Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Mkuu UMUGHAKA ni mke wangu wa ndoa kabisa,ndoa ya kanisani,na vyeti via ndoa ninavyo,tumejaaliwa watoto wawili,wote wapo shule na vyeti vyao vya kuzaliwa ninavyo,mke wangu tulimzika nyumbani kwangu,hapa hapa ninapoishi sasa.
Mkuu Capt Tamar hilo ni jambazi wewe lifungulie mashitaka kaka na tena hakikisha anakulipa vyote alivyopora!,Daah ila sielewi ulikubali vipi huyo jamaa akawa msimazi wa mirathi wakati mwenye mali upo au ulirogwa mkuu?,maana kwa akili ya kawaida naona kama haiingi akilini!
 
Hatujui kulikuwa na mazingira gani ikawa hivyo lakini huenda kuna sababu ingawa simshauri aanike kila kiyu humu.

Yeye akajieleze kinagaubaga kwa Mwanasheria wajue kwa kuanzia.
Mkuu@May day nilichoeleza ni 95%ya uhalisia,sina cha kuficha,nahitaji ushauri wako tafadhali.siondoki hapa
 

Unaona kilichotokea ni upande wa mke wake wanafahamu mali ambazo Dada yao alikua nazo kabla ya kukutana na jamaa na inaonekana mke wa jamaa alikua vyema kiuchumi kuliko mume ndio maana familia ya mke ikamteua kaka mtu kusimamia hasa mali wanazofahamu mtoto wao alichuma mwenyewe na mume wa marehemu anachukuliwa kama Mario
 
Kufiwa na mke si jambo rahisi kaka,hata mimi huwa najiuliza nilikubalije?I wish ungekuwepo siku hiyo,maybe ungekuwa msaada kwangu,nahitaji kutoka hapa sasa,msaada tafadhali.
 
Kwa kuwa huyo Shemeji keshaonesha muelekeo wa kipigaji.

Mkienda kisheria mtihani niuonao hapo ni namna ya kuthibitisha kwamba hiyo nyumba ni kati ya mali za ndoa, maana hapa nyaraka ndio muhimu.
 
Mkuu Arovera hiyo ni endapo wangekuwa hawajafunga ndoa na hawana watoto,sasa wamefunga ndoa na wamekuwa mume na mke!,Hiyo familia ya mwanamke ni wapumbavu!,any way nadhani afuate sheria
 
Wewe ni dereva wa daladala nini?

Umetiririka hakuna cha paragrafu, nukta, koma, nk.
 
Wewe ni mind reader,hata mimi naona kabisa labda wanadhani hivyo,ila ukweli ni tofauti kabisa brother,natokaje hapa?
 
Mkuu@May day nilichoeleza ni 95%ya uhalisia,sina cha kuficha,nahitaji ushauri wako tafadhali.siondoki hapa
Sawa ndugu, ingawa wanasema Msema pweke ni mshindi...ila kama ndivyo basi hiyo familia ya Mkeo wana viashiria vya kudhulumu...na hapo ni mpaka Mahakamani.

Ushauri ni kutafuta Mwanasheria tu na kufungua shaur Mahakamanii...wewe andaa nyaraka zote muhimu.

Na je vipi hao ndugu wengine wa Mkeo, hakuna mnayesikilizana au wote wapo na Kaka yao?.
 

Una mikono miwili, macho, akili na kazi, achana na vitu hivyo, tafuta maisha, uhasama wa hivi umeacha watoto wengi yatima! Nani alikwambia haki inapatikanaga kwenye hela za mke?
 
Kweli,familia yao ina dada watatu,kaka watatu,na mume wa dada yao mkubwa ndiyo msemaji wa familia yao,kiufupi hawa dada zake wawili wananipa ushirikiano kiasi,kaka zake wawili pia wananisapoti kiaina,ila kuna huyo dada yao wa nje ya ndoa ndiyo anamsapoti shemeji kidogo,huyo dada mkubwa aliniambia kuwa ndugu zake hawamthamini kwa kuwa si mtoto wa mama yao,alikuja na baba,na ananipa ushirikiano wa kutosha,ila anasema hana sauti kwao.
 
Natamani ningekua karibu sana na huyo shemeji yako, nimwambie shida anayotafuta ila sina nafasi.
Kumwombea afunguliwe aachane na mali za marehemu asitamuacha mtu salama mpaka mwisho wake.
 
Una mikono miwili, macho, akili na kazi, achana na vitu hivyo, tafuta maisha, uhasama wa hivi umeacha watoto wengi yatima! Nani alikwambia haki inapatikanaga kwenye hela za mke?
Siyo za mke mkuu,kuna nyingi zangu pia.
 
Pole jamaa, nafikir busara ni kuitisha kikao ndug upand wako na wao myazungumze.

Ikishindkan tumia ubabe, ukifel ndo uende kweny hayo masheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…