Je, mbinguni kutakua na wanyama kama Simba, Chui, Swala au Mamba, na je wataishi pamoja bila kulana?

Je, mbinguni kutakua na wanyama kama Simba, Chui, Swala au Mamba, na je wataishi pamoja bila kulana?

Watu wadunian bana ..et wanaulizia mambo ya mbinguni dunian hahahaa.. Aya bana endeleen kutoa majbu
 
Kuna dada mmoja vipimo vya Dr vilionyesha amekufa baadae akafufuka/akaamka hapo hospitalini... Ndo akawa anasimulia Mambo ya mbinguni.... Anasema mbinguni ni hatari hakuna mahala pa kufananisha ni pazuri Sana na Kuna vibes Kama zote Kila unachokitaka kipo iwapo duniani ukiwa mtu Safi... So wew mzee wa Mizigo duniani ikaushie tu ili ukaifaidi Ile mizigo ya shekh kipozeo
 
Kuna dada mmoja vipimo vya Dr vilionyesha amekufa baadae akafufuka/akaamka hapo hospitalini... Ndo akawa anasimulia Mambo ya mbinguni.... Anasema mbinguni ni hatari hakuna mahala pa kufananisha ni pazuri Sana na Kuna vibes Kama zote Kila unachokitaka kipo iwapo duniani ukiwa mtu Safi... So wew mzee wa Mizigo duniani ikaushie tu ili ukaifaidi Ile mizigo ya shekh kipozeo

Itakuwa huyu dada Alikunywa bia nyingi akapata fofo ya usingizi ..hizi ni ndoto kama ndoto zingine
 
Dhana ya mbingu ni ya kiroho zaidi ya mwili

Jr[emoji769]
Mbinguni kuna Roho na Mwili. Haviachani viwili. Hata ukifa leo hii, ukizikwa Roho inarudi kwenye mwili, na maisha yanaendelea kama kawaida, tofauti ya maisha ya kaburini ni kuwa hakuna kutafuta pesa wala mfano wake, zaidi ya kuruzukiwa kutokana na kile ulichokitenda huku ukisubiri hukumu.
 
Hats huko mbinguni wabishi wa kumpinga mungu kwa hoja kama lissu watakuwepo
Hivyo tutegemee mengi tufikapo huko
Na hata itafikia hatua watu watampinga kuwa hafai na wanamtaka mwingine
 
MBINGUNI NI KWA AJILI YA AKINA NANI?

Tumezoea kusikia kuwa watu wazuri mara wanapokufa muda huo huo wanaenda mbinguni.
Utasikia watu wakihimizana kutenda mema ili mwisho wa siku waende mbinguni.

Hii ni habari inayoonekana kama ni ya kufurahisha ila sivyo neno la Mungu linavyofundisha.
Acha tuone:

Mtu anapokufa awe mzuri au mbaya, uhai wake unakuwa umekoma. Hawi na ufahamu au na kumbukumbu tena.
Mhubiri 9:5 - kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

Mwanadamu katika hali ya kifo (anapokufa) hawi tofauti na mnyama mwingine yeyote anavyokufa. Wote wanageuka mavumbi.
Mhubiri : 3 : 19 - Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama;
Mhubiri : 3 : 20 - Wote huendea mahali pamoja; WOTE hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.

Hivi ndivyo hata Adamu alivyoambiwa na Mungu kuwa atairudia ardhi. Mwanzo 3:19 - kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

Fundisho la kwamba mtu mzuri mara anapokufa anaenda mbinguni si la kimungu, hata Yesu mwenyewe anapinga hilo.
Yohana 3:13 - Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu(Yesu).

Yesu peke yake ndiye aliyepaa kurudi mbinguni kwa maana awali alikuwa wa mbinguni.
Hata mara alipokufa, Yesu alienda kuzimu kwanza ambako ndiko makao ya wafu kabla ya kufufuliwa. Alipaa baadaye, siku ya arobaini kurudi kwenye makao yake yeye ya awali.

