Je, Mgombea Urais wa CCM ashitakiwe kwa kuwa na kusudio la Kuhujumu Uchumi?

mwita ke mwita

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2010
Posts
8,070
Reaction score
3,792
Mara nyingi mgombea huyu amekuwa akitishia watu kuwa wasipomchagua mgombea anayemtaka yeye mara atawanyima maji , mara atawanyima barabara,na mambo mengine mengi.

Mgombea huyu atambue kwa kufanya hivyo atakuwa anahujumu uchumi, mathalani atatakiwa kutengeneza barabara nzuri ili TRA wafike huko kukusanya kodi, atatakiwa kupeleka maji ili mamlaka za maji zipate wateja, wateja wakinunua maji , mamlaka zitatoa ajira zaidi, watu wakipata ajira watalipa kodi , pia loan board atapata marejesho yake kadhalika NSSF, NHIF na wengine watapata wachangiaji.

Wakuu hebu tiririkeni na nyie madhara ya kiuchumi ambayo huyu mgombea kwa kutokujua na au kwa makusudi anaenda kutusababishia kwenye nchi, ili watu wema wapate nafasi ya kumuandalia mashtaka ya kuwa na njama ya kutaka kuhujumu uchumi wa nchi
 
Ambacho hamtambua J.P.M ni kama msimamizi tu.

Endapo Mbunge utakuja bungeni kusinzia bila kuonesha kero za wananchi wake,tufanyaje?
au mbunge unapinga pinga bajeti bila sababu za msingi.

sometimes,Inabidi mtambue wajibu wa wabunge na mawaziri katika idara zao.
 
Sawa... ila swali ni nani anapaswa kumuwajibisha mbunge??? Je ni Rais kwa kuwatishia wapiga kura au wananchi wenyewe????
 
Waziri wa wizara husika endapo mambo hayajaenda sawa katika wizara|idara yake ndio huwa responsible.

Mmesahau kuwa na Nyie mnatutisha kuwa endapo hamtapita mtaingia barabarani na mtetezi wa mapenzi kinyume na Maumbile T.Lissu.
 
Ambacho hamtambua J.P.M ni kama msimamizi tu.

Endapo Mbunge utakuja bungeni kusinzia bila kuonesha kero za wananchi wake,tufanyaje?
au mbunge unapinga pinga bajeti bila sababu za msingi.

sometimes,Inabidi mtambue wajibu wa wabunge na mawaziri katika idara zao.
Umeelewa hoja lakini?Tunduma amesema kuwa serikali ilishakamilisha mpango wa kupeleka maji na kilichobaki ni utekelezaji ambao utafanyika hivi karibuni!Lakini akasema kama wasipomchagua Silinde basi maji hapeleki tena na watayasikia tu kwenye bomba!
Sasa ndio mleta mada anahoji,huu sio uhujumu uchumi?
Yaani watu kupata maji ni mpaka watoe hongo?
 
TAL anasema endapo tukishinda na tume isitutangaze hakitaeleweka...sasa hapa mmetishwa wapi??? Je kuambiwa ukweli ndio vitisho??? Kwanini msitende haki ili kuliepusha hilo badala ya kuendelea kutishia wananchi wenu.

Na hii ni mbaya sana MATHARANI kwakuwa sisi wote ni watanzania ukimnyima maendeleo mwanachadema aishie Tunduma maji basi umewanyima watanzania wote waishio Tunduma pasipo kujali vyama vyao... sasa hii MNAICHUKULIJE KWENU???
 
Ambacho hamtambua J.P.M ni kama msimamizi tu.

Endapo Mbunge utakuja bungeni kusinzia bila kuonesha kero za wananchi wake,tufanyaje?
au mbunge unapinga pinga bajeti bila sababu za msingi.

sometimes,Inabidi mtambue wajibu wa wabunge na mawaziri katika idara zao.
Rubbish [emoji706] [emoji706].... This worked in previous regimes but not now ambapo hata bajeti iliyopitishwa na bunge haifuatwi....
 
Mimi nadhani huyu Jamaa Magu aanze kufunguliwa kesi Ana madudu mengi ya kumpeleka lumande.
 
Ambacho hamtambua J.P.M ni kama msimamizi tu.

Endapo Mbunge utakuja bungeni kusinzia bila kuonesha kero za wananchi wake,tufanyaje?
au mbunge unapinga pinga bajeti bila sababu za msingi.

sometimes,Inabidi mtambue wajibu wa wabunge na mawaziri katika idara zao.

Unachotakiwa kujua kazi kubwa ya bunge ni kutunga sheria ,masuala ya maendeleo yote yana idara zake mfano Umeme (TANESCO) hawa wanapaswa wakufuate tangu unaanza ujenzi wakushawishi ufunge umeme mapema ili wapate malipo, unakumbuka zamani TTCL na posta walivyotesa watu ila baada ya kuja kampuni nyingine leo hii TTCL wanatubembeleza turudi kwao.

