Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 761
- 6,985
Moja ya changamoto kubwa inayokabili watawala wetu nikuaminishwa kwamba usipokuwa Mwenyekiti wa chama hautoweza kuongoza Nchi. Hii ni doctrine imewekwa kulinda maslahi ya chama na kumfanya Rais awe na jukumu lakulinda chama. Kulinda chama hakuhitaji haki maana ukisimamia haki hakuna namna chama kitabaki hai, lazima uibe na kuumiza wapinzani wako wenye nguvu ndani na nje hivyo ndani ya chama hakuna haki. Hasa ni vipi Rais atasimamia haki za wananchi nakuvunja haki kwa maslahi ya chama? Lazima atafeli
Hoja nyingine au doctrine nyingine inayotumika kuwaumiza wenyeviti nikuminishwa kwamba hawatakiwi chama kifie mikononi mwao, utasikia chama kinafia mikononi mwako. Tukumbuke JK walivyomsumbua kwakumwaminisha kwamba anapaswa kuhakikisha chama hakifi Jambo lililopelekea kumleta mgombea ambaye alikuja kusimamia chama kisife huku akiliua Taifa. Doctrine hii kila Mwenyekiti anayo na ukiikubali umekubali kuacha kusimamia nchi.
Jambo la tatu ni ushawishi wa wajumbe wanaonufaika na urais wake, Wapo Wana CCM biashara zao zinakwenda kwa Rais kuwa Mwenyekiti wa chama, vijana wao wanapata ajira na chama kinakuwa sehemu ya serikali hivyo kumwondoa Rais kwenye kiti Cha Mwenyekiti nakumkabidhi mtu asiye na mamlaka ya nchi itawiwia vigumu kumlilia shida zao. Kwa tafsiri nyingine kuwa Mwenyekiti wa CCM bila mamlaka ya nchi hauna tija kwani watu hawataki misaada na nafuu zakichama wanataka nafuu za kiserikali ambazo ni Kodi, miradi na biashara zao. Mwenyekiti asiye Rais hana tija kwa wanamtandao.
Nne, Rais akijiondoa kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa chama itakuwa vigumu wenye chama kuingia kwenye dola na ikulu. Yapo Mambo yakichama yanaenda kwa mtu flani kusema Rais kaagiza badala yakusema mwenyekiti kaagiza. Watu wanataka wasiseme Mwenyekiti kasema Bali waseme Samia Suluhu kasema na kwa nafasi ya Mwenyekiti wa chama wewe unayeambiwa itakulazimu utekeleze ukiamini Samia kaagiza Kama Rais kumbe kaagiza Kama Mwenyekiti wa chama. Hivyo mama analazimika awe mwenyekiti Mambo yaende.
Kama Mhe. Rais anataka kufanya kazi asikubali kuwa Mwenyekiti wa chama, abaki kuwa Rais wa nchi. Nchi inahitaji vyombo kwenda mbele na si chama Cha siasa. Chama ni mlango wakupata madaraka na si njia yakuongoza nchi. Lakini pia usiwe na nia yakugombea awamu mbili. Maisha yanahitaji Jambo dogo lenye tija kuliko mrundikano wa mambo yasiyo na tija.