Mpango wa Mungu ulikuwa Adamu akae hapa duniani akianzia pale Eden na kuzaana na kuijaza dunia. Mpango huu haujabadilika. Mungu aliendelea kutembea na wanadamu wema waliofuata baada ya Adamu, watu kama Abel, Enoko Ibrahimu, Isaka, Yakobo na wengine wengi waliokuwa wanaisikiliza sauti ya Mungu.

Watu wote wema(wenye haki) watakujakurithi kile ambacho Adamu na hawa walipoteza. Hilo ndio lilimleta Yesu duniani, ili kurudisha ule uhusiano wa Mungu na mwanadamu, aliopoteza Adamu.

Yeyote atakayempokea Yesu, hatapotea bali atakuwa na uzima wa milele, kama Mungu alivyokuwa amekusudia kwa Adamu.

Hivyo kuja kwa Yesu, ni kwa ajili ya kurejesha ule mpango wa Mungu kwa mwanadamu.
Yeye anasimama kama Adamu mwingine asiye na dhambi.
1 Wakorintho 15:45 - Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. (yaani Yesu.

Mungu akipanga jambo kwa wanadamu lazima afanikishe hata kama wengine wataishia njiani kama Adamu na Hawa.

Fikiria habari ya wana waisrael. Mungu aliwatoa Misri maelfu ya watu ila wakiwa njiani walikuwa wakimchukiza Mungu. Ni watu wawili tu kati ya wale walioanzia safari Misri, Kalebu na Yoshua ndio walofanikiwa kufika Kaanan.

Mambo yote Mungu aliyomuahidi Adamu, hayatapita bure, yatarithiwa na wale watakaotii sauti yake Mungu.
Isaya 55:11 - ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.


Ingelikua kichekesho kwamba Adamu baada ya kumuasi Mungu ndiposa(Mungu) aruhusu uzao wa Adamu upate kibali cha kuhamishiwa mbinguni.
Ingekuwa hivyo! basi, dhana ya “mbingu ni mbingu za Bwana na dunia amewapa wanadamu” ingelikuwa haina maana, na Mungu angelikuwa ameshindwa na shetani, kutimiza ahadi yake yakuwapa wanadamu nchi(dunia).
Zaburi 115:16 - Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu.

Ukweli ni kwamba dunia(nchi), Mungu amewapa wanadamu. Hakuna wa kumzuia Mungu kutekeleza hili.

Tangu awali Mungu ameumba aina mbili za miili. Miili ya wale watakaokaa mbinguni na miili ya watakaokaa duniani. Kila mwili una uzuri(fahari) yake

Wanadamu wasiokuwa na ujuzi sahihi wa Mungu wanatamani kuwa na miili kama ya malaika, na hata malaika waovu wanatamani kuwa na miili kama ya wanadamu, ila Mungu sii mjinga amepanga hiyo miili kwa jinsi ya kufaa.

Ona :1 Wakorintho 15:40 - Tena kuna miili ya mbinguni(celestial bodies), na miili ya duniani(terrestrial bodies); lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.

Tuendelee.
Unakumbuka habari za Lazaro wa Bethania? Alikuwa rafiki wa Yesu. Ikiwa basi watu wazuri wakifa walikuwa wakienda mbinguni Yesu asingemlilia Lazaro alipokufa, angefurahi na angewanyamazisha wengine wasilie, kwamba Lazaro amewatangulia kwenda kwa Mungu(kama watumishi wengine wanavyohubiri). Ila Yesu alilia.
Yohana : 11 : 35 - Yesu akalia machozi.

Pia kitendo cha kumrudisha Lazaro duniani kwa kumfufua ilhali tayari alikuwa basi kwa Mungu, kingekuwa sio cha haki.