Barabara ziko chini ya TANROADS na TARURA, wao wanatakiwa waone potential za uchumi kila maeneo ili wajenge barabara ili kuisaidia serikali ikusanye pato la kutosha na pia kupunguza gharama ,kumbe umeme na barabara zikifikia uchumi unakua ,biashara kama welding, usafirishaji, vinywaji na vileo, na nyingine zinakuwa kwa kasi hivyo serikali inasaidiwa kuondoa ukosefu wa ajira na pia uchumi kukua.

Maji , yako chini ya mamlaka za Maji , mfano Pwani tuna DAWASA na DAWASCO wao wanatakiwa wapambane usiku na mchana kutafuta wateja wapya, wakitafuta wateja wapya wenye biashara za pipes na mita wanapata biashara, mafundi mchundo na vibarua pia wanapata pesa , mama ntilie pia wanapata kuuza ubwabwa kwa mafundi, mwisho wa siku uchumi wa nchi unasonga mbele yapo mengi sana , ipo mifano mingi sana, hivyo ondoeni ujinga wa kuwaza kuwa mbunge anatakiwa alete maendeleo.

mbunge anatakiwa apambanie sheria mfano , vitu kama vitambulisho vya umachinga, PAYE kubwa, NSSF ishushwe, WCF iunganishwe kwenye NSSF, SDL iondolewe kwani Loan board inatoza riba warudisha mikopo, corporate taxes ziwe rafiki, tax administration iwe rafiki kwa mfanya biashara, mkulima awe huru kuuza mazao yake, kuondoa ubabaishaji kwenye sheria za ushirika etc
 
Chedema kwanini na wao wasipeleke malalamiko kuhusu kauli na ahadi pamoja na matishio ya Magufuli kwa wananchi? Wapeleke tuone double standards zaidi.
 
Umeelewa hoja lakini?Tunduma amesema kuwa serikali ilishakamilisha mpango wa kupeleka maji na kilichobaki ni utekelezaji ambao utafanyika hivi karibuni!Lakini akasema kama wasipomchagua Silinde basi maji hapeleki tena na watayasikia tu kwenye bomba!
Sasa ndio mleta mada anahoji,huu sio uhujumu uchumi?
Yaani watu kupata maji ni mpaka watoe hongo?
Umeelewa hoja lakini?Tunduma amesema kuwa serikali ilishakamilisha mpango wa kupeleka maji na kilichobaki ni utekelezaji ambao utafanyika hivi karibuni!Lakini akasema kama wasipomchagua Silinde basi maji hapeleki tena na watayasikia tu kwenye bomba!
Sasa ndio mleta mada anahoji,huu sio uhujumu uchumi?
Yaani watu kupata maji ni mpaka watoe hongo?
Ikumbukwe J.P.Magufuli ni Mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi.

Wakati huu muda wake wa urais unaenda kufika kikomo kuna baadhi ya miradi ameianzisha lakini bado haija kamilika na Mingine ni Mipango tu lakini utekelezaji bado haujaanza.

Sasa iwapo bado ni Mgombea ana haki ya kuzungumza ya kuomba kura kupitia hii miradi ili aendeleze alipoanza..endapo mtashindwa kumchagua anaamini kila rais|serikali inavipaumbele vyake wenda alichokianza kisitimie.

Upande wa Silinde bado ni haki yake kufanya hivyo kama Mwenyekiti wa chama ili tumchague mtu ndani ya chama chake..Hili si kosa kabisa kunadi mgombea wake ndani ya chama chake.

Isitoshe pia anaogopa msije mkachagua upinzani wakaanza kupinga mradi huu kama wanavyoonesha sasa wakiwa wanapinga miradi inayoendelea nchini kama S.G.R ,ujenzi wa flyover n.k
 
unachotakiwa kujua kazi kubwa ya bunge ni kutunga sheria ,masuala ya maendeleo yote yana idara zake mfano
Umeme (TANESCO) hawa wanapaswa wakufuate tangu unaanza ujenzi wakushawishi ufunge umeme mapema ili wapate malipo, unakumbuka zamani TTCL na posta walivyotesa watu ila baada ya kuja kampuni nyingine leo hii TTCL wanatubembeleza turudi kwao.
Barabara ziko chini ya TANROADS na TARURA, wao wanatakiwa waone potential za uchumi kila maeneo ili wajenge barabara ili kuisaidia serikali ikusanye pato la kutosha na pia kupunguza gharama ,kumbe umeme na barabara zikifikia uchumi unakua ,biashara kama welding, usafirishaji, vinywaji na vileo, na nyingine zinakuwa kwa kasi hivyo serikali inasaidiwa kuondoa ukosefu wa ajira na pia uchumi kukua.
Maji , yako chini ya mamlaka za Maji , mfano Pwani tuna DAWASA na DAWASCO wao wanatakiwa wapambane usiku na mchana kutafuta wateja wapya, wakitafuta wateja wapya wenye biashara za pipes na mita wanapata biashara, mafundi mchundo na vibarua pia wanapata pesa , mama ntilie pia wanapata kuuza ubwabwa kwa mafundi, mwisho wa siku uchumi wa nchi unasonga mbele
yapo mengi sana , ipo mifano mingi sana, hivyo ondoeni ujinga wa kuwaza kuwa mbunge anatakiwa alete maendeleo.
mbunge anatakiwa apambanie sheria mfano , vitu kama vitambulisho vya umachinga, PAYE kubwa, NSSF ishushwe, WCF iunganishwe kwenye NSSF, SDL iondolewe kwani Loan board inatoza riba warudisha mikopo, corporate taxes ziwe rafiki, tax administration iwe rafiki kwa mfanya biashara, mkulima awe huru kuuza mazao yake, kuondoa ubabaishaji kwenye sheria za ushirika etc

