Je, mbinguni kutakua na wanyama kama Simba, Chui, Swala au Mamba, na je wataishi pamoja bila kulana?

Je, mbinguni kutakua na wanyama kama Simba, Chui, Swala au Mamba, na je wataishi pamoja bila kulana?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Je, mbinguni ambapo tunaahidiwa kutakua na perfect life, hakuna kifo, hakuna kulia, hakuna njaa, ni furaha mwanzo mwisho, ni kuimba na kuabudu mwanzo mwisho wanyamapori kama simba, chui, swala, nyumbu na wengine watakuwepo? Je wataishi kwa upendo bila kulana, watashirikiana kila kitu?

Je, wao wanyama kama watakuwepo watakua na wao kazi yao ni kuimba na kuabudu siku zote bila kikomo? Je wanyama hao watakua wanazaliana?

Kama wanyama wataenda kushirikiana huko mbinguni, je huku Duniani nani aliwagombanisha kwa sababu hawaongei, hata wale wa species moja kama simba, paka, mbwa, chui hawaelewani wakati wale wanaokula majani wanaelewana.

Naomba kufahamu mbinguni kutakuwaje ama kukoje, nasikia tu kua kuna misosi imeandaliwa kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu (hizo hotpot ni balaa). Angalau waislamu wanatoa picha ndogo ya mbinguni kukoje, wanawake warembo na pombe, hapo kwa wanawake wamenipata, nitajilia vimwana😂. Vimwana wa mbinguni mjiandae tafadhali (nasikia hakuna cha alkasusu, viagra wala vumbi la congo, ni mpini mwanzo mwisho hata goli 12)

Je, mbinguni kukoje?

Ahsante.
 
Sijui niwe mchungaji tu maana naona inalipa sana hii biashara!.. unawezaje kuamini kuwa kuna mbinguni..😅
Ati utapewa vimwana! How..?
Ati Simba na chui watakuwa kama ng'ombe tu! How..?
Ati kutakuwa na maakuli hivyo na kukata gogo kutakuwepo Sasa..😂

Mkuu Kama unafikiri huko mbinguni ni salama futa hilo wazo maana huu ubaya tunaouita ubaya hapa duniani,kwa mujibu wa vitabu husika uasi ama ubaya ulianzia hukohuko unapopaita mbinguni!! Na chaajabu aliesema anakupenda ndio huyohuyo aliemtupa shetani duniani!!.

He he! Ndugu achana na hizo theory hakuna Cha mbinguni wala motoni ukifa ndo kwisha habari yako!.. hizi habari ni sehemu tu ya evolution of man!.. huko mbeleni sana watakuja kutusoma historia yetu ya Sasa kuwa tulikuwa tukiomba na kuabudu na kuamini kuna mbinguni na peponi!!.

Wewe ni Kama kabla ya kuzaliwa tu hukuwepo na baadae ukawepo na Kisha utakufa it means hali ya kutokuwepo inajirudia tena so hakuna cha mbingu wala mbangu au mbinguana!! Chagua tu kuishi kiuweledi kwa kufuata misingi ya ufahamu lkn usihofu kuhusu mbinguni nothing huko ni ku collapse kwa ufahamu wa mwanadam tu na kutokujua what is what ndio maana anatapatapa!.
 
Kwenye safina ya Nuhu kwani Simba walifungashiwa lunch packs?

Ina tegemea na imani yako. Kuna imani nyingine mbinguni ni hapa hapa, nyingine ni juu huko ila hawaendi na miili hii ya nyama hivyo swala la pisi kali na mivinyo halipo n.k sasa wewe imani yako ni ipi?
 
Hoja sio imani yangu, hoja ni mbinguni kukoje?
 
Sijui niwe mchungaji tu maana naona inalipa sana hii biashara!.. unawezaje kuamini kuwa kuna mbinguni..😅
Ati utapewa vimwana! How..?
Ati Simba na chui watakuwa kama ng'ombe tu! How..?
Ati kutakuwa na maakuli hivyo na kukata gogo kutakuwepo Sasa..😂
Wewe unaweza kututhibitishia kwamba kuwa hakuna "Mbinguni" ?
 
