screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,857
- 15,866
Mi sielewi hizi media zetu kubwa ambazo zimeonekana kususia kupiga nyimbo za WCB, kama Diamond ndio kawakosea ni kwanini wasimpe adhabu yeye? Hawajui kama wanawakomoa kina Mbosso,Lavalava na wengine bila sababu za msingi? Mi nnachoona hapa ni kwamba wameona kwa level aliyofikia Diamond kwasasa hawawezi kumkwamisha kwa kutopiga nyimbo zake, hategemei promo ya eatv,efm,clouds fm pekee maana tayari ana die hard fans wa kutosha na TV/redio za kimataifa zinamtambua, so walichoona kinawezekana kwao ni kuwabana na wasanii wake ambao bado hawajawa na fanbase ya kutosha, kwakuwa wanajua kuzidi kung'aa kwa hawa wasanii ndivyo akaunti ya Mond inavyozidi kunona. Hii imenikumbusha utotoni kama kwenye ugomvi umepigana na kakamtu kakudunda unamvizia mdogo wake, siku ukimbahatisha unatoa ndonga za kutosha kumaliza hasira za kipigo cha kaka.