Maendeleo na bunge yapo hivi.

Mbunge ni representative wa wananchi katika jimbo lake.
Anawajibu mkubwa wa kutoa kero na mahitaji ya wananchi katika Jimbo lake.

Hii itamsaidia katika kujadili Bajeti yeyote basi jimbo lake lizingatiwe.Hii kusema kutatuliwa changamoto za wananchi wake katika jimbo(na hii ndio kazi kubwa inayowapeleka bungeni).

Mambo ya kutunga sheria ..hizi principle law zimedelegate power ya bunge kwa ministers waweze kutunga by Laws pia.

Wizara itatambua vipi changamoto za wananchi wa Jimbo lako na kuwatengea budget kama mbunge wao upo kimya??

Wizara zimejikita katika utekelezaji na sio kutoa kero za wananchi bungeni.
 
kero zote inatakiwa ziende kwenye halmashauri, bunge linatakiwa ku deal na mambo ya nchi , thats why mbunge ni mjumbe kwenye vikao vya halmashauri, kama ni barabara tayari tunao TARURA, barabara kama zikizorota awajibishwe TARURA, kama hakuna maji awakilishwe Mamlaka ya maji, eg MORUWASA, KISHUWASA<TUWASA etc, tatizo lako wewe na makada wenzako nafasi hizi mnawekana makada ,hawawekwi watu wenye weledi na mamlaka hizi still mnaziingilia kisiasa upo hapo jo
 
Ikumbukwe J.P.Magufuli ni Mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi.

Wakati huu muda wake wa urais unaenda kufika kikomo kuna baadhi ya miradi ameianzisha lakini bado haija kamilika na Mingine ni Mipango tu lakini utekelezaji bado haujaanza.

Sasa iwapo bado ni Mgombea ana haki ya kuzungumza ya kuomba kura kupitia hii miradi ili aendeleze alipoanza..endapo mtashindwa kumchagua anaamini kila rais|serikali inavipaumbele vyake wenda alichokianza kisitimie.

Upande wa Silinde bado ni haki yake kufanya hivyo kama Mwenyekiti wa chama ili tumchague mtu ndani ya chama chake..Hili si kosa kabisa kunadi mgombea wake ndani ya chama chake.

Isitoshe pia anaogopa msije mkachagua upinzani wakaanza kupinga mradi huu kama wanavyoonesha sasa wakiwa wanapinga miradi inayoendelea nchini kama S.G.R ,ujenzi wa flyover n.k
Yeye anasema akiwa Rais na mbunge akawa upinzani basi wasahau hiyi miradi!Yaani hapa ni kuwakomoa wananchi kisa wamemkataa Silinde!Msijaribu kupoza poza maneno,hicho ndicho alichosema!
 
Waziri wa wizara husika endapo mambo hayajaenda sawa katika wizara|idara yake ndio huwa responsible.

Mmesahau kuwa na Nyie mnatutisha kuwa endapo hamtapita mtaingia barabarani na mtetezi wa mapenzi kinyume na Maumbile T.Lissu.
BRAINLESS
 
unapowakomoa wananchi unahujumu uchumi wa wanachi, unapohujumu uchumi wa wananchi unahujumu uchumi wa nchi
 
Waziri wa wizara husika endapo mambo hayajaenda sawa katika wizara|idara yake ndio huwa responsible.

Mmesahau kuwa na Nyie mnatutisha kuwa endapo hamtapita mtaingia barabarani na mtetezi wa mapenzi kinyume na Maumbile T.Lissu.

Mtetezi wa mapenzi kinyume na maumbile nadhani ni yule anayeomba mwanaume mwenzie amsugue vizuri
 
Umeelewa hoja lakini?Tunduma amesema kuwa serikali ilishakamilisha mpango wa kupeleka maji na kilichobaki ni utekelezaji ambao utafanyika hivi karibuni!Lakini akasema kama wasipomchagua Silinde basi maji hapeleki tena na watayasikia tu kwenye bomba!
Sasa ndio mleta mada anahoji,huu sio uhujumu uchumi?
Yaani watu kupata maji ni mpaka watoe hongo?
Mnapoteza muda kujadili ndoto za mshindi wa pili wa kura.
 
Back
Top Bottom