Hapa nasisitiza kwamba Lazaro hakuwa popote akiwa na ufahamu, maandiko yanasema, wafu hawajui lolote.
Ndio maana Lazaro alipofufuliwa kulikuwa na furaha kuu.

Uhai ni zawadi kubwa kwetu kutoka kwa Mungu.

Unaweza kusikia watu wakisema, fulani alipaa mbinguni, kama akina Elia nk, ila mwalimu wetu mkuu, Yesu Kristo, aliyekuja baada ya hao akina Elia anasema HAKUNA aliyewahi kupaa mbinguni ila yeye(Yesu).

Dokezo kuhusu Eliya:
Mungu alimuhamisha(vusha) Eliya kutoka alikokuwa, na kumpelea nchi nyingine hapa hapa duniani kabla hajafa. Njia aliyotumia Mungu ni kumpaisha angani kwa upepo wa kisulisuli, na si kwamba alimpeleka mbinguni kwenye makao yake Mungu.

Siku hizi, watu wanapopaa angani kwa ndege au helkopta si kwamba wanspaa kwenda mbinguni kwa Mungu.

Kama unaona hujaelewa vizuri hili la Elia kupaa, basi shika hili Yesu alilosema, kwamba hakuna mtu aliyewahi kupaa mbinguni ila yeye Yesu mwenyewe.

Yesu kabla hajaja duniani alikuwa anakaa mbinguni. Kama Eliya alikuwa amepaa mbinguni kwenye makao ya Mungu basi Yesu asingelisema vile, kwamba “hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye” Yohana 3:13

Mtu mzuri kama Daudi naye pia hakupaa mbinguni.
Matendo ya Mitume 2:34 - Maana Daudi hakupanda mbinguni;

Ona jinsi hata Paulo alivyojaribu kuwaelewesha watu wakati ule kwamba Daudi hakupaa mbinguni.
Matendo ya Mitume : 2 : 29 - Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo. (Matendo ya Mitume 2:34 - Maana Daudi hakupanda mbinguni😉

Habari njema na ya kufurahisha,ambayo wengi hawajaisikia ni hii:-
Zaburi 115:16 - “Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu”.

Mungu ameumba dunia ikaliwe na wanadamu. Huo ndio mpango na kusudi la Mungu. Mungu hasemagi uongo.

Duniani ndio makao ya Mwanadamu na si mbinguni.

Adamu aliambiwa wazae waongezeke watawale hapa duniani.
Mwanzo 1:28 - Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Mpango wa Mungu uko pale pale, ni Adamu na mke wake ndio walichemka, ila watu wazuri watakaosikia sauti ya Mungu watakuja kuirithi nchi na kukaa huko milele.
Zaburi 37:29 - Wenye haki watairithi nchi, Nao watakaa humo milele.

Wanadamu wataishi kwenye nchi(Duniani) na si mbinguni.

Kama wewe unatamani kwenda mbinguni wewe endelea kutamani tu ila Mungu anasema mbingu ni za kwake ila nchi ndiyo ametupa sisi wanadamu.
Rudia tena andiko la Zaburi 115:16 -

(Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu.)

Isaya 45:18 - Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba DUNIA na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na WATU; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine.

Hapa Mungu anasema aliifanya dunia ikaliwe na watu. Tunarudi pale pale Zaburi 115:16 - Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu.

Karibuni Mungu ataondoa mambo yale yote mabaya yanayomsumbua mwanadamu hapa duniani mojawapo kikiwamo kifo.
1 Wakorintho 15:26 - Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.

Dunia iliharibika na kuwa mbaya kwa sababu ya Adamu na Hawa kumsikiliza na kumtii shetani.
Mungu bado anakumbuka ahadi yake kwa wanadamu watiifu kuwa watairithi nchi, ndio maana akamtoa mwana wake pekee Yesu ili kila amwaminie asipotee bali awe na ule uzima wa milele kwenye nchi(duniani).

