Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
JE, KUNA HAJA YA RAIS MAGUFULI KUWA NA HOFU NA MASHAKA JUU YA CHANJO YA CORONA?
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Dunia kwa sasa ipo katika mjadala mkubwa kuhusiana na janga la Corona na chanjo zake. Nadharia mbalimbali zimezuka ama zingine zilikuwepo na zimepata nguvu katika kipindi hiki cha janga hili la Corona. Wapo wanaosema Chanjo ya Corona ni salama na wapo tayari kuipokea; Pia wapo wanaosema Chanjo ya Corona sio salama na hawapo tayari kuipokea, kundi hili huchukulia kuwa Corona ni njama na hila ya watu wa dunia ya kwanza kuathiri watu wa dunia ya pili katika njia isiyo ya moja kwa moja.
Nimekuwa mfuatiliaji wa karibu wa mambo haya tangu mwaka juzi december 2019. Janga la Corona kwa upande wangu nalichukulia kama njama/hila na vita ya kibaiolojia yenye malengo makuu mawili; Mosi, Biashara ambapo kwa hakika mataifa makubwa yatajipatia fedha nyingi mno kupitia chanjo hii. Lengo hili ni short-term plan.
Pili, Kudhibiti Ongezeko la watu Duniani hasa kwa nchi za dunia ya tatu. Hii ni long-term plan.
Kuna watu ni kawaida yao kubisha, iwe kwa kupata faida au hubisha tuu bila hata kupata faida. Moja ya mambo yanayoumiza vichwa watawala wa dunia ya kwanza ni suala la ongezeko la kasi la idadi ya watu katika nchi masikini hasa hasa Afrika.
Kuna watu wanasema kuwa; kama wazungu wangekuwa na nia ya kutuua wangeshatuua wote, na chanjo ya corona sio silaha yao ya mwisho kuiangamiza Afrika. Mawazo hayo ni ya kijinga na huwazwa na watu wajinga. Wazungu hawawezi na hawana mpango wa kutuua wote hilo lipo wazi, lakini hatuwezi jidanganya kuwa hawana mpango wa kupunguza ongezeko letu la watu barani Afrika.
Hata kipindi cha zamani, Misri ilivyowachukua Israel utumwani, walipoona idadi ya waisrael ni tishio ndani ya taifa lao, utawala wa Mafarao uliunda njama za siri za kupunguza idadi ya waisrael kwa kuua wazaliwa wakiume watakaozaliwa kipindi hicho. Lengo sio kuua wasirael wote bali kupunguza kasi ya ongezeko la watu.
Katika utawala, ni kawaida kwa wakubwa kujadili population ya wale wanaowatawala, na ikiwezekana hatua zichukuliwe kudhibiti ongezeko lolote la watu litakaloleta athari hasi kwenye maslahi ya wakubwa wa dunia.
Mhe. Magufuli mara kwa mara amekuwa akionyesha hofu yake kuhusiana na kile kinachoendelea duniani. Tangu mwaka jana amekuwa akionyesha msimamo wake kuhusu suala la Corona na namna ya kulikabili. Wapo wanaomuunga Mkono na wapo wanaompinga basi kila mmoja na utashi wake.
Mhe Rais amekuwa akisema wazi na hadharani na kila mtu akisikia kuhusu mashaka yake makubwa dhidi ya wazungu, mara kadhaa amekuwa akisema wazungu hawatutakii mema, mara kadhaa amenukuliwa akisema kuwa chanjo hizi sio za kuziamini haraka haraka.
Mimi binafsi namuunga mkono kwa asilimia mia moja. Dunia ya sasa sio kila kitu ni chakukirukia rukia tuu, dunia ya sasa ni ya kuviziana, ina hila, njama na mitego mingi mno. Kukurupuka kukubali kitu kwa upesi ni dalili ya kutokukomaa.
Binafsi ninaiona haja ya Magufuli kuwa na hofu na mashaka ju ya chanjo ya Corona kwa sababu zifuatazo;
1. Hatuna wataalam wa Afya na vifaa tunaotengeneza sisi wenyewe kama taifa
Hii ni sababu namba moja kabisa, Magufuli lazima awe na hofu katika chanjo ya Corona na chanjo nyingine maana watu wanafikiri ni chanjo ya corona pekee yake. Hii ni kutokana na kuwa nchi yetu hatuna wataalamu wa kuthibitisha ubora ama udhaifu wa chanjo tutakayoletewa wala hatuwezi kutengeneza vifaa vyetu wenyewe. Hii hata mimi lazima niwe na mashaka, ingekuwa tunaowataalam na vifaa vyetu wenyewe wala pasingekuwa na sababu ya kuhofia kwani tunajua wapo Watanzania wenzetu ambao hawawezi kuiangamiza jamii yao wenyewe.
2. Rushwa na Vibaraka ndani ya Taifa
Taifa letu limejaa vibaraka kila kona ya nchi. Hii ni kutokana na sababu kuu mbili, mosi, ubinafsi na kukosa uzalendo, pili, uwekezaji uliofanywa na mabeberu. Wazungu waliwekeza na bado wanawekeza kwenye wataalam wetu hapa nchini, wataalam wengi walipewa Scholarship kusomea nje ya nchi, na wengi wakirudi ni vibaraka vya hao mabeberu.
