Naamini, 'mtoto' anarithi mali za 'mzazi' wake.
'Mzazi'haijalishi ni baba au mama kwa sababu, ikiwa mama yake ataachana na baba yake, basi katika mgawanyo wa mali mama atapata sehemu gake ambayo na "mtoto wa kambo" anaweza kurithi kwa mama yake.
Imekuwa ni desturi kwamba baba ndiye mwenye kurithisha mali za familia na sio mama, na hata kama baba akitangulia mbele za haki basi mali inagawanywa na familia inasambaa (bila kujali kuwa mama yupo), ikiwa ni tofauti na pale inapotokea mama akatangulia mbele za haki kabla ya baba huwa hakuna mgawanyo n.k
Naamini, japo sheria haimtambui mtoto wa kambo moja kwa moja, lakini ana haki ya kupata sehemu ya mali za mzazi wake pekee, kama ni baba au mama, lakini wale watoto waliozaliwa na pande zote mbili wao watarithi katika jumuisho la 'familia'.
Kumbuka, mama ana mchango wake katika mali za familia, kwa mtazamo wangu hata kama utarithisha watoto wa ndoa...najiuliza tu wakati unakutana na huyu mama akiwa na mwanae hakuwa na mali yoyote kiasi cha kutodhani mwanaye anastahili kitu pia?
Nadhani suala lenu linahitaji kuchimbwa vizuri, nami naona kabisa kuna sehemu ya mali atapata mtoto wa kambo kupitia mama yake (hata kama sheria haijataja moja kwa moja).
Sent using
Jamii Forums mobile app