Najibu hapo mwisho kwenye mchango wa mwanamke. Mke wako ana haki na mali zako hata kama amezikuta.. mchango wake sio lazima uwe pesa..Kama anatekeleza majukumu ya kulea familia na kukutunza huo ni mchango tosha. Haki anayo kama hajakiuka mambo mengine ya mahusiano yenu.
Kuhusu mtoto wa kambo subiri wanasheria wabobezi waje. Ila mtoto kufahamu baba yake mzazi ni Jambo la kheri..sema bidada kakiuka makubaliano yenu.
Binafsi niliolewa nikiwa nina mtoto. Mume akanipa masharti kama hayo nikaona poa tu maana baba mtoto hakuwa responsible kwa mwanae. Na jina akataka nimbadilishe atumie la kwake nikakubali lakini kishingo upande.
Miaka inasonga sioni akitekeleza majukumu kwa mtoto ipasavyo..hata ukaribu wa baba na mtoto hakuna, anatoa matunzo kwa kujivuta vuta as if sio mwanae vile. Uzuri ni kwamba mie sio mlalamishi naridhika na chochote kidogo ila ikawa inaniuma sioni kama mtoto anatunzwa ipasavyo na uwezo anao mkubwa tu. Napambana mwenyewe kila siku ninastress za matunzo.
Nikaona isiwe taabu.. nikamrudishia jina lake la awali..nikamtafuta baba yake na shangazi zake nikawakutanisha na mtoto wao. Maana niliona nampeleka mtoto kwenye ukoo ambao ipo wazi kabisa hawamchukulii uzito, why nimpe jina lao?Now nina amani moyoni!
Kama jamaa angelibeba jukumu ipasavyo nisingefanya hivyo. Na mbaya zaidi mtoto alianza kumuulizia baba yake mzazi..loh nikasema isije niletea matatizo makubwa baadae.
Sent using
Jamii Forums mobile app