Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Kuhusu yeye kufungua maombi ya usimamizi wa mirathi sina hakika nalo kwa asilimia 100,na ndiyo nikasema nina mashaka kuwa hakwenda mahakamani, kwa kuwa huko angetakiwa kwenda na vielelezo ambavyo hana, alichonacho ni barua ya muhtasari wa kikao cha familia tu na je naweza kwenda mahakamani kuuliza kama alikwenda kufungua shauri hilo?
Sasa hapo inabidi ufuatilie mahakamani kama kumewahi funguliwa mirathi, fuatilia pote pote Mahakama ya Mwanzo na Mahakama Kuu.

Ukishakuwa na uhakika sasamambo mengine ndio yataweza kuendelea vizuri kaka.
 
Asante mkuu
 
Huna hata haja ya kutafuta Mwanasheria, kama upo Dar nenda pale Temeke kwenye Mahakama ya familia.
Na umesema hajakuomba vielelezo, unahisi bado hajafungua mirathi Mahakamani. Sasa wahi wewe kwenda, utapata vielelezo vyote.
Na huenda hataki kufungua, ili aendelee kuneemeka na mali za Marehemu.

Hizo ni mali za watoto, nimefiwa na Mama mwaka jana, mali zake zote tumepewa watoto wake wawili tuliobaki. Zilizobaki ni walizochuma na Baba sababu yuko bado hai.

Popote ulipo kesho nenda kwenye Mahakama inayoshughulikia mambo ya familia.
Kikao kitakaa tena ndugu wa pande zote, na utapewa kuwa msimamizi wa mali za mpedwa mkeo. Pole kwa kufiwa na mke.
 
Kweli,familia yao ina dada watatu,kaka watatu,na mume wa dada yao mkubwa ndiyo msemaji wa familia yao,kiufupi hawa dada zake wawili wananipa ushirikiano kiasi,kaka zake wawili pia wananisapoti kiaina,ila kuna huyo dada yao wa nje ya ndoa ndiyo anamsapoti shemeji kidogo,huyo dada mkubwa aliniambia kuwa ndugu zake hawamthamini kwa kuwa si mtoto wa mama yao,alikuja na baba,na ananipa ushirikiano wa kutosha,ila anasema hana sauti kwao.
Mwenyezi mungu anisamehe ila hiyo familia mbona ya ajabu sana?

Inakuwaje tena kwenye hiyo familia Mme wa Dada yao mkubwa(yaani mkwe wao,ambao kimsingi hawana nae nasaba hata kidogo isipokuwa ni mtu kaoa tu kwao) anakuwa ndio msemaji wa familia??

Yaani shemeji yangu(kamuoa Dada yangu) aje ndio awe msemaji tena kwenye familia yetu Duuh

Au huyo Mme wa Dada yao mkubwa ana vijisenti na kielimu kidogo nini?(kama ndivyo hivyo hiyo familia basi ni wajinga na huyo bwana Mme wa Dada yao mkubwa nae ni mjinga Mara dufu, in any how mtu mwenye akili zake haijalishi mwenyezi mungu kampa nini kwenye maisha yake hawezi kukubali yeye ndio awe msemaji ukwenu kwenye ukoo ambao sio wake na hana nao udugu, labda ushauri wakimuomba tena pia yatakiwa auotoe kwa adabu kubwa isionekane kama ndio majibu)

Kama hiyo ndio nature ya hiyo familia basi hao ni wajinga bwana Capt Tamar na wewe cha kufanya hapo baada ya kupata ushauri humu jukwaani, usisahau kuwa consult wataalam wa sheria wakupe muongozo andaa vielelezo panga mashambulizi tena kimya kimya fungua kesi na haki itapatikana
 
Huyo kaka mtu ana tofauti gani na mwenda zake[emoji41]

Ila pole sana tafuta mwanasheria atakupa muongozo na usimfiche kitu ili ajue ananyumbulishaje vifungu.

Ukishindwa nitafute tukamuombe mungu aamue ugomvi[emoji23][emoji23]
 
Kwanza nikuulize mirathi ilishafunguliwa kisheria mahakamani? Kuhusu mali za mke marehemu wako?
 
