Je, Mizimu na mashetani ndio huchoma shule zetu?

Je, Mizimu na mashetani ndio huchoma shule zetu?

Matatizo ya moto yanatokana na ujinga,maradhi na umaskini.

Nitafafanua.

Ujinga.
Kutojua athari za matumizi kwa njia ya wizi ya umeme mashuleni mfano heater.
Wanafunzi wanazuiliwa kutumia vitu vingi vya umeme ikiwepo pasi,heater,hata simu na laptops. Sasa wengi hufanya utundu wa kujiungia kwa wizi ili watumie vitu hivyo.

Ujinga mkubwa uliowekezwa hapo ni wakati wa wiring,wahusika huweka nyaya na mifumo inayoruhusu matumizi ya taa tu na kuamini kuwa wanafunzi hawatakiwi kutumia chochote zaidi ya taa kwa ajili ya mwanga.Na kwa hiyo mifumo huruhusu umeme mdogo kwa matumizi ya kawaida kabisa katika bweni.

Maradhi

Unaweza kudhani ni utani,ila watanzania wengi wana maradhi yanayoathiri afya ya akili.Kuna kitu wanaita sadism. Hii ni ile hali ya mtu kupata furaha na raha anapoona binadamu mwingine anateseka.

Kuna walimu wengi wanaamini kuwa mwanafunzi anatakiwa kuteseka ndiyo anapata akili.Wanafurahia sana kuona hawa watoto wakiteseka.Ndiyo maana wanaona kuwa hawana haki ya kutumia umeme kunyooshea nguo,hata kuchemsha maji ya kunywa,ingawa shule haziwaandalii maji safi na salama.

Huu ugonjwa wanao hata viongozi wetu wengi.Wanafurahia sana kuona mtu anapoteseka.Kama kukiwa shwari,utashangaa tu kinatokea kitu ili mradi watu wapate misuko suko.


Umaskini.

Kukosa pesa ya kutosha kugharimia umeme na ujenzi bora wa miundo msingi yake.
Kuishi kwa kuwaza kimaskini na kuona umeme kama kitu cha starehe.
Umaskini ni mama wa yote hapo juu.

Kutokana na hayo yote,tumekuwa tayari kushuhushudia hasara ya mali na hata maisha.Tumeshindwa kuhalalisha matumizi ili tujipange kuweka miundo msingi imara katika mashule yetu.
Mungu atusaidie sana
 
Back
Top Bottom