JAYJAY
JF-Expert Member
- Oct 31, 2008
- 8,191
- 8,490
Hivi Leo hii, vituo vya radio viamue kucheza nyimbo za nje tu kwa kipindi cha mwaka mzima na hata habari za wasanii wetu wasizitangaze, unadhani radio ndio zitaathirika au wasanii!? Binafsi natumia mitandao lakini radio zinanisaidia sana kufahamu nyimbo mpya kabla ya kuziendea huko mitandaoni.
Nguvu ya media ilikua enzi hizo sio sasa hivi. Kwanza hata mara ya mwisho kusikiliza radio sijui lini mambo yote online bro.
Zamani ilikua lazima nyimbo ipigwe kwa radio ili watu waisikie siku hizi ipo hivo?? Tunadownload tu vibanda vya kuweka nyimbo vingi ajabu tusiwatukuze sana hawa wa media wanaojiona wanaweza kumshusha na kumpandisha mtu.