Wakati huo dunia itaboreshwa na kuwa nzuri kabisa kwa kuwa “lishetani” halitakuwepo tena. Hata mbinguni kutaboreshwa.
Unajua kuwa awali shetani alikuwako pia mbinguni? Mungu tayari alishaanza vita ya kumng’oa shetani kutoka huko. Shetani hayuko tena mbinguni kwa sasa, ila yuko huku duniani, ila karibuni ataondolewa.

Soma habari hii upate picha.
Ufunuo wa Yohana 12:7 - Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata NCHI, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Mapepo na majini tunayosikia, ni malaika zake shetani waliotupwa, baada ya kumuasi Mungu.

Habari njema ni kwamba watang’olewa pia huku duniani.
Mbingu na nchi, zote zitakuwa shwari
shetani atakapoondolea.
Kuna vita kuu inayokuja ya Har-magedoni Ufunuo 16:16

Ufunuo wa Yohana : 21 : 4 - Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti HAITAKUWAPO TENA; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

Watu watafurahia maisha ajabu!

Ufunuo wa Yohana : 21 : 1 - Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

Hapa kwenye andiko juu unaona pia kuwa nchi bado itakuwepo kwenye mpango wa Mungu kwa ajlli ya wanadamu, na mbingu itakuwa mpya kwa maana mbingu ile ya awali alikuweko pia shetani.

Je, ulipata kuisikia habari hii njema namna hii?

Nafikiri utataka kujua namna watu watakavyorudia maisha duniani, ikiwa wameshageuka mavumbi baada ya kufa.

Hiyo ni rahisi, Mungu anafanya hivi:-
Ezekieli 37:6 - Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.

Kama tulivyoona aya zilizotangulia, ni kweli kabisa mtu akiwa kaburini ni uchafu tu na mifupa ila Mungu aweza kurudisha viungo vyote; mishipa, nyama, ngozi nk.

Ezekieli 37:7 - Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe.

Hii ni habari iliyotukia katika agano la kale ila ni kivuli cha yanayokuja karibuni wakati huu wetu.

Yesu anasema kaburini mna
mifupa na uchafu tu. Mathayo 23:27 - Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa MIFUPA ya wafu, na UCHAFU wote.

Sasa basi, Jibu la kichwa cha habari hii ni hili:
Mbinguni kuna wenyeji wake, vivyo hivyo duniani kuna wenyeji wake.
1 Wakorintho 15:40 - Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.

Sasa basi, Jibu kamili ni hili:-
Zaburi 115:16 -
MBINGU ni mbingu za Bwana, Bali NCHI amewapa wanadamuuuuuuuu.

Nafikiri umepata picha tofauti kabisa na kile ulichofundishwa miaka yote iliyopita.

Ukijua habari hii kuhusu hali ya mpendwa wako aliyekufa, itakutoa katika mateso na mahangaiko ya kiakili.
Watoto waliofiwa na wazazi wasipokuwa na ujuzi huu wanabaki wakifikiri kwamba hao wazazi wanasikia, kumbe hao wazazi hawahisi chochote, hadi Mungu atakapowafufua.

Hii inaweza kuleta kitulizo. Sii kwa watoto tu hata wazazi waliofiwa na mtoto, au kufiwa na mwenzi, rafiki nk.
Mhubiri 9:5 - kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

Shetani akijua huna ujuzi sahihi awezakujivika mwili wa mpendwa wako yeyote ili kukuamisha habari fulani ya uongo.

Onyo: Endapo utatokewa na mtu mwenye sura ya mtu unayejua huku ukijua kwamba alishakufa, kemea kwa jina la Yesu, huyo siye yule mpendwa wako.

Ubarikiwe kwa kusoma ujumbe huu

Baki salama.

