Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Una makosa mengi ulifanya mkuu

1. Kosa la kwanza
Kununua kiwanja Cha ukweni kwako

2. Kosa la pili,
Kujenga kwenye kiwanja Cha ukweni

3. Kosa la tatu,
Kumruhusu shemej yako kusimamia ujenzi

4. Kosa la nne,
Kumruhusu shemej yako kusimamia Kodi za wapangaji

5. Kosa la tano,
Kuruhusu shemej yako kua msimamizi wa mirathi

Nnachokiona hapa,
Hata kabla ya mkeo hajafariki,
Haukua na power yoyote ya kimaamuzi kwenye familia yako Kama baba wa familia

Kingine,
Hata baada ya mkeo kufariki,
Bado inaonyesha unakosa power ya kimaamuzi Kama baba wa familia yako.
Very TECHNICAL MISTAKES!

Wengine sie ukweni na upande wa wakwe tunasalimiana tu na kushirikiana issues za msingi. Hayo ya kuwekeza unawashirikisha wakwe ili iweje, huna ndugu zako?
 
Ma ndugu ya kibongo sio ya kuyakaribisha hata kukaa nayo home huwa ndo masoma weakness point ya familia yenu akifa ndugu yao utasumbuana nayo kama nzi kwenye kimba
 
Ww ni mtu mzima,kwa nini ulishindwa kushinikiza ili uwe msimamizi wa.mirathi.Kama kweli una haki katika mali hizo mkatae huyo msimamizi.Wanasheria watakusaidia zaidi
Walimseti mtu wa kukusumbua wewe ukabariki msimamizi kaka yake kwani wewe ni ndugu yao mmefiwa na mama yenu au? Kuna haja ya kuandika mirathi kabisa kupunguza huu ujinga
 
Hizo mali wa kusimamia ni wewe tafuta mwanasheria fungua kesi mahakamani utashinda
Kweli mkuu,asante kwa kunipa matumaini, naamini nitashinda,nitakushukuru pia baada ya ushindi,ubarikiwe sana kaka.
 
Walimseti mtu wa kukusumbua wewe ukabariki msimamizi kaka yake kwani wewe ni ndugu yao mmefiwa na mama yenu au? Kuna haja ya kuandika mirathi kabisa kupunguza huu ujinga
Nimeshakiri kosa mkuu,ndiyo maana nimekuja kwenu mnisaidie kutoka hapa nilipo,hii issue inaniumiza kichwa sana.
 
Nikisoma reply zako zinaonesha wew ni mpole sana.Em waoneshe upande wako wa pili wakuheshim. Chunga isitengeneze shimo akili kumkichwa
Nadhani upole unatafsiriwa tofauti,ukiwauliza watu wawili kama mimi ni mpole mmoja atasema ndiyo na mwingine atasema hapana,hapa natafuta suluhu ya kisheria,lakini kuna pengine nimepeleka kijeuri na ika fit,sipo kama unavyonisoma mkuu,kila kitu kinaenda kwa utaratibu wake,hapa nahitaji ushauri wa kisheria zaidi,asante sana mkuu
 
Up
Nadhani upole unatafsiriwa tofauti,ukiwauliza watu wawili kama mimi ni mpole mmoja atasema ndiyo na mwingine atasema hapana,hapa natafuta suluhu ya kisheria,lakini kuna pengine nimepeleka kijeuri na ika fit,sipo kama unavyonisoma mkuu,kila kitu kinaenda kwa utaratibu wake,hapa nahitaji ushauri wa kisheria zaidi,asante sana mkuu
Update
 
Mpk sasa umethibitisha ww n Punga kabisa... Mwanaume gan unashindwa kusimamia mirathi ya mke wako??

Ungepewa watoto je ungeweza??

Tunarud kwenye ushauri sasa,
Kuchaguliwa kuwa msimamizi wa mirathi haimaanishi ndo imeisha, Subiri wafungue kesi ya mirathi mahakaman then utaenda kuweka caviet (zuio) ya mtu huyo kuwa msimamizi wa mirathi

Utatoa sabab zako mahakaman then zikiwa na mashiko basi mahakama itamtengua huyo msimamizi.

Kwa ushauri zaidi mwone mwanasheria wako
 
Habari za shughuli ndugu zangu,

Naombeni mnishauri kwa jambo hili ambalo naona nalazimika kulifanya, nilipata msiba kwa kufiwa na mke wangu wa ndoa mwanzoni mwa mwaka huu, baada ya mazishi kuna kikao cha ndugu kilikaa kujadili mustakabali wa familia kama ilivyo desturi sasa kwenye kikao kile, wengi walikuwa ni ndugu wa mke wangu.

Wengi wao hata nilikuwa siwafahamu, kikao kikamteua shemeji yangu ambaye ndiye kaka mkubwa wa mke wangu awe msimamizi wa mirathi, mke wangu alikuwa na mali alizochuma yeye mwenyewe kabla hatujaoana, na mimi nilikuwa na zangu binafsi.

Na kuna kiwanja alikinunua kwa kaka yake huyohuyo wakati tukiwa tunaishi pamoja, higher kiwanja tukajenga nyumba za kupangisha, na tukapata mpangaji mmoja aliyepanga vyumba vyote 8, wakati huo mimi nilikuwa nipo nje ya mkoa kikazi.

Kwa hiyo, hata wakati ujenzi unaendelea, mimi sikuwepo, mtu aliyekuwa akisimamia ujenzi ni huyo kaka wa mke wangu, kwakuwa hakuwa na shughuli yoyote kipindi hicho hivyo nikawa namlipa asaidie kusimamia ujenzi na hata shughuli nyinginezo za ujenzi kwenye nyumba nyingine niliyokuwa naijenga mtaa mwingine ambayo ndiyo tunayoishi hata sasa, sasa tabu imekuja baada ya yeye kukabidhiwa jukumu la kusimamia mirathi.

Kwanza alikosana na yule mpangaji hali iliyomlazimu mpangaji yule kuhama mimi nikiwa sipo, kisha akawapangishia wapangaji wengine bila kunitaarifu.

Baadaye kodi ikaanza kusumbua, mara anitumie mara asitume, nikaamua kumfuata ili anieleze tatizo ni nini, baada ya kufokeana sana akaniambia yeye ndiye msimamizi wa mali zote kwa hiyo sipaswi kumpangia.

Ni takriban miezi mitano sasa hajaleta kodi ya nyumba, wale wapangaji sijui aliwaseti vipi, maana kila nikijaribu kuwafata huwa wananikwepa, nadhani hajafungua mirathi mahakamani kwani kuna vielelezo ambavyo angepaswa kuvipata kutoka kwangu ila hakuwahi kuniomba nimpatie, sasa nafikiri nimpeleke mahakamani, ila huko sina nijualo especialy kwa kesi ya aina hii.

Naamini hapa kuna wajuzi wa mambo kama haya. Hivyo naomba mchango wenu wa mawazo ili niweze kuilinda haki ya familia yangu nikiwa na ujasiri.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
Hicho kikao chenu kilikua cha kijinga ,.mlitakiwa kumalizana kwenye kikao kila mtu apite na chake
Hio sio familia yako tena ,chukua chako waachie Chao wasismamie watakavyo
 
Back
Top Bottom