Je, mikataba ya DP World iliyosainiwa ina kikomo cha miaka 30? Jibu hili hapa

Tanzania ina Wananchi na Viongozi wajinga sana!
Mikataba ya DP World HAINA UKOMO kwa mujibu wa IGA!
Hiyo miaka 30 wanayosema kwenye HGA HAINA nguvu kwani ikiisha kama kazi bado zinaendelea inaingiwa tena upya kwa mujibu wa IGA!
HUO NDIO UMILELE WA MIKATABA YA BANDARI NA DP World.
Tanzania ni Nchi ya Ajabu sana!
Profesa wa Chuo Kikuu anafundishwa mikataba na Form Four Failure!!!!
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Wakati wa kusaini mikataba miatatu ya uendelezaji bandari kati ya TPA na waarabu wa DPW tuliaminishwa na serikali kuwa hii mikataba ni ya miaka 30. Je, mikataba hii kweli ni ya miaka 30 au tumepigwa?

Nimejaribu kufanya uchunguzi binafsi ndani ya serikali kwa watu wangu wa karibu waliomo kwenye uongozi wa juu serikalini wameniambia nao hawana uhakika kama kweli kipengele hicho kimerekebishwa kutoka umilele hadi miaka 30. Kufuatia kupigwa changa kwenye mkataba wa awali, wananchi tunakosa imani ndio maana tunakuwa na dukuduku kama kweli kipengele hiki kilirekebishwa au la! Sasa sisi tumuamini nani ikiwa serikali haiaminiki?

Nijuavyo mimi mkataba mama (usiokuwa na kikomo) hauwezi kuwa tofauti na mikataba midogo. Tembo hawezi kumzaa sungura kama ambavyo sungura hawezi kumzaa tembo! Na kwa kuwa kitendo cha kumtambulisha Makonda kilienda sambamba na utiaji wa saini za mikataba ya DPW hili huenda limefanyika kwa makusudi ili kuwaondolea utulivu watanzania kutoka kuzungumzia mikataba kwenda kujadili uteuzi wa Makonda.

They know exactly that Tanzanians are good at discussing petty issues leaving aside crucial matters. Na wanafahamu fika kuwa watanzamia ni wasahaulifu. Kabla ya mwaka kuisha, watanzania watakuwa wameishasahau sakata lote la banndari. Ikiwa inawachukua mwezi mmoja tu kusahau mambo sembuse miaka 30!

Kitu kingine kinachowaongezea wasiwasi watanzania ni kitendo cha serikali kuwaalika viongozi wa TEC kwenye hafla ya kutia saini. Tukumbuke TEC walipiga kelele sana kuhusu sakata la DPW. Kwa hiyo, kualikwa kwao inaweza ikawa ni moja ya mbinu za serikali kuwaaminisha wananchi kuwa kila kitu kiko sawa ijapokuwa hata wao TEC hawakuonyeshwa hiyo mikataba mipya.

Ikiwa hii ndiyo hali halisi je sisi wananchi tutaaminije kama kweli mikataba hii ni ya miaka 30? Hili ndilo swali kubwa na gumu ambalo tunajiuliza hadi sasa bila majibu.

Mkuu kwa utafiti nilioufanya kuhusu ukomo wa mikataba ya DP WORLD na nchi kadhaa, naona ukomo wao hauzidi miaka 30.

Nimeainisha baadhi Nchi hizo na ukomo wa mkataba wake kwenye mabano kama ifuatavyo:
1. Djibouti (miaka 30)
2. Romania (miaka 30),
3. India (miaka 30),
4. Canada(miaka 30)
5. Senegal(miaka 25),
6. Angola(miaka 20)
7. na kadhalika ,

Mkuu ukiangalia hapo juu, mpaka hapo ukomo wa mkataba wao hauzidi Miaka 30.

Sisi Tanzania tumesaini mkataba wa ukomo wa miaka 30. Kwa hiyo tuamini kuwa ni kweli mkataba wetu wa HGA ni wa miaka 30.

Mkuu sioni sababu ya ukomo kuwa zaidi kwetu Tanzania tofauti na nchi nyingine.
 
