Je, mfumo wetu wa elimu ni chanzo cha umasikini?

Je, mfumo wetu wa elimu ni chanzo cha umasikini?

raxx

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2016
Posts
326
Reaction score
284
Moja kwa moja kwenye mada!!

Mara nyingi najiuliza kwamba suala hili la mfumo wetu wa elimu kuzalisha mbumbumbu, Serikali hailioni imeshindikana kuubadilisha, au kuna manufaa gani inapata kwa mfumo huu.

Miaka 7 ya primary school tunafundishwa Mkwawa alikufa mwaka gani? Mara Kinjekitile Ngwale ni nani?, na bla bla nyingine nyingi

Miaka minne secondary school mtoto anafundishwa tena kuhusu Kinjekitile Ngwale na Newton alizaliwa mwaka gani tofauti hapa amebadilishiwa lugha ya kizungu. sana sana na Hesabu zisizokuwa na maana yeyote katika kiwajenga kiuchumi watoto

Miaka 2 Advance level hapa mtoto anafundishwa yalele ya Kinjekitile Ngwale na bla bla nyingine ambazo haziwezi kumletea tija katika maisha yake ya utafutaji.

Na kwa wale wa michepuo ya science nao wanasoma science kwa njia ya kusimuliwa yaani umbea mtupu, waelezwa Newton alingundua hiki na hiki , Enstein aligundua hiki, Faraday aligundua hiki, ndio science yetu imeishia hapo bila kuambiwa na wao wanatakiwa wagundue vyao.

Unakuta Dogo wa PCM hata maintainance ndogo ya kiswaswadu tu hajui..lakini mapractical ya Newton ambayo hayamsaidii kitu yote anayo kichwani.

Huu mfumo wa Elimu wa namna hii hauna tija kwa taifa, kubwa huzalisha vijana wasiokuwa na tija katika kukuza uchumi wa nchi sana sana huwaharibia watoto future zao.

 
Mwandishi anaonekana uelewa wake uko low.. na pia amejikatia tamaa.. huenda ameathirika na elimu iso na tija..

Pole mleta uzi. Pumzika halafu urudi tena ukiwa umetulia. Huenda una hoja nzito, tatizo uwasilishaji ni wa kina Msukuma family

Asante
 
Naona unaandika usichokielewa, mi naona elimu imayofundishwa Kwa Sasa sio tatizo, na pili usitegemee mtu anayesoma mchepuko wa PCM atengeneze simu, Kwa kuwa anasoma fizikia na sio uhandisi hilo Moja.

Pili, Hesabu wanazofundishwa elimu ya sekondari Zina faida kubwa sana kuliko una vofikiri, sema wanafundishwa Kwa hatua, kutokana na ukomavu wa akili, mfano Algebra na Calculus ile ni muhimu sana kwenye masomo ya uhandisi wa Kompyuta.

Tatizo la elimu yetu, waalimu wanashindwa kufundisha practical applications kwasababu kwanza teknolojia ndogo na pia waalimu wenyewe hawana moyo na hawapendi kufanya utafiti so wanabaki kuwakaririsha wanafunzi. Kama mwalimu wako hajakuhamasisha kufanya utafiti, huwezi gundua kitu chochote hata tukupeleke Cambridge Leo.

Ulaya wanasoma Fizikia ileile......ila tofauti ya sisi na wao ni teknolojia wako juu, pili waalimu wao wanafundisha wakiwa na uhakika wanachokifanya( wanajua practical applications za masomo mbalimbali).

Historia ni muhimu sana kuijua Ili ufahamu utokako na uendako, wazungu wanafundishwa Historia yao.
 
Back
Top Bottom