Je mbinu gani zitumike kutengeneza ajira kwa vijana wetu

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Ni jambo lililo wazi kuwa jamii yetu inakabiliwa na tatizo kubwa sana la ajira. Takwimu zisizo rasmi zinasema kila vijana 2 kati ya 3 wanaohitimu elimu za juu wanakosa ajira katika mambo wanayoyasomea na kurudi mtaani kufanya shughuli zinazofanywa na watu wasiosoma.

bila kujiingiza kwenye mjadala wa je ni sahihi kumkopesha kijana mamilioni ya fedha au mzazi kumlipia mamilioni ya fedha kumsomesha mwanasheria akawe machinga, kumsomesha mhandisi amalize akaendeshe boda boda kumsomesha dakitari amalize masomo akawe mama ntilie?

Jamii lazima ijitahidi kufundisha wataalamu wanaokuja kufanya kazi za utaalamu katika jamii zao na kama haiwezekani basi badala ya kuendelea kutoa kozi za masomo yasiyokuwa na ajira basi vyuo vijikite katika kutoa taaluma hizo hizo za mamantilie, bodaboda, machinga.

mfano Bachelor of science in bodaboda au bachelor of arts in mamantilie na vijana wasome wakijua tunaenda kufanya haya.

kwa upande wangu naona jamii inahitaji kuwa na ubunifu wa kutengeneza ajira kwa vijana kulingana na uzalishaji wa vyuo vya taaluma.

kwamba tunahitaji kutengeneza fursa za ajira za maafisa jamii katika jamii kulingana na uwezo wetu wa kuzalisha maafisa jamii. tunahitaji kutengeneza fursa za wanasheria katika jamii kulingana na uwezo wetu wa kuzalisha wanasheria.

mfano tuna makubaliano mbalimbali katika jamii yanafanyika mfano uuzaji wa vitu mbalimbali vyenye kuhitaji makubaliano ya kisheria, kwanini tusiwachomeke wanasheria wetu kwenye makubaliano haya mfano uuuzaji wa viwanja na mashamba. Tuna migogoro mbalimbali katika jamii mfano migogoro ya ardhi kwa nini tusitunge sheria za kuwachomeka wanasheria wetu huko, wafanye kazi za jamii na walipane huko huko.

mimi naamini katika jamii kutengeneza mazingira ya kila mwanajamii kutafuta taaluma na wakisha pata taaluma wategemeane.

ni lazima tujiulize kwa mwaka mmoja tuzalishe madaktari wangapi? wanasheria wangapi? wahandisi wangapi n.k kwa kada zote. alafu tuangalie tunatengezaje fursa katika jamii za kuwabeba vijana wetu katika jamii.

kwamba labda tunazalisha wanasheria 1000, na tunajiwekea kila mwaka serikali itaajiri wanasheria 1000 na kutengeneza angalau katika jamii fursa za jamii kuajiri wanasheria 900. tunaweza kusema kila mtu akishitakiwa lazima atumie mwanasheria na tunawaweka katika makundi kiasi kwamba hata wale junior wanapata kazi za kuwakilisha watu mahakama za chini na pengine kulipwa kwa siku.

Tunaweza kuwa na kundi la wanasheria na madakitari wakizunguka kufundisha mashuleni elimu ya afya na haki na wanalipwa na wazazi kupitia michango.

Wengi watatazama umasikini na kusema jamii tunaweza kuibebesha mizigo mikubwa lakini hiyo ni njia ya kufuta umasikini kwa kujaribu kutengeneza mifumo ya wanajamii kutegemeana
 
moja wapo ya kazi za wizara ya kazi na ajira iwe ni kuwa na think tank ya kutengeneza ajira kwa kuwaambia wizara mbalimbali jinsi ya kutengeneza fursa.
 
Back
Top Bottom