HIVI MAJESHI YETU YANALINDA NINI? MAANA NGUVU YAO NI JESHI KUWALINDA. SASA MUDA HUU NASHAURI ILI TAIFA KUSALIMIKA MAJESHI YAACHE WATANZANIA WACHAGUE VIONGOZI WAO WAWAPENDAO SIO KUIBEBA CCM KIMABAVU TUNAELEKEA HATARI. MAJESHI HAMUONI? MAJESHI SIMAMIENI MAMBO YA HAKI. LAWAMA KUBWA NI MAJESHI YA NCHI BADALA KUWA WAZALENDO KWA MALI NA WANANCHI WAO UZALENDO NI KUMLINDA RAISI HATA KAMA INAIHUJUMU NCHI NA KUVUNJA KATIBA NA SHERIA. HAPA NAONA DAMU INATAFUTWA TANZANIA. HAO WATU KUMWAGA DAMU WAO ETI NI IBADA YAO. HAWAFAI HAO. JESHI JITENGENI NA KUWALINDA HAO WACHACHE NARUDIA NI HATARI
 
Muda si mrefu wafukunyuzi watafanya yao na kuchapisha mitandaoni Kama walivyo fanya mwanzoni na kuleta kelele za kuanza upya…hata wakileta habari za dhulumati wa uhai wa watu - kelele zitakuwa pale pale- ni vema tu waachane na kukabidhi mali hizi za asili ba urithi wetu tubane tuziendeshe wenyewe Kama Wahabeshi/ Ethiopia wanavyo endesha mashirika yao- mbona wao wanaweza, Sisi Kwa nini tushindwe?
 
Baada ya kikao cha head line ilikua PAUL MAKONDA na sio DPW tena wakaenda mbali zaidi na kuaminisha uma kua tuko kwenye mwelekeo sahihi.
Nchi hii ni ya kipumbavu sana. Bora isingepata uhuru kutoka kwa wakoloni ingekuwa mbali sana kiuchumi. Namlaumu sana Nyerere kwa kiherehere chake cha kutuletea uhuru huu wa bandia. Bora mkoloni mweupe (mwingerza) kuliko mkoloni mweusi (CCM).
 
Muda si mrefu wafukunyuzi watafanya yao na kuchapisha mitandaoni Kama walivyo fanya mwanzoni na kuleta kelele za kuanza upya…hata wakileta habari za dhulumati wa uhai wa watu - kelele zitakuwa pale pale- ni vema tu waachane na kukabidhi mali hizi za asili ba urithi wetu tubane tuziendeshe wenyewe Kama Wahabeshi/ Ethiopia wanavyo endesha mashirika yao- mbona wao wanaweza, Sisi Kwa nini tushindwe?
Huwa najiuliza: hivi tulishapata uhuru au kuna ukombozi mwingine tunausubiri? Mbona kama vile bado nchi ipo utumwani? Ni nchi gani hii isiyojitambua? Nadhani pia wananchi wanapaswa kuamka na kuanza kuwanyuka hawa wakoloni weusi (CCM) ili kuwaonyesha kuwa hatufurahishwi jinsi wanavyoshirikiana na waarabu na wahindi kunyonya rasilimali za wanyonge. Haikubaliki kuona CCM wakiendelea kufyonza rasilimali za wananchi tukiwa tumekaa kimya.
 
Mkuu kwa utafiti nilioufanya kuhusu ukomo wa mikataba ya DP WORLD na nchi kadhaa, naona ukomo wao hauzidi miaka 30.

Nimeainisha baadhi Nchi hizo na ukomo wa mkataba wake kwenye mabano kama ifuatavyo:
1. Djibouti (miaka 30)
2. Romania (miaka 30),
3. India (miaka 30),
4. Canada(miaka 30)
5. Senegal(miaka 25),
6. Angola(miaka 20)
7. na kadhalika ,

Mkuu ukiangalia hapo juu, mpaka hapo ukomo wa mkataba wao hauzidi Miaka 30.

Sisi Tanzania tumesaini mkataba wa ukomo wa miaka 30. Kwa hiyo tuamini kuwa ni kweli mkataba wetu wa HGA ni wa miaka 30.

Mkuu sioni sababu ya ukomo kuwa zaidi kwetu Tanzania tofauti na nchi nyingine.
Mkuu Tanzania ina upumbavu wa kipekee. Acha kufananisha hii takataka na nchi zinazojitambua. Walah sijawahi kushuhudia nchi ya kilaghai kama Tanzania hapa ulimwenguni.
 