Wewe unaweza kututhibitishia kwamba kuwa hakuna "Mbinguni" ?
Nitakuwa mpuuzi wa mwisho kukuthibitishia kitu ambacho hakipo huku nyinyi mnaosema kipo hamjakithibitisha kuwa kipo..!
So ndugu usiumize Sana kichwa fata njia yako tu.
 
Nitakuwa mpuuzi wa mwisho kukuthibitishia kitu ambacho hakipo huku nyinyi mnaosema kipo hamjakithibitisha kuwa kipo..!
So ndugu usiumize Sana kichwa fata njia yako tu.
Unakuwa mpuuzi zaidi kuandika juu ya jambo ambalo huwezi kulithibitisha. Swali rahisi sana ambalo huwezi kulijbu ni Kutuambia sisi umejuaje kama hakuna mbinguni ? Hili ni swali rahisi ambalo mpaka unakufa huwezi kulijibu.

Mimi ukiweza tu kuniambia umejuaje,hakuna Mbinguni, mimi hii ID nitaomba uongozi wa "jf",waifute na wewe utakuwa shahidi.

Unataka uthibitishiwe mara ngapi juu ya kuwepo "Mbinguni" ? Kama unakubali Mbingu ipo basi na Mbinguni kupo, kama ilivyo "Ardhi" na "Ardhini".
 
Unakuwa mpuuzi zaidi kuandika juu ya jambo ambalo huwezi kulithibitisha. Swali rahisi sana ambalo huwezi kulijua ni Kutuambia sisi umejuaje kama hakuna mbinguni ? Hili ni swali rahisi ambalo mpaka unakufa huwezi kulijibu.

Mimi ukiweza tu kuniambia umejuaje,hakuna Mbinguni, mimi hii ID nitaomba uongozi wa "jf",waifute na wewe utakuwa shahidi.

Unataka uthibitishiwe mara ngapi juu ya kuwepo "Mbinguni" ? Kama unakubali Mbingu ipo basi na Mbinguni kupo, kama ilivyo "Ardhi" na "Ardhini".
Tusichoshane wewe kwa mijadala isiyoisha baki unavyojua na usubiri ukifa uende huko mbinguni kwenye mbingu sasa ukapewe na pisi kali,ukale na kusaza ukaabudu na kusifu.. kwako mbinguni kupo basi elewa kwangu mbinguni hakupo unasumbuka na nini Sasa si uishi tu.. sikufaidishi chochote hata nisipoenda huko mbinguni so we pumua tu.
 
Mbinguni hakuna kuabudu huko wala kusifu.

Hakuna anae sumbuka hapa, bali nakuonyesha ni ujinga kuandika mambo usiyo kuwa na ujuzi nayo wala kutuambia umejuaje mambo hayo. Ujinga huu huwa nauona "jf" tu.
 
We kamongo kweli wewe!.. au utakuwa na kitabu chako tu kichwani kwahiyo kwa mujibu wa vitabu vyenu Kama hakuna kuabudu na kusifu Kuna nini kupiga selfie..??

We unafahamu nini kama kunithibitishia ndo kuandika kuwa kwa kuwa mbingu ipo basi na mbinguni kupo..😂😂
Mkuu tusichoshane nawe hakuna unachokijua chakufanya kila mmoja afanye anachokiweza tu.
 
[/QUOTE]
Maisha baada ya kifo/ mbinguni/ Akhera
Wanyama hawatakuwepo
Kule kutakuwa na Wanadam na Majini
Hawa ndio viumbe watakaohukumiwa aidha waende motoni au peponi
 
Usiulizie habari za mahali ambako hutofika, huko wacha mie ndo niulizie maana kwenda huko kwangu ni "Given"
 
Maisha baada ya kifo/ mbinguni/ Akhera
Wanyama hawatakuwepo
Kule kutakuwa na Wanadam na Majini
Hawa ndio viumbe watakaohukumiwa aidha waende motoni au peponi
So nikitaka nile kuku watatoka wapi?
 
Back
Top Bottom