Bofya hapa chini[emoji3593]

 
Kuna dada mmoja vipimo vya Dr vilionyesha amekufa baadae akafufuka/akaamka hapo hospitalini... Ndo akawa anasimulia Mambo ya mbinguni.... Anasema mbinguni ni hatari hakuna mahala pa kufananisha ni pazuri Sana na Kuna vibes Kama zote Kila unachokitaka kipo iwapo duniani ukiwa mtu Safi... So wew mzee wa Mizigo duniani ikaushie tu ili ukaifaidi Ile mizigo ya shekh kipozeo
la saba B.....Hivi shule bado hamjafungua?
 
Mbinguni kuna Roho na Mwili. Haviachani viwili. Hata ukifa leo hii, ukizikwa Roho inarudi kwenye mwili, na maisha yanaendelea kama kawaida, tofauti ya maisha ya kaburini ni kuwa hakuna kutafuta pesa wala mfano wake, zaidi ya kuruzukiwa kutokana na kile ulichokitenda huku ukisubiri hukumu.
hujielewi kabisa.......roho na mwili haviachani?
 
So nikitaka nile kuku watatoka wapi?
Kila utakachokitaka utakipata, mfano ukiwa hotel ukiagiza kuku huwa unamuona akichinjwa au utamuona tu katika sahani kwa namna ulivyoagizwa
 
Fumbo la kifo halinaga majibu mpaka ufe...achana na maswali ya aina hii..
Hakuna aliyekufa akafufuka na hata yesu mwenyewe alifufuka akapaa hakutaka kusema kakuta nini huko kwa babaake kwahivo utaumiza kichwa tu hapa..
Hakuna majibu sahihi ya swali lako na imani yako ndio msingi wa maisha yako
 
Hao VIUMBE habari chao huko peponi.
Sisi wana Adam na majini ndo Mali yetu huko.
Hao dunia ikiisha watageuzwa mavumbi
ILA BINADAM tukijaaliwa kwenda peponi tunakwenda kula raha.
Mwenyeezi mungu atujaalie

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Je, mbinguni ambapo tunaahidiwa kutakua na perfect life, hakuna kifo, hakuna kulia, hakuna njaa, ni furaha mwanzo mwisho, ni kuimba na kuabudu mwanzo mwisho wanyamapori kama simba, chui, swala, nyumbu na wengine watakuwepo? Je wataishi kwa upendo bila kulana, watashirikiana kila kitu?

Je, wao wanyama kama watakuwepo watakua na wao kazi yao ni kuimba na kuabudu siku zote bila kikomo? Je wanyama hao watakua wanazaliana?

Kama wanyama wataenda kushirikiana huko mbinguni, je huku Duniani nani aliwagombanisha kwa sababu hawaongei, hata wale wa species moja kama simba, paka, mbwa, chui hawaelewani wakati wale wanaokula majani wanaelewana.

Naomba kufahamu mbinguni kutakuwaje ama kukoje, nasikia tu kua kuna misosi imeandaliwa kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu (hizo hotpot ni balaa). Angalau waislamu wanatoa picha ndogo ya mbinguni kukoje, wanawake warembo na pombe, hapo kwa wanawake wamenipata, nitajilia vimwana[emoji23]. Vimwana wa mbinguni mjiandae tafadhali (nasikia hakuna cha alkasusu, viagra wala vumbi la congo, ni mpini mwanzo mwisho hata goli 12)

Je, mbinguni kukoje?

Ahsante.
Kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu kunathibitika katika nadharia tu (yaani theory) na si katika fact, kwa hiyo hata swali uliloulza hapa sana utapewa majawabu na siyo majibu, cha msingi kam una iman yako amin katika hiyo iman inaweza kukusaidia kuishi bila mkanganyiko wa kutokuelewa mambo [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Dini bana yani mtu ukikaa chini ukawa open minded afu uanze kufatakari story za dini kwa reasoning unaweza ukajikuta unajipiga Vibao vingi sana mwenyewe mana sio kwa umbumbu huo
 
Back
Top Bottom