Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Pole sana kwa unayopitia ndugu. Jambo la msingi hapo kama wengine walivyoshauri ni kumtafuta mwanasheria/wanasheria wazoefu kwenye masuala haya ili upate msaada wa kitaalamu.
 
Cha kufanya ni kwenda kutengua usimamizi wake wa mirathi Kwa sababu anatapanya mali. Ya familia Kisha mengine yatakuja baada ya msimamizi mwingine kuteuliwa
 
Mkuu pole sana kwa kufiwa na mkeo...
Japo sipo vzr katika haya mambo, ila usikubali huyo mpuuzi aka take advantage kisa eti msimamizi wa milathi! Huyo ni kupe tu atanyonyaje jasho lako ingali upo hai? Inakuwaje anaweka wapangaji kwenye mali zako?
Kaweke zuio mahakamani la kutokuwa na imani na huyo bwege. Na hao wapangaji wakiendelea kuleta ukaidi wape notes wahame haraka sana.

Ukimchukulia poa huyo shemejiyo huo usimamizi wake utadumu miaka dahari huku akijineemesha na kujiimalisha zaidi.
 
Pole sana kwa kumpoteza mke wako, na pia kwa changamoto unazopitia. Nilichojifunza kwenye hili tatizo lako, ni kwamba hamkuwa na serikali moja! Na ndiyo maana kumetokea hizo changamoto kwenye usimamizi wa hizo mali.

Kiufupi hakukutakiwa kuwa na mali za mke, au mali za mwanaume; mfano hivyo viwanja!!! Mali zote zilitakiwa za wote! Na hivyo wewe kama mume wa marehemu ulistahili kabisa kuwa msimamizi wa mirathi ya mke wako.

Na hiyo mirathi ilitakiwa igawanywe kwa kuwapa watoto zaidi mali za mama yao, halafu wewe na wazazi wa marehemu mngefuatia kwenye huo mgao. Hao ndugu wa marehemu, hawakuwa na ulazima wa kusimamia, wala kupata mirathi.

Ushauri; itisha kikao cha ndugu wa pande zote mbili ili mjadiliane, na kufikia muafaka. Kugombania mali za marehemu, siyo poa kabisa.
Kugombania mali za marehemu kivipi yaani?

Kwa maelezo yake yeye ni mume halali wa ndoa,agombanie na nani tena hapo?

hajagombania na wala kulipeleka hilo suala mahakamani siyo kugombea bali ni kutafuta haki.
 
Mkuu UMUGHAKA ni mke wangu wa ndoa kabisa,ndoa ya kanisani,na vyeti via ndoa ninavyo,tumejaaliwa watoto wawili,wote wapo shule na vyeti vyao vya kuzaliwa ninavyo,mke wangu tulimzika nyumbani kwangu,hapa hapa ninapoishi sasa.
Wapi? Dodoma? Pole sana Ndugu Yangu, kama sio Wewe basi Kuna story kama hii inafanana Kwa 98%
 
Kikao cha familia kazi yake ni kuteua msimamizi wa mirathi na kuandaa mhitasari utakao mtambulisha aliyeteuliwa kua msimamizi.baada ya hapo huyo msimanizi anatakiwa kwenda mahakamani kufungua shauri la mirathi litakalosikilizwa na kutolewa hukumu ili mahakama iwe imemthibitisha na kumuidhinisha huyo msimamizi.Nayeye jukumu lake sio kumiliki mali za marehem bali ni kusimamia mali za marehemu nakuhakikisha mgawanyo wa mali zote za marehem umefanyika kwa haki.Ikiwemo kulipa na kukusanya madeni ya marehem.Kwahiyo kama bado huyo shemeji yako hajaidhinishwa na mahakama anakua bado sio msimamiz bali mteuliwa kua msimamizi hadi hukumu ya mahakama imuidhinishe..Baada ya hukumu kunakaa kikao cha kumaliza msiba na kufanya mgawanyo wa mali.Baada ya mgawanyo wa mali kufanyika msimamiz atatakiwa kurejesha mahakamani taarifa ya mgawanyo wa mali ulivyofanyika.Ata hivyo kikawaida endapo mwenza amefariki na ameacha chochote nyuma anayebaki automatik anapata kipaumbele cha kua msimamiz wa mirathi labda awe na changamoto.Sasa kwavile umekiri kuna makosa umefanya wasiliana na mwenyekiti wa hicho kikao mweleze kusudi lako lakuitishwa kwa kikao upya chakumteua msimamizi ili ujenge haja zako na kama atakataa nenda kwamwanasheria kamweleze upate ushauri wakisheria.
 
