Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Tunaweza kujiuliza maswali magumu kuhusu usalama wa viongozi wa chama cha mapinduzi. Lakini pia ikawa hoja ya usalama wa viongozi na watu maarufu nchini.
Sina uhakika kama anayetukanwa ni Rais au ni Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi lakini najiuliza huko wapi usalama wa wanaotuhumiwa?
Je, anayetuhumu taarifa anapata wapi?
Anayempa taarifa ana malengo gani?
Anayeruhusu kuletewa taarifa alipewa hiyo kazi na nani?
Aliyempa kazi alimwambia aripoti kwa njia gani?
Tusipojiuliza maswali haya na kutaka majibu tutarudi kule tulipotoka ambapo mtu alikuwa anamtuhumu, anakamata na wakati mwingine anaeliminate.
Wengi walipotezwa kwa tuhuma kwa msingi kwamba tuhuma zinatosha kuhukumu na hukumu yake inatolewa na yule anayetuhumu.
Tulidhani tumetoka huko ila upo uwezekano kwa ukimya wa Mamlaka hata kazi ya Mungu huko tuendako itaonekana ni kazi ya binadamu.
Niwaombe viongozi waliopewa dhamana wajadiliane ndani pale wanapoona upo uvunjifu wa maadili au sheria miongoni mwao. Tanzania tukianza kutangaza hofu hasa kwenye ukanda wa utalii hata hao watalii watagoma kwenda. Kama waziri anahujumu juhudi za mwenyekiti na Mteule wake unategemea huyo waziri atafurahi watalii kuongezeka nchni?
Asipopendezwa na juhudi za Rais na akimaliza kutoa rushwa watu wamtukane atakwenda mbali zaidi na kuhujumu juhudi zake. Swali lakujiuliza ni kweli haya yanayosemwa au mtu katunga stori za kisiasa bila kuangalia athari zake kiuchumi?
Tunaamini watalii watakuja kwenye nchi ambayo Mawaziri wameshindwa kumheshimu Rais?