Uchaguzi 2020 Je, mchujo wa washindi wa kura za maoni CCM kugubikwa na sintofahamu nyingi?

Unataka walevi na porn stars wakatunge sheria bungeni? Kwa hali hiyo Utapona ?
Tafakari liquid yuko mjengoni akibugia kilaji na sheria.
 
Mbona CDM mmeanza kua na wasiwasi kuliko Wana ccm wenyewe?
Huo utaratibu upo miaka nenda Rudi na ni mzuri Sana kwa wale wacheza rafu na kupanga mashambulizi.

Wapinzani kwa Sasa mnaicheza ngoma ya ccm tu maana ndo gumzo kila Kona.Si bure ndo Mana mliitwa CCM B
 
CCM kulazimisha kupeleka watu ambao siyo chaguo la wengi kwa vigezo vyao visivyozingatia haki za wapiga kura za maoni ndiyo hupelekea vitendo vya wizi wa kura uchakachuaji kupora ushindi
 
CCM ikipeleka magara jimboni huwatesa wapinzani kwa kuwaibia kura
 
Yani nimegundua hata wapigakura za maoni hawako knowledgeable vyakutosha!

Yani vigezo vya jinsi ya kuchagua kujua nani apewe kura havijulkani!

Nimejaribu kuuliza walochukua form mfano watu 40 Je mnatumia vigezo gani vya kuwachagua?

Eti wanazungumza muda mfupi kisha wanapigiwa kura [emoji87][emoji87]

Eti hakuna mchujo wa Vigezo vya elimu wala uzoefu wa utumishi [emoji108][emoji108]

Imagine [emoji87][emoji87][emoji87]

Yani Bongo bado sana!
 
Kuna mapungufu mengi kwenye mchakato wa watia nia
 
Usiwe na wasiwasi kama kuna mchakato huwa ni wa haki (mara nyingi sana) kwa CCM ni huu wa wazee 24.
 
Hii ndio kete anayoitegemea Bashite😂😂
 
Katiba mkuu kajidai kusema watakusanya report za mwenendo wa upigaji kura ndipo waje na maamuzi ya kiccm eti ni utaratibu wa kiccm, huo utaratibu wa kwenda kumkata mtu aliyeshinda kura za maoni kwa visingizio vya uchunguzi ni mfumo wa hovyo sana na umepitwa na wakati kwani watu wabaya wanye chuki zao wanaweza kuvitumia vyombo vya uchunguzi kuwahujumu wale walioshinda kura za maoni, vyombo vya uchunguzi siyo malaika siyo mungu vina mapungufu na pia wapo wenye mahaba na watu wao waliokatwa kwenye kura za maoni, mfumo huo ni wa hovyo na unawavunja moyo wapiga kura
 
Usiwe na wasiwasi kama kuna mchakato huwa ni wa haki (mara nyingi sana) kwa CCM ni huu wa wazee 24.
Huo mchakato wa kwenda Dodoma kuchagua jina umepitwa na wakati sasa ni mfumo wa hovyo waachane nao waje kisasa zaidi.
 
Huu mfumo ukifaa zamani wakati watanzania wakiwa hawajaamka, lakini sasa kila mmoja yupo macho ukimkata mpendwa wao kwa visingizio vya report za uchunguzi zisizo tokea kwa mungu mbinguni lazima watagoma kujitokeza kwenda kupiga kura ama kupiga kura za hasira kwa watu wengine kinyume na yule waliyewalazimisha kumpenda kwa nguvu ya vikao vya Dodoma.
 
Kama aligawa rushwa si akamatwe? Kamati ya usalama na maadili itakuwa sio salama na haina maadili!
 
Mwenyekiti wa Kinondoni kasema eti wataenda kuhoji mshindi kapata pataje ushindi? huyo ni mfumo wa hovyo waliweka Takukuru wa nini sasa kama kuna uchunguzi mwingine hufuata?
Wamtoe tu mzee wa kubetisha wamuweke yule Pusha ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…