Mkuu UMUGHAKA ni mke wangu wa ndoa kabisa,ndoa ya kanisani,na vyeti via ndoa ninavyo,tumejaaliwa watoto wawili,wote wapo shule na vyeti vyao vya kuzaliwa ninavyo,mke wangu tulimzika nyumbani kwangu,hapa hapa ninapoishi sasa.
Aisee sasa mbona kama amekudharau sana mkuu na hii mikwara yake? Yaani mume wa ndoa shemeji anakupangia tena inaonekana na kipato unamzidi? Mbona inaonekana unammudu kabisa bila hata ya kupoteza hela na muda huko mahakamani?

Mi nikajua ulikuwa na mahusiano ya kawaida tu na marehemu kumbe mume kabisa? Hebu acha uzembe mkuu, simama pambana huo ndio urithi wa watoto baadae usiwachukulie poa kabisa
 
Huyu jamaa anatia aibu Sana,

Inaonekana familia ya mke imeona kabisa jamaa hafai kusimamia Mali zilizoachwa na marehemu mkewe au vipi?

Kwanza ulionaga wapi MKE anafariki kinakaa kikao Cha mirathi?

Nnachojua mke akishafariki automatically Mali zote zinabaki chini ya mume, na ndo anacontroll kila kitu. Na hakuna mahojiano.

Sasa Huyu mwenzetu atwambie,
Kwenye hiyo familia Alikua marioo analelewa au vipi?
Yaah labda alikuwa mariooo...
 
Mkuu UMUGHAKA ni mke wangu wa ndoa kabisa,ndoa ya kanisani,na vyeti via ndoa ninavyo,tumejaaliwa watoto wawili,wote wapo shule na vyeti vyao vya kuzaliwa ninavyo,mke wangu tulimzika nyumbani kwangu,hapa hapa ninapoishi sasa.
Itisha kikao cha familia, na mwenyekiti wa mtaa awepo, muweke maazimio; mali za biashara za marehemu, ziwanufaishe watoto pamoja na wazazi wa marehemu, na si vinginevyo.
Kwa mali za mkeo ambazo si za kibiashara, uza na mgawane na wazazi wa marehemu.
Baada ya hapo nenda kaanzishe familia yako mpya inayokuja​
 
@capt, usisahau kutuletea mrejesho,na hili zoezi lianze haraka iwezekanavyo sisi waswahili wasije wakakuendea kwa Babu mukulu ukapoteza kila kitu hizo ni Mali za wanao bwana kutoka kwa mama yao
 
Angalia fafanua pia hao kabila gani na wewe kabila gani angalizo, huo msiba wewe huna ndugu? Inamaana wewe zezeta kiasi hicho duuh hatari sana, Take care
 
Kweli,familia yao ina dada watatu,kaka watatu,na mume wa dada yao mkubwa ndiyo msemaji wa familia yao,kiufupi hawa dada zake wawili wananipa ushirikiano kiasi,kaka zake wawili pia wananisapoti kiaina,ila kuna huyo dada yao wa nje ya ndoa ndiyo anamsapoti shemeji kidogo,huyo dada mkubwa aliniambia kuwa ndugu zake hawamthamini kwa kuwa si mtoto wa mama yao,alikuja na baba,na ananipa ushirikiano wa kutosha,ila anasema hana sauti kwao.
Wazazi wa mke wapo?
 
Back
Top Bottom