Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Yeye kwa udhaifu wake ndiye alisababisha chama kizuiwe kufanya mikutano, kitu ambacho ni haki yao kikatiba. So maridhiano yalikuwa ni kurudisha haki alizozipoteza.Seriously?
Mbowe aliulizwa hilo swali na alijibu kuwa hawatarudi. Akaulizwa kama CDM yake itawasamehe, akasema suala la msamaha linaingiaje wakati hawajawahi kuomba msamaha. Akagusia kidogo kuwa kuna dalili kuwa wengine wameishahamia kwingine. Sasa mnataka aseme nini?
Watanzania wanahusika vipi hapa? CHADEMA sio chama tawala. Priority yao kubwa ni wanachama wao ( hasa wale ambao wamesimama nao siku zote).
Unasema kuwa anajijali yeye na genge lake lakini wale ambao wanaosema asipochaguliwa mtu wao mnaona ndio wenye mapenzi na CDM. Kwangu mimi hao wanampenda mtu kuliko chama.
Hiyo mipango yao mibovu ndio iliyokifikisha chama hapa kilipo ambapo sasa kila mtu anajiona kuwa anakijua kuliko wale waliotokq nacho mbali. Hao wenye mapenzi ya dhati walikuwa wapi wakati kinapitia wakati mgumu.
Leo mnabeza maridhiano wakati kabla yake hata kukutana chumbani hamkuweza. Kabla yake mamia ya wanachama na wafuasi wa CDM walikuwa ndani kwa mashtaka ya ajabu ajabu ( mengine walishtakiwa kwa murder). Sikusikia watu wakichangisha michango ya kuwalipa mawakili wa kuwatetea. Nilichokiona na viongozi wa CDM, Bavicha na Bawacha wakiwatembelea mara kwa mara. Mlitaka hao waendelee kuozea mahabusu kwa sababu tu ya Covid 19? Halafu mnasema mnawajali wanachama wa Chadema?
Mimi nadhani kinachotakiwa ni mjadala wa kiungwana, kati ya watu wanaoheshimiana ingawa wanatofautiana mawazo. Baada ya hapo wale wenye mamlaka ya kupiga kura wamchague mtu ambae wanaona anaweza kuijenga CDM yenye matumaini kwao. Baada ya hapo waendelee kujipanga kwa ajili ya chaguzi zijazo.
Mnachofanya sasa ni kubomoa hata kile mlicho nacho kwa misguided efforts za kumtoa mtu msiyemkubali.
Mkataeni lakini msimvunjie heshima. Matumaini yangu ni kuwa yeyote atakayeshinda ataweza kuchukua mawazo mazuri ya washindani wake kwa faida ya chama chao.
Amandla...
Pia watu hawalalamiki Mbowe kushindana na Lissu, au hawataki kura ziamue, bali wanalalamika kung'ang'ania kwake madaraka. Alibadili katiba na kuondoa ukomo. Huo ni uhuni. Miaka 20 amekuwa mwenyekiti. Hapaswi kuingia kupigiwa kura. Mbowe hata akishinda, uenyekiti wake utakuwa batili myoyoni mwa wanachama wanaojielewa.