Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Mkuu naona wachangiaji wengi wanaikwepa sana hio point,,, Kikao cha mirathi.!?? Halafu Ukweni.!?? Ili iweje.!?? Ndugu wa Mume nao walikuwa wapi.!??? Tatizo liko hapa na wala sio hio mirathi au aliyechaguliwa.

Sawa mfiwa ulikuwa na wakati Mgumu,,,, Je,Ndugu wa Mume walikuwa wapi.!? Walishiriki kikao?? Nini sababu ya kikao kufanyika Ukweni.!??

Mleta uzi Pole sana kwa Kufiwa na Mkeo.. Kilichofanya ufike hapo ndio kitafanya ushindwe hata huko Mahakamani... Rekebisha Mentality yako.. Unaonekana Mtoto wa mama sana,,, Kuwa Mwanaume kwanza ndio ulishughulikie hilo...

Be a man,,, Stay taliban...

ROBERT HERIEL msaidie huyu mawazo kisheria
Mkuu,sidhani kama kuna mahali nimeandika kuwa kikao kimefanyika ukweni,pia kisheria msimamizi wa mirathi huteuliwa na kikao cha familia au ukoo,aliyeteuliwa atapaswa kwenda mahakamani akiwa na muhtasari wa kikao hicho.
 
Nilijaribu kuyamaliza polepole,ila sasa nalazimika kutumia nguvu,ushauri please.
Wala Hata haujachelewa! Kwa jinsi ulivojibu na hali ilivo mpaka sasa, tafuta mwanasheria na fungua kesi ya mirathi, utarudishiwa haki zako zote! Walichofanya ndugu wa wife ni ku-assume tu kwamba kwa kuwa wao ni ndugu then they can decide kuhusu Mali za dada yao! It’s wrong tena very wrong unless hicho kiwanja kiliandikwa jina la kaka yake au wazazi wake …if not then hawana cha kukubabaisha!
 
Mtoa mada anatuficha,
Atakua alkua analelewa huyu
Unababaishwa vipi na shemeji aisee
Hizo Mali anazong'ang'ania Hao watoto wa marehemu atasomesha yeye au vipi?[emoji848]
Mkuu,sikuwa nalelewa,mke wangu alikuwa ni mama wa nyumbani tu,hizo Mali zake alizipata kabla hatujaoana,wakati tunaoana alikuwa ameshaacha kazi, kiuchumi mimi ndiye niliyekuwa na nafuu kuliko ndugu zake wote,sorry mkuu
 
Kuna watu wa ajabu sana,

Unakubali vipi shemeji yako , kuwa msimamizi wa mirathi.
 
Kikao cha familia au ukoo huwa kinakaa,kisha kinampendekeza msimamizi wa mirathi,then aliyependekezwa anapaswa aende mahakamani kuidhinishwa,na huko mahakamani anatakiwa aende na muhtasari wa hicho kikao cha ukoo,death certificate,na hati nyinginezo,halafu mimi sikuwa "marioo" ndugu,ndiyo maana maisha ya familia yangu yanasonga hata baada ya kufiwa,hata sasa naona kama huyu jamaa anaona kama hizo Mali sina haja nazo,kikao huwa kinakaa mkuu
Wewe ni baba wa familia so wew ndio msimamizi mkuu wa hizo mali alafu hao ndugu wa mkeo wanachofanya sio kusimamia mali bhali wamezirithi wanazitumia wanavyotaka wakati wew upo hai.. Kusimamia ni kuhakikisha hakuna natumizi mabaya ya mali za marehemu mfano Mali kuuzwa ovyoo... watoto kunyanyasika kwenye nyumba walioachwa huko ndo kusimamia ila sio anachofanya shemeji yako kiufupi kakudharau anyway ulishakosea na kama unavyosema huna shida na hizo mali fanya kama umetoa sadaka kiboyaaa tu
 
Mimi hata hiyo habari ya usimamizi wa mirathi sikuwa na habari nayo,yaani we acha tu mkuu,ungekuwa mimi siku hiyo wala usingenilaumu hapa
Wewe jamaa inaonekana hauko sawasawa.
Kesi ya usimamizi wa mirathi inafunguliwa mahakamani , na tangazo linawekwa ili kama kuna pingamizi basi upate muda wa kushughulikia.
Sasa wewe unakuja na habari zako hapa eti hukuwa na taarifa.

Kuna shida mahali..
 
Haya mambo haya nimeyapitia ila huwa ni magumu.
Ulikosea ulipokubali shemeji awe msimamizi wakati ww ukiwa hai
Shemeji bado hajawa msimamizi wa Mirathi officially, maana kuna Vielelezo Kama vile cheti Cha kifo kiko kwa Mume hajampa kwenda nacho Mahakamani kufunguwa Mirathi,au labda Shemeji kaamua kugushi hiyo Mirathi ya Dada yake bila Shemeji yake kua na taarifa!!
 
Wewe ni dereva wa daladala nini?

Umetiririka hakuna cha paragrafu, nukta, koma, nk.
Jikite kwenