Unalipa mrithi bossMwenye mali akifa, kodi za ardhi zinaendelea kuhesabiwa ?
Nani anadaiwa ?
Shauri la Mirathi limeisha baada ya miaka 7, Daudi umepewa nyumba ya marehemu babaako. Kupata nyaraka za umiliki mpya unaambiwa nyumba ina deni la kodi ya ardhi miaka 7.
Nani alipe ? Kwanini ?
Unalipa mrithi boss
Marehemu alipoondoka madeni yake , mali na amana kamwachia mwenzaje anaitwa Estate.Kwani marehemu kaondoka na nyumba yake?
Sasa tukirudi kwenye Estate Account ni lazima hayo madeni yalipwe na mrithi wa nyumba husika kama wakati wa mgawanyo wa mirathi madeni hayakuhusihwa. Ilitakiwa assets za marehemu zihesabiwe kisha kuthaminishwa ameacha kiasi gani. Kisha madeni yake yote yalipwe kupitia mali alizonazo. Kama hakuna pesa basi asset mojawapo inauzwa ili kulipa.Marehemu alipoondoka madeni yake , mali na amana kamwachia mwenzaje anaitwa Estate.
Bwana Estate ndio adaiwe.