Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Uko wapi kaka naweza kukupa msaada wawatu wanaoweza kukusaidia, ila kiufupi huyo jamaa ni mdhulumaji, kwahyo kamfungulie kesi ya aina hiyo ingawa sijui itakua ni jinai au ni nini, kama unarekod zozote za malipo ya mwisho, na baadhi ya meseji au risit za miamala, au maongez yenu kabla hajaanza bugdha hizi itakiwa vzr maana itakuwa ni ushahidi, pia umejarbu kuongea na upande wa ndugu zake? Maana haya mambo ya familia bwana yanalawama sana, anza kuongea na upande wa ndugu zake kama hawatakuelewa na kumuweka chini ujue ni njama, kwahyo unakata nao mazoea then unaenda kortin sasa.
 
Very simple Nenda mahakamani pinga uteuzi wa uyo msimamizi kwasababu hizi na nyinginezo mf mda mrefu aliotumia kusimamia na mrejesho zero, atatenguliwa then mkuu ww upo hair watoto wakiume mirathi itagaiwa kwenu na asilimia chache sanaaa inaenda kwa wazaz wake mwanamke uyo shemeji mduansii hapatikan ata kidogo Yaan kisheria
 
Kosa la kwanza wanakaaje kikao wagawane majukumu ya kuangalia mali wakat wewe ndio muhusika mkuu?
Inawezekana wanahis wewe umedandia mali za dada yao
Mtoa mada anatuficha,
Atakua alkua analelewa huyu
Unababaishwa vipi na shemeji aisee
Hizo Mali anazong'ang'ania Hao watoto wa marehemu atasomesha yeye au vipi?[emoji848]
 
Yaah labda alikuwa mariooo...
Kikao cha familia au ukoo huwa kinakaa,kisha kinampendekeza msimamizi wa mirathi,then aliyependekezwa anapaswa aende mahakamani kuidhinishwa,na huko mahakamani anatakiwa aende na muhtasari wa hicho kikao cha ukoo,death certificate,na hati nyinginezo,halafu mimi sikuwa "marioo" ndugu,ndiyo maana maisha ya familia yangu yanasonga hata baada ya kufiwa,hata sasa naona kama huyu jamaa anaona kama hizo Mali sina haja nazo,kikao huwa kinakaa mkuu
 
Nitafute Dm nikuunge na mwanasheria mzuri akusaidie

Lakini kuacha shemejio awe mrithi ni moja ya kosa kubwa ulifanya but akijaaribika kitu maana vielelezo vyote unavyo mwenyewe.
 
Itisha kikao cha familia, na mwenyekiti wa mtaa awepo, muweke maazimio; mali za biashara za marehemu, ziwanufaishe watoto pamoja na wazazi wa marehemu, na si vinginevyo.
Kwa mali za mkeo ambazo si za kibiashara, uza na mgawane na wazazi wa marehemu.
Baada ya hapo nenda kaanzishe familia yako mpya inayokuja​
Mkuu Equation x wazazi wa mke wangu walishafariki mke wangu akiwa mdogo sana,akalelewa na shemeji yake.
 
@capt, usisahau kutuletea mrejesho,na hili zoezi lianze haraka iwezekanavyo sisi waswahili wasije wakakuendea kwa Babu mukulu ukapoteza kila kitu hizo ni Mali za wanao bwana kutoka kwa mama yao
Mara nyingi huwa nipo mbali na nyumbani kikazi,ila kwa miezi hii nipo,na hadi kuniona natafuta ushauri huku ni kwa sababu nipo tayari kulishughulikia hili,mrejesho nitaleta,spending mtu mwingine apite njia ninayopitia,asante mkuu.
 
Nimesoma kwa makini nimebaini kuwa hii ndoa yako ilikuwa na shida in some points ni vile tu vitu vingi umeficha kwa faida yako binafsi.. unayokutana nayo sasa ni matokeo ya hayo matatizo uliyokuwa unapambana nayo kwenye ndoa yenu hapo awali.. tafuta njia muafaka ya kumaliza tatizo hilo la familia, Mungu akusaidie.
Mkuu Mcanada ndoa yangu haikuwahi kuwa na shida hata chembe, na hakuna nilichoficha,ila tu ni vile ndugu wa mke wangu walishapaona pale kwangu ni kama kwao,ukizingatia kuwa mimi muda mwingi nakuwa mbali na nyumbani.
 
Nenda pale Radio Njiro, kuna advocates wazuri tu.


Ukitaka namba zake fata PM..
 
Watu wengi wamechangia kwa hisia siyo kisheria. Shemeji anaweza kuwa kuwa msimamizi.
Wewe upo sahihi. Msimamizi wa mirathi lazima akaape mahakamani na lazima muhutasari wa kikao cha wana familia ndugu wa mfiwa uwasilishwe mahakamani.
Kama hajaenda mahakamani basi huyo ni batili kisheria kufanya kazi za usimamizi kabla hajarasimishwa.
Wewe upo sahihi zaidi,alichonacho huyu shemeji ni huo muhtasari wa kikao cha familia tu,alipaswa awe pia na death certificate ambayo sidhani kama anayo,maana ninayo mimi,mahakamani sidhani kama alienda.
 
Back
Top Bottom