Sawa kabisa mkuu,naomba kwanza unieleweshe jambo moja zaidi,mtu aliyeteuliwa na familia kusimamia mirathi anapaswa kwenda kuthibitishwa na mahakama,nimeambiwa kwa ndoa ya kikristo ni mahakama ya wilaya tu,lakini pia mtu huyo atapaswa kwenda na vielelezo kadhaa,vikiwemo muhtasari wa kikao cha familia,hati ya kifo,barua ya kiongozi wa serikali wa eneo alilokuwa akiishi marehemu na kiapo,sasa hati ya kifo ninayo mimi,na hakuwahi kunitaka nimpatie kwa sababu yoyote,mwenyekiti wa mtaa tunaoishi pia ameniambia kuwa hakuna mtu aliyemwendea kutaka barua yoyote kuhusiana na mirathi ya mke wangu,huyu mwenyekiti ni mtu wa karibu na familia yangu sana,ila nyumba na viwanja vyenye utata vipo kwenye mitaa tofauti tofauti,sasa je kuna uwezekano wa huyo ndugu kupata hati nyingine ya kifo tofauti na ile niliyonayo?na je nikitaka kuonana na kiongozi wa mtaa nitapaswa kwenda kwa huyu wa hapa tunapoishi au kule ambapo ndipo penye hizo Mali? Hata hivyo ni takribani miezi kumi na moja imeshapita toka mke wangu alipofariki,na kwa maelezo yako ya kisheria ni wazi kuwa alipaswa awe ameshafunga jalada la mirathi,kitu ambacho hajafanya hadi muda huu,na sidhani kama alikwenda mahakamani.