Uwekezaji huu ni sehemu ya kuongeza vibaraka ndani ya nchi. Pia Rushwa ni sehemu ya udhaifu wa baadhi ya viongozi wetu hapa nchini. Ubinafsi na kukosa uzalendo kumepelekea viongozi wengi kupewa rushwa ya fedha kama sio ahadi ya mali ili watimize matakwa fulani ya mabeberu.
Sio ajabu kusikia kiongozi wa Afya akipewa pesa kwa ajili ya kutimiza lengo fulani la wazungu, hiyo sio ajabu. Sio ajabu viongozi wa afya wakipewa rushwa ili tuu watoe taarifa zisizo na maslahi kwa taifa hili kwa lengo la kuwapa faida wazungu, sio ajabu.
Sababu hizi zinapelekea hata ningekuwa mimi kuwa na hofu na mashaka dhidi ya chanjo ya Corona. Hivyo ipo haja kwa Magufuli anye kuwa na mashaka.
3. Historia ya nyuma baina ya mzungu na muafrika bado ni Tata
Hakuna asiyejua mabaya waliyowafanya wazungu kwa muafrika, hakuna asiyejua mauaji, utesaji, maumivu, unyonyaji wa mali na nguvu za muafrika uliofanywa na Mzungu kwa muafrika. Hakuna asiyejua dharau na udhalilishaji uliofanywa na mzungu kwa muafrika.
Hakuna asiyejua kuwa Mzungu anamchukuliaje Mwafrika. Hakuna asiyejua utumwa na ukoloni uliofanywa na Muafrika.
Ni mtu mjinga na mwendawazimu peke yake ambaye atapuuza historia ya nyuma ya mzungu na kumuona mzungu anania njema na bara la Afrika. Kusema mzungu anampenda Mwafrika ni dalili ya ukosefu wa akili kulikopitiliza. Sababu ya kihistoria ndio inayomfanya Mhe Rais kuwa na mashaka dhidi ya chanjo ya Corona.
Binafsi namchukulia mzungu kama mtu anayetutumia kwa faida zake mwenyewe, asiyependa maendeleo ya muafrika, anayefurahia mateso ya Waafrika.
Nafikiri huu sio wakati wa kupapukia na kukimbilia chanjo ambayo hata hivyo kwa sasa ni bei ghali. Huu ni wakati wa kuchukua tahadhari kwa ugonjwa huu ambao kimsingi naona ni njama na hila na wala hauna nguvu kama inavyosemwa.
Kama mimi ndio ningekuwa Rais wa taifa hili sidhani kama hata hiyo Corona ingesemwa kwenye vyombo vya habari.
Sidhani kama watu wangekula hata hivyo vidonge vya ARV, sidhani!
Sidhani kama hata tungepewa hata chanjo sijui ya ndui, pepopunda na polio na magonjwa mengine, sidhani.
Kama Afrika inataka kujikomboa, basi lazima tuwe tayari kuhenyeka, kuumia, ikiwezekana kufa mpaka pale akili itakapotukaa sawa.
Hakuna chanjo ya Corona, tupo tayari kukabiliana na matokeo, waganga wetu wa jadi na wa kisasa muingie maabara, huu ndio wakati wenu sasa.
Kama tutaogopa kufa kwa maradhi bila kutafuta suluhu ya madawa sisi kama sisi, tukitegemea madawa ya mtu mwingine basi tunajiua mara elfu elfu bila ya sisi kujua, sio kujiua sisi wenyewe pekee bali tunaua mpaka kizazi chetu kinachokuja.
Naamini kama Uongozi wa Afrika ungekataa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI kipindi kile HIV ilipokuwa imechanganya, tukahangaika kutafuta dawa ya UKIMWI tangu kipindi kile mpaka sasa nina uhakika kabisa leo hii UKIMWI ungekuwa umepata dawa yake. Licha ya kuwa wengi wetu tungeumia na kufa lakini leo hii dawa ingekuwa imepatikana.
Hakuna taifa linaloweza tafutia dawa taifa jingine, hakuna taifa kama hilo hasa kwa wenzetu wazungu.
Sasa tuliogopa Kufa kwa Muda kwa Ugonjwa wa Ukimwi tukakubali kupewa dawa za kupunguza makali ya virusi sasa chamoto ndio tunakipata, kufa lazima tutakufa, pesa sasa tunatoa za madawa, pesa za kondomu, yaani badala ya kusuluhisha ndio tumevurugwa kabisa.
Mimi ningekuwa Kiongozi, hakika ugonjwa ukizuka tutahangaika nao sisi kama sisi, hata tufe najua hatutakufa sote mpaka dawa ipatikane miongoni mwetu, na hiyo ndio itaitwa dawa.
Dawa haiwezi itwa dawa ikiwa haitoki miongoni mwetu, huko ni kujidanganya, nani asiyejua magonjwa ya ajabu ajabu yaliyozuka siku hizi, nani asiyejua matatizo ya uzazi siku hizi, nani asiyejua tatizo la nguvu za kike na za kiume, nani asiyejua hayo?
Najua andiko hili litapingwa na wasomi uchwara wasiojua moja wala elfu moja na moja.
Hakuna chanjo hapa, vita iendeleee, hatutaogopa kupigana tungali tupo kwenye uwanja wa vita.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Mikocheni, Dar es salaam