Mkuu kwa utafiti nilioufanya kuhusu ukomo wa mikataba ya DP WORLD na nchi kadhaa, naona ukomo wao hauzidi miaka 30.

Nimeainisha baadhi Nchi hizo na ukomo wa mkataba wake kwenye mabano kama ifuatavyo:
1. Djibouti (miaka 30)
2. Romania (miaka 30),
3. India (miaka 30),
4. Canada(miaka 30)
5. Senegal(miaka 25),
6. Angola(miaka 20)
7. na kadhalika ,

Mkuu ukiangalia hapo juu, mpaka hapo ukomo wa mkataba wao hauzidi Miaka 30.

Sisi Tanzania tumesaini mkataba wa ukomo wa miaka 30. Kwa hiyo tuamini kuwa ni kweli mkataba wetu wa HGA ni wa miaka 30.

Mkuu sioni sababu ya ukomo kuwa zaidi kwetu Tanzania tofauti na nchi nyingine.
Ungekuwa na akili japo kidogo ungejiuliza pia kama hizo Nchi pia ziliridhia IGA.
Kwa mujibu wa IGA iliyoridhiwa na Bungee la Tanzania ni kwamba hata kama hiyo miaka 30 ikiisha na kazi zinaendelea basi mikataba ya DP World itakuwa renewed!
Hapo ndo kuna dhana ya UMILELE!
 
Sijapata kuona serikali ya kitapeli zaidi ya hii anayoiendesha Samia.
Sasa hata kule kufunikafunika hawafanyi. Aibu hawana tena.
Saa100 mishipa ya aibu imeshaaktika ukitoa ule ushungi kinachobakia kama ni mhuni tu flani
 
Huwa najiuliza: hivi tulishapata uhuru au kuna ukombozi mwingine tunausubiri? Mbona kama vile bado nchi ipo utumwani? Ni nchi gani hii isiyojitambua? Nadhani pia wananchi wanapaswa kuamka na kuanza kuwanyuka hawa wakoloni weusi (CCM) ili kuwaonyesha kuwa hatufurahishwi jinsi wanavyoshirikiana na waarabu na wahindi kunyonya rasilimali za wanyonge. Haikubaliki kuona CCM wakiendelea kufyonza rasilimali za wananchi tukiwa tumekaa kimya.
Umetoa maoni kuntu Sana Na Pokea Maua yako Ndugu, hawa ccm Kwa kweli sijui ni Kwa Nini hawana uchungu Na nchi yetu... halafu wanajeshi wa Jwtz Ni Kama vile hawawaoni. Tunawalilia Jeshi la wananchi Kama lilivyo Jina Lao lakini Ni Kama vile hawasikii kilio chetu wananchi... sasa ya nini kuitwa jeshi la wananchi ili hali wametushiti na kuicha ccm iitafune nchi Kama mchwa bila aibu wala kificho? Haya mambo ya Mikataba yapo toka Enzi za karl peters lakini ccm bado inatembelea mule mule... tumechoka- Jwtz sasa tukomboeni toka makucha ya ccm...
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Wakati wa kusaini mikataba miatatu ya uendelezaji bandari kati ya TPA na waarabu wa DPW tuliaminishwa na serikali kuwa hii mikataba ni ya miaka 30. Je, mikataba hii kweli ni ya miaka 30 au tumepigwa?

Nimejaribu kufanya uchunguzi binafsi ndani ya serikali kwa watu wangu wa karibu waliomo kwenye uongozi wa juu serikalini wameniambia nao hawana uhakika kama kweli kipengele hicho kimerekebishwa kutoka umilele hadi miaka 30. Kufuatia kupigwa changa kwenye mkataba wa awali, wananchi tunakosa imani ndio maana tunakuwa na dukuduku kama kweli kipengele hiki kilirekebishwa au la! Sasa sisi tumuamini nani ikiwa serikali haiaminiki?

Nijuavyo mimi mkataba mama (usiokuwa na kikomo) hauwezi kuwa tofauti na mikataba midogo. Tembo hawezi kumzaa sungura kama ambavyo sungura hawezi kumzaa tembo! Na kwa kuwa kitendo cha kumtambulisha Makonda kilienda sambamba na utiaji wa saini za mikataba ya DPW hili huenda limefanyika kwa makusudi ili kuwaondolea utulivu watanzania kutoka kuzungumzia mikataba kwenda kujadili uteuzi wa Makonda.

