Je, Makonda ni asset au liability kwa CCM?

Missile of the Nation

Bandiko#1 umechambua vizuri tu, niweke senti sumuni. Jibu la swali DAB ni Liability kubwa.

1. Kampeni ya ''vyeti fake''. lilikufa baada ya watu kuhoji vyeti vya Makonda. Hakuna aliyeweza kuendelea na zoezi kwasababu ilikuwa 'uonevu' kwa kuchagua wakati. Magufuli aka feli kwasababu ya Makonda. Liability

2. Makonda aliendesha kampeni zisizo na kichwa wala miguu. Zoezi la majina ya wauza madawa limekwisha bila ya mtu yoyote kufunguliwa mashtaka, ilikuwa uonevu uliopaka uchafu serikali ya Magufuli. Liability

3. Makonda akaanzisha zoezi la la kupima tezi dume lililofeli kabla ya kuanza. JPM akaonekanawa ajabu. Liability

4. Makonda akaleta zoezi la watoto wasio na baba bila hata kujua suala hilo ni ''social na si political' zoezi likafeli, Magufuli akabeba msalaba kwasababu ni kijana wake. Liability

5. Makonda alivamia vituo vya TV . Magufuli akamlinda bila kutathmini akaubeba uozo wake Liability

6. Tuhuma za Viroba coco beach anahusishwa na kutuhumiwa kutokuwepo Dar es Salaam siku ya Tundu Lissu
Si Makonda ndiye aliyewezesha kupatikana kwa Roma Mkatoliki!

Makonda hajakanusha wala kwenda mahakamani. Tuhuma '' zilitoa mashaka' alitumwa- Liability

7. Majuzi tu kaendesha kampeni za chama na kuitia Serikali hasara ya V8 10 katika ajali.
Watu wanamuuliza Mh Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM , kulikoni? Rais SSH anabeba 'msalaba' - Liability

Orodha ni ndefu, hakuna shaka SSH anamrudisha serikali kiaina.

Baada ya ku test kina cha maji ameona kuna uwezekano, nakuhakikishia hii ni njia ya kumrudisha Serikalini.
Ni karata mbovu sana anacheza Rais na itamgharimu kisiasa, at any moment Makonda ni Liability

Makonda hana charisma, influence au political persuasion. Nguvu yake ni ''Bullying'

Mikutano yake inakuwa organized kwa fear ndio maana uliona magari 10 ya serikali yakipata ajali.
Think about this, hivi DMO (Daktari wa Mkoa) anawajibikaje kwa mwenezi wa chama? ni bullying tu.

Kauli yake wakati wa kupokea ndege ''kuna wapuuzi wanataka kumtenga mama na Magufuli' ilikuwa ushahidi wa ''bullying' lakini pia Rais SSH aliona ni Liability kwasababu Magufuli ha-fit katika 4Rs!

Huwezi kumhusisha Magufuli halafu ukabaki na 4Rs , DAB anataka hilo liwe Mwenyekiti anajitenga naye.

Kibaya, Rais SSH amempleka Arusha, tukijua wakati wa Msiba wa Mzee Reginald Mengi Makonda alitoa kauli ya kuudhi kuhusu Kaskazini hadi Bushiru Ally akaomba Msamaha. Pia alikuwa 'mpambe ' wa JPM aliyechukia kanda hiyo. Nina uhakika hata pata ushirikiano kutoka kanda ya Kaskazini.

Mh Rais, SSH kwanini wasaidizi wako hawakuliona hili? huyu kijana ni Liability, 'will drag you down'

JokaKuu Tindo Pascal Mayalla Mag3
 
Wadau nimekuwa napitia matukio mbalimbali ya Bw Bashite ya Siku za nyuma. Miongoni mwa Matukio yalionisikitisha ni pamoja na haya Mawili aliyoyafanya kwa WAZEE wetu VIONGOZI wakubwa Walioitumikia nchi hii na CHAMA cha CCM ambacho leo kinamlea Bw. Bashite.

Tukio la kwanza ambalo ningependa kujua ni:

1. Kwanini Bw. Bashite alimpiga Mzee WARIOBA Waziri Mkuu Mstaafu?
2. Kwanini Bw. Bashite alimdhalilisha Mzee LOWASSA Waziri Mkuu Mstaafu kuwa Katelekeza Mtoto kumbe sio kweli?
 
Wakati Mzee Warioba anapigwa, his body guard (mlinzi wake) alikuwa wapi?
 


Makonda ana laana ya asili. Kumpiga baba yako hata uende wapi hutoboi.
 
Hajawahi mpiga. Walimtoa nje mzee, alikua analeta vurugu tu pale.
Ila simkubali kabisa makonda.
Nimekujibu maana umeua thread kwa kusema kitu kisicho kua na fact.
 
Braza, ukimuacha huyu jamaa ambaye hata kumjadili ni kumuongezea kiki, kuna suala muhimu mno linaloibuliwa na aina ya 'kiongozi' wa aina yake. Kama Taifa tumefikaje hapa? Licha ya kuwepo kwa utitiri wa UJINGA unao-ongezeka kila kukicha katika jumuiya zetu (sina takwimu zinazijibu hili) wapo pia Watanzania ambao sio zero brains hata kidogo. Wapo wengi na hili pia sihitaji kutoa takwimu zake. Linalofikirisha ni KWA NINI ZERO BRAINS wameshika hatamu? Zero brains wa rangi ya kijani, wengine manjano ndani ya madaraka ya rangi hizo hizo, kana kwamba kuwa na cheti cha 'USIFURI' ni kigezo na sifa toshelezi kua mwenzao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…