Pole sana kwa yote tafuta Mwanasheria haki yako na Watoto ipatikane.
 
Huna hata haja ya kutafuta Mwanasheria, kama upo Dar nenda pale Temeke kwenye Mahakama ya familia.
Na umesema hajakuomba vielelezo, unahisi bado hajafungua mirathi Mahakamani. Sasa wahi wewe kwenda, utapata vielelezo vyote.
Na huenda hataki kufungua, ili aendelee kuneemeka na mali za Marehemu.

Hizo ni mali za watoto, nimefiwa na Mama mwaka jana, mali zake zote tumepewa watoto wake wawili tuliobaki. Zilizobaki ni walizochuma na Baba sababu yuko bado hai.

Popote ulipo kesho nenda kwenye Mahakama inayoshughulikia mambo ya familia.
Kikao kitakaa tena ndugu wa pande zote, na utapewa kuwa msimamizi wa mali za mpedwa mkeo. Pole kwa kufiwa na mke.
Asante kwa ushauri mzuri dada,nipo arusha,ila nitajaribu kujua kama mahakama ya familia inapatikana huku,asante sana.
 
Mwenyezi mungu anisamehe ila hiyo familia mbona ya ajabu sana?

Inakuwaje tena kwenye hiyo familia Mme wa Dada yao mkubwa(yaani mkwe wao,ambao kimsingi hawana nae nasaba hata kidogo isipokuwa ni mtu kaoa tu kwao) anakuwa ndio msemaji wa familia??

Yaani shemeji yangu(kamuoa Dada yangu) aje ndio awe msemaji tena kwenye familia yetu Duuh

Au huyo Mme wa Dada yao mkubwa ana vijisenti na kielimu kidogo nini?(kama ndivyo hivyo hiyo familia basi ni wajinga na huyo bwana Mme wa Dada yao mkubwa nae ni mjinga Mara dufu, in any how mtu mwenye akili zake haijalishi mwenyezi mungu kampa nini kwenye maisha yake hawezi kukubali yeye ndio awe msemaji ukwenu kwenye ukoo ambao sio wake na hana nao udugu, labda ushauri wakimuomba tena pia yatakiwa auotoe kwa adabu kubwa isionekane kama ndio majibu)

Kama hiyo ndio nature ya hiyo familia basi hao ni wajinga bwana Capt Tamar na wewe cha kufanya hapo baada ya kupata ushauri humu jukwaani, usisahau kuwa consult wataalam wa sheria wakupe muongozo andaa vielelezo panga mashambulizi tena kimya kimya fungua kesi na haki itapatikana
Shukrani sana mkuu,nimepata mwanga hapa,Mwenyezi Mungu awabariki wote,Maxence Melo na JF kwa ujumla,asanteni sana.
 
Huyo kaka mtu ana tofauti gani na mwenda zake[emoji41]

Ila pole sana tafuta mwanasheria atakupa muongozo na usimfiche kitu ili ajue ananyumbulishaje vifungu.

Ukishindwa nitafute tukamuombe mungu aamue ugomvi[emoji23][emoji23]
Sawa mkuu,asante sana.
 
Kwanza nikuulize mirathi ilishafunguliwa kisheria mahakamani? Kuhusu mali za mke marehemu wako?
Nimejibu hili swali mara kadhaa,sina uhakika kama alifungua mirathi mahakamani,kwa kuwa vielelezo anavyopaswa kwenda navyo mahakamani ninavyo mimi na hakuwahi kuniomba nimpatie,hivyo sidhani kama Alikwenda mahakamani mkuu.
 
Ondoa shaka mkuu,huyo jamaa hata help ya kunilogea labda aje kuniomba,nadhani ni njaa tu zinamsukuma kufanya hivyo,ndugu zake wa kuzaliwa wamemwita na kumtaka mara kadhaa aachane na Mali za watu,sasa hivi amewa block wote,hakuna kitu ataachiwa mkuu,nitaleta mrejesho hapa,wadau hapa wamenipa nguvu na are ya kupigania haki yangu kwa mustakabali wa familia yangu,nipo njiani sasa hivi,nimeanza rasmi.
Safi mkuu komaa.

nimeshashughudia ktk harakati za kugombea mali zaidi ya watu wawili yaliwakuta makubwa, haki yako lakini unapotezwa.
 