They know exactly that Tanzanians are good at discussing petty issues leaving aside crucial matters. Na wanafahamu fika kuwa watanzamia ni wasahaulifu. Kabla ya mwaka kuisha, watanzania watakuwa wameishasahau sakata lote la banndari. Ikiwa inawachukua mwezi mmoja tu kusahau mambo sembuse miaka 30!

Kitu kingine kinachowaongezea wasiwasi watanzania ni kitendo cha serikali kuwaalika viongozi wa TEC kwenye hafla ya kutia saini. Tukumbuke TEC walipiga kelele sana kuhusu sakata la DPW. Kwa hiyo, kualikwa kwao inaweza ikawa ni moja ya mbinu za serikali kuwaaminisha wananchi kuwa kila kitu kiko sawa ijapokuwa hata wao TEC hawakuonyeshwa hiyo mikataba mipya.

Ikiwa hii ndiyo hali halisi je sisi wananchi tutaaminije kama kweli mikataba hii ni ya miaka 30? Hili ndilo swali kubwa na gumu ambalo tunajiuliza hadi sasa bila majibu.
Kweli 100%
 
🙏🙏🙏
 
They know exactly that Tanzanians are good at discussing petty issues leaving aside crucial matters. Na wanafahamu fika kuwa watanzamia ni wasahaulifu.
Aisee.
Teua Tengua.

Fupa la Makonda na Sasa la Mishahara....na mengineyo ya kutengeneza.

....
 
HIVI MAJESHI YETU YANALINDA NINI? MAANA NGUVU YAO NI JESHI KUWALINDA. SASA MUDA HUU NASHAURI ILI TAIFA KUSALIMIKA MAJESHI YAACHE WATANZANIA WACHAGUE VIONGOZI WAO WAWAPENDAO SIO KUIBEBA CCM KIMABAVU TUNAELEKEA HATARI. MAJESHI HAMUONI? MAJESHI SIMAMIENI MAMBO YA HAKI. LAWAMA KUBWA NI MAJESHI YA NCHI BADALA KUWA WAZALENDO KWA MALI NA WANANCHI WAO UZALENDO NI KUMLINDA RAISI HATA KAMA INAIHUJUMU NCHI NA KUVUNJA KATIBA NA SHERIA. HAPA NAONA DAMU INATAFUTWA TANZANIA. HAO WATU KUMWAGA DAMU WAO ETI NI IBADA YAO. HAWAFAI HAO. JESHI JITENGENI NA KUWALINDA HAO WACHACHE NARUDIA NI HATARI
Mkuu umeongea ukweli tupu, hasa kwa poliCCM ambao wako tayari kuua wanasiasa wa upinzani kwa maagizo ya rais aliyeko madarakani bila kuhoji uhalali wa kuondoa uhai wa mtu kisa madaraka. Tazama kile walichomfanyia Tundu Lissu utagundua kuwa majeshi nayo yameambukizwa uchawa na serikali ya kiqumer ya CCM. Inahudhunisha sana.
 
Umetoa maoni kuntu Sana Na Pokea Maua yako Ndugu, hawa ccm Kwa kweli sijui ni Kwa Nini hawana uchungu Na nchi yetu... halafu wanajeshi wa Jwtz Ni Kama vile hawawaoni. Tunawalilia Jeshi la wananchi Kama lilivyo Jina Lao lakini Ni Kama vile hawasikii kilio chetu wananchi... sasa ya nini kuitwa jeshi la wananchi ili hali wametushiti na kuicha ccm iitafune nchi Kama mchwa bila aibu wala kificho? Haya mambo ya Mikataba yapo toka Enzi za karl peters lakini ccm bado inatembelea mule mule... tumechoka- Jwtz sasa tukomboeni toka makucha ya ccm...
Tatizo mtu yeyote anayeonekana kuwa na uchungu na rasilimali za nchi anaitwa mpinzani. Najiuliza: hivi ndani ya CC hakuna mzalendo hata mmoja? Ina maana wazazalendo wamebaki ndani ya upinzani tu? Makubwa!
 
Makonda namuona kama mtu sahihi sana kuliko watangulizi wake tukiondoa Polepole, kazi hii anaiweza ndiyo maana Chadema wanamgwaya na hawakulitegemea hili, kutokea walijua amezikwa jumla wasubili mziki wake.
 
Back
Top Bottom