tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Wakati wa kusaini mikataba miatatu ya uendelezaji bandari kati ya TPA na waarabu wa DPW tuliaminishwa na serikali kuwa hii mikataba ni ya miaka 30. Je, mikataba hii kweli ni ya miaka 30 au tumepigwa?
Nimejaribu kufanya uchunguzi binafsi ndani ya serikali kwa watu wangu wa karibu waliomo kwenye uongozi wa juu serikalini wameniambia nao hawana uhakika kama kweli kipengele hicho kimerekebishwa kutoka umilele hadi miaka 30. Kufuatia kupigwa changa kwenye mkataba wa awali, wananchi tunakosa imani ndio maana tunakuwa na dukuduku kama kweli kipengele hiki kilirekebishwa au la! Sasa sisi tumuamini nani ikiwa serikali haiaminiki?
Nijuavyo mimi mkataba mama (usiokuwa na kikomo) hauwezi kuwa tofauti na mikataba midogo. Tembo hawezi kumzaa sungura kama ambavyo sungura hawezi kumzaa tembo! Na kwa kuwa kitendo cha kumtambulisha Makonda kilienda sambamba na utiaji wa saini za mikataba ya DPW hili huenda limefanyika kwa makusudi ili kuwaondolea utulivu watanzania kutoka kuzungumzia mikataba kwenda kujadili uteuzi wa Makonda.
They know exactly that Tanzanians are good at discussing petty issues leaving aside crucial matters. Na wanafahamu fika kuwa watanzamia ni wasahaulifu. Kabla ya mwaka kuisha, watanzania watakuwa wameishasahau sakata lote la banndari. Ikiwa inawachukua mwezi mmoja tu kusahau mambo sembuse miaka 30!
Kitu kingine kinachowaongezea wasiwasi watanzania ni kitendo cha serikali kuwaalika viongozi wa TEC kwenye hafla ya kutia saini. Tukumbuke TEC walipiga kelele sana kuhusu sakata la DPW. Kwa hiyo, kualikwa kwao inaweza ikawa ni moja ya mbinu za serikali kuwaaminisha wananchi kuwa kila kitu kiko sawa ijapokuwa hata wao TEC hawakuonyeshwa hiyo mikataba mipya.
Ikiwa hii ndiyo hali halisi je sisi wananchi tutaaminije kama kweli mikataba hii ni ya miaka 30? Hili ndilo swali kubwa na gumu ambalo tunajiuliza hadi sasa bila majibu.