Huna hata haja ya kutafuta Mwanasheria, kama upo Dar nenda pale Temeke kwenye Mahakama ya familia.
Na umesema hajakuomba vielelezo, unahisi bado hajafungua mirathi Mahakamani. Sasa wahi wewe kwenda, utapata vielelezo vyote.
Na huenda hataki kufungua, ili aendelee kuneemeka na mali za Marehemu.

Hizo ni mali za watoto, nimefiwa na Mama mwaka jana, mali zake zote tumepewa watoto wake wawili tuliobaki. Zilizobaki ni walizochuma na Baba sababu yuko bado hai.

Popote ulipo kesho nenda kwenye Mahakama inayoshughulikia mambo ya familia.
Kikao kitakaa tena ndugu wa pande zote, na utapewa kuwa msimamizi wa mali za mpedwa mkeo. Pole kwa kufiwa na mke.
Kuna mahali umekosea Mkuu, kumwambia hana haja ya kutafuta mwanasheria. Watu wengi wanahofu kutafuta wakili sababu wanadhani ni gharama sana kuwa na wakili, lakini mambo yakivurugika ndio utawaona wanatafuta wakili wakati 'its too late' na gharama itakuwa kubwa bila uhakika wakuweka mambo sawa.

Nadhani badala yakumwambia hana haja.ya kutafuta mwanasheria ungemshauri atafute muongozo au ushauri wa kisheria kwa wakili au vituo vya msaada wa kisheria.

Tuachane na hili, naomba.nikupe ujuzi wa jambo lingine. Urithi huwa ni wa warithi ambao kimsingi wanaweza kuwa.mtu yeyote yule aliyetajwa na marehemu kwenye wosia au mwenye uhusiano naye. Anaweza kuwa mke, mume, mtoto wa kumzaa, mtoto wa kuasili, mtoto wa kumlea na ndugu, jamaa na marafiki pia au taasisi, hadi serikali kwa nyakati fulani.

Urithi sio lazima uende kwa mtoto japo wana haki kirithi kutoka kwa baba yao, kumbuka ni kutoka kwa baba yao na hapa aliyefariki ni mama.
 
Mahakama ya familia mfano Temeke ukifika, unapewa mwanasheria. Nimekuelewa ila nimemwambia aanzie huko kwanza wao watampa ushauri mzuri wa kufuata.
Kwa upande wangu nimeona hivyo, hata ushauri wako wa kutafuta Mwanasheria kwanza ni mzuri pia Mkuu.
 
Upande wao wanajua mpaka mali zote. Mpaka unazozichuma sasa hivi na mpaka kesho ni za ndugu yao
 
Hivi mke akinikuta na mali alafu baadae labda nikatangulia hizi mali hazimuhusu?

Na je nimemkuta yeye na mali alafu akatangulia hizi mali hazinihusu mimi?
Zitakuhusu kama tu hakutatokea sababu zakuhitaji uthibitisho huo iwapo mmoja atatangulia.

Suala likashakuwa mgogoro na kufika kwenye vyombo vya kisheria maneno peke yake hayatoshi...ni nyaraka zitakazokidhi...inashauriwa kuandika kabisa mali za kila mmoja kabla ya ndoa.
 
Upande wao wanajua mpaka mali zote. Mpaka unazozichuma sasa hivi na mpaka kesho ni za ndugu yao
Hapana mkuu,ningetamani ujue mfumo wa maisha yangu,usingefikiri hivyo,hajui na hatakaa ajue maisha yangu zaidi ya vile anavyojua,anachojua yeye ni hizo Mali chache zinazomhusu mke wangu ambaye ni mdogo wake tu,nothing else.
 
Mkuu UMUGHAKA ni mke wangu wa ndoa kabisa,ndoa ya kanisani,na vyeti via ndoa ninavyo,tumejaaliwa watoto wawili,wote wapo shule na vyeti vyao vya kuzaliwa ninavyo,mke wangu tulimzika nyumbani kwangu,hapa hapa ninapoishi sasa.

Hizo mali wa kusimamia ni wewe tafuta mwanasheria fungua kesi mahakamani utashinda
 
Back
Top Bottom