Je, mfumo wa kupata viongozi ni sahihi?

Joined
Apr 24, 2024
Posts
9
Reaction score
7
Tanzania Tunayoitaka na Viongozi Wabeba Maono Ni sawa? Jua linapochomoza huwa na hali ya utulivu na pambazuko lenye kuvutia ila kila linapozidi kutoka huwa na hali tofauti na mazingira hali ambayo kuna wakati wanadamu hushindwa kuivumilia na kutoa maongezi tofauti na yale ya mwanzo waliyokuwa wakiyasema pindi jua linapochomoza. Hali hii pia hutokea katika uongozi wa nchi kwani kuna nyakati inatubidi tuweze kufanya mabadiliko makubwa katika mifumo ya uteuzi wa viongozi hususani viongozi wa kuteuliwa, kwani mbaka sasa hatujaweza kujua je mfumo tunao utumia kupata nafasi za viongozi wetu hawa wanaoteuliwa ni sahihi au si sahihi.

Mfumo wa uongozi hutofautiana kwa ukubwa kulingana na mahitaji ya eneo husika ila kwa nchi yetu inaonekana kwa nafasi kubwa viongozi wengi wa kuteuliwa huwa ni watu wanaoteuliwa moja kwa kufuata utashi wao ila sio kwa kuangalia zaidi wanafaa katika eneo husika au laah. Siku za karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la teuzi ambazo zimekuwa zikitolewa ila watu wengi wanaopewa nafasi hizo kubwa mara nyingi wamekuwa ni watu maarufu na wale wale ambao wamewahi kupewa nafasi hizo za uongozi sehemu tofauti ila walishindwa pia kuzitumikia vyema ila kuna kuwa hakuna budi zaidi ya kuwafuata hao hao.

Je, mfumo uliokuwepo sasa unatufaa? Kwa kiasi fulani hatujachelewa sana ila kwa upande wangu ningependa kuwe na mdahalo wa wazi kwa umma kutoa maoni yao juu ya mfumo wa uteuzi wa viongozi hususani viongozi wa kuteuliwa hapa tungeweza kutoa fursa kwa watu wengi kuweza kupata njia sahihi ya kupata viongozi sahihi kuliko kuliacha jambo hili kuwa utashi wa watu fulani pekee.

Vilevile ningependa kupendekeza kuna nafasi mbalimbali za uongozi zingepelekwa moja kwa moja kwa wananchi wao wawe na pendekezo la moja kwa moja juu ya mtu anayewafaa katika eneo hilo ambaye analijua vyema mfano wakuu wa wilaya na mikoa, wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali. Pia kuna nafasi zinabidi watu tuwe tuna waweke kwa kuwaajiri huku tukiwapa malengo ambayo wanapaswa kuyatimiza kwa ajili ya kulinda kazi zao hizo hii itatupa nafasi kubwa ya kuweza kuwa wajibisha viongozi hao wanaposhindwa kufanya malengo ambayo wameweza kupewa katika idara husika au eneo husika.
 
mfumo mzuri ni ule ulioakisiwa kwenye sheria ya utumishi wa umma no 8 ya mwaka 2002 inayotaka nafasi hizi zijazwe kwa ushindani on meritocracy,hapo tutapona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…