Ngoja nikueleweshe mkuu...miaka ya mfalme daudi iliisha alipofikia uzee sana na mwanae Suleiman akatawadhwa kuwa mfalme, malkia Bilqis au Sheba alikua malkia wa ethiopia au kush akaskia sifa za hekima za mfalme suleiman kwa hiyo akaenda hadi israel akiwa na zawadi lukuki kutoka Afrika..
Sasa hapo ndio inasemekana alitembea nae na kuzaa nae kabisa na mtoto huyo alikua mrithi wa ufalme wa ethiopia
Na huyo malkia alirudi ethiopia wala hakupata tena kurudi israel.
Sasa uzao ule ukaendelea Hadi miaka ya juzi ya 60 ndio utawala wa kifalme ukaishia kwa mfalme Haile Selasie baada ya kupinduliwa na kuuliwa na waziri mkuu Mengistu Haile Mariam.
YESU alizaliwa na Joseph aliekua wa ukoo wa Daudi, ila wao ni mtiririsho wa kizazi hicho ambacho kilibaki israel.
Kutoka daudi hadi YESU ni miaka 2000 na kutoka YESU hadi Haile Selasie ni miaka 1935
Kama ni kweli kuhusu habari ya Malkia wa Sheba basi Haile Selasie Babu wa mababu zake walikua Daudi na Suleiman..
Karibu