inataka nini, au iko desperate kupata watu wanaoweza kukisaidia kwa merit

3. Kuvamia Studio za Clouds FM kwa silaha.
Mtu alionekana katika video, akivamia studio kinyume cha sheria, akakingiwa kifua na mamlaka ya urais, lakini bado akaendelea kufanya mambo ya ajabuajabu. Huyu anafaaje kuwa Msemaji wa Chama. Inamaana CCM nacho kinataka kutwambia kuwa nacho ni chama cha THUGS?. Uteuzi wa Makonda kimsingi umeifunua CCM na kuionyesha kuwa ni chama ambacho ni muflisi

4. Kuendesha zoezi la Kumsingizia Lowasa kutelekeza Mtoto
Huyu Makonda ndiye aliitisha zoezi la eti wanawake wakawashitaki wanaume waliowatelekezea watoto. na hapo anatokea binti mwenye miaka kibao eti anaenda kushitaki kwa mkuu wa mkoa kuwa katelekezwa na waziri mkuu mstaafu. mazoezi ya kucheza na hisia za watu, kuwatumia watu kisiasa, kudhalilisha watu. Huyu anawezaje kuwa msemaji wa chama kikubwa kinachoongoza dola?

5. Mtu aliyetajwa na katibu mkuu mstaafu wa CCM kuwa anapwaya katika uongozi
Bashiru Ally aliwahi kutamka wazi kuwa huyu kijana bado hajakomaa katika uongozi, kuna mambo anayafanya ni kinyume cha maadili ya uongozi. Ni lini huyu Makonda karudi tena darasani ili kupigwa tena msasa wa uongozi ili kujua maaili ya uongozi?

MAONI YANGU:
1. Samia tangu alipoingia Madarakani alikuwa anatafuta namna ya kumrudisha Makonda katika mfumo kwa sababu ya urafiki tu lakini alikuwa anasubirisubiri kwanza kutafuta timing.

2. Upepo wa bandari ulipokuwa mkubwa akaona hiyo ni fursa ya kumrudisha swahiba wake katika mfumo lakini wakati huohuo kujaribu kuspin mjadala wa kitaifa wa bandari.

3. Samia anadhani kwa kuwa Makonda alikuwa karibu na Magufuli basi Makonda ataleta upako wa kimagufuli kwake, yaani by virtue ya watu wa kawaida kumkubali Magufuli, basi watafurahi na kumuongezea ratings akimpa nafasi Makonda.

4. Samia anadhani anaweza kupata uungwaji mkono kanda ya ziwa kwa kuwasogeza watu wa kanda ya ziwa katika nafasi kadha wa kadha. Hiyo ndo sababu mojawapo ya kuwaleta karibu akina Biteko na makonda , lakini hata hivyo sidhani kama hili litamsaidia.

NINACHOKIONA KINAFUATA

1. Upepo wa Makonda utakata muda si mrefu, maana aina yake ya ufanyaji siasa ni usanii na vichekesho. Sanaa zinaweza kulipa kwa muda mfupi lakini baadae wananchi wanataka vitu serious. Wakati bei ya sukari inapanda, watu wana shida ya maji safi na salama, umeme wa manati, ajira kwa vijana tabu, halafu unawaletea wananchi sanaa. Itabackfire tu. CCM waliitaji mtu anayeweza kuelezea Issues za serikali yao vizuri, mwenye charisma, mwenye upeo.

2. It is a matter of time kabla Makonda hajarudi katika ngozi yake ya asili. Kama Samia asipomdhibiti mapema huyu kijana atageuka soon kuwa liability kwake kama alivyokuwa katika siku za mwisho za utawala wa Magufuli. Ni kweli Makonda aanajua sana kumteka mtu na kumfanya rafiki wa kuaminika. Alifanya hivyo kwa Mzee Sitta, Membe, Familia ya Jakaya, Familia ya Magufuli na sasa Samia. Samia asidhani anamjua Makonda saaaana kuliko Riziwani. Na sote tunajua kilichomkuta Riziwani baada ya Makonda kufanikiwa kumuweka JPM kiganjani. Je Samia ataweza kulirudisha jini katika chupa?- Time will tell
Braza, ukimuacha huyu jamaa ambaye hata kumjadili ni kumuongezea kiki, kuna suala muhimu mno linaloibuliwa na aina ya 'kiongozi' wa aina yake. Kama Taifa tumefikaje hapa? Licha ya kuwepo kwa utitiri wa UJINGA unao-ongezeka kila kukicha katika jumuiya zetu (sina takwimu zinazijibu hili) wapo pia Watanzania ambao sio zero brains hata kidogo. Wapo wengi na hili pia sihitaji kutoa takwimu zake. Linalofikirisha ni KWA NINI ZERO BRAINS wameshika hatamu? Zero brains wa rangi ya kijani, wengine manjano ndani ya madaraka ya rangi hizo hizo, kana kwamba kuwa na cheti cha 'USIFURI' ni kigezo na sifa toshelezi kua mwenzao?
 
Back
Top Bottom