Je mtu akifa, tozo za kodi endelevu kama za ardhi, zinasimama ?

Je mtu akifa, tozo za kodi endelevu kama za ardhi, zinasimama ?

espy

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2021
Posts
363
Reaction score
706
Mwenye mali akifa, kodi za ardhi zinaendelea kuhesabiwa ?

Nani anadaiwa ?

Shauri la Mirathi limeisha baada ya miaka 7, Daudi umepewa nyumba ya marehemu babaako. Kupata nyaraka za umiliki mpya unaambiwa nyumba ina deni la kodi ya ardhi miaka 7.

Nani alipe ? Kwanini ?
 
Madai yoyote Huwa hayafi na Mtu. Yataendelea kwa warithi wake. Nendeni mkalipe Kodi kuepuka usumbufu baadae.

Kumbuka Ardhi ni ya Serikali, anayemiliki anapewa haki tu ya kutumia kwa miaka kadhaa. Ikiisha ataomba tena na anaweza akapewa au asipewe

Kumbuka pia, kutolipa Kodi ni Moja ya sababu zinazoweza kupelekea hati kufutwa.
 
Wabongo wakati mwingine maswali yetu ya ajabu sana! Sasa huyo mwenye nyumba akifariki wewe mrithi kama ulikuwa unakaa humo utaendelea kukaa au utafunga nyumba na kuondoka? Na je utapangisha na kuchukua hela? Maana mwenye nyumba ameshakufa!
 
Mwenye mali akifa, kodi za ardhi zinaendelea kuhesabiwa ?

Nani anadaiwa ?

Shauri la Mirathi limeisha baada ya miaka 7, Daudi umepewa nyumba ya marehemu babaako. Kupata nyaraka za umiliki mpya unaambiwa nyumba ina deni la kodi ya ardhi miaka 7.

Nani alipe ? Kwanini ?
Unalipa mrithi boss
 
Kwani marehemu kaondoka na nyumba yake?
Marehemu alipoondoka madeni yake , mali na amana kamwachia mwenzaje anaitwa Estate.

Estate of Marehemu ndio adaiwe.
 
Marehemu alipoondoka madeni yake , mali na amana kamwachia mwenzaje anaitwa Estate.

Bwana Estate ndio adaiwe.
Sasa tukirudi kwenye Estate Account ni lazima hayo madeni yalipwe na mrithi wa nyumba husika kama wakati wa mgawanyo wa mirathi madeni hayakuhusihwa. Ilitakiwa assets za marehemu zihesabiwe kisha kuthaminishwa ameacha kiasi gani. Kisha madeni yake yote yalipwe kupitia mali alizonazo. Kama hakuna pesa basi asset mojawapo inauzwa ili kulipa.

Sasa kama walikaa kimya basi kila mnufaika atawajibika kulipa deni linalotokana na urithi wake otherwise kama hajaridhishwa arudi kwenye vikao vya mirathi. Kama ni yeye pekee mnufaika basi alipe tu. Deni huwa halifi
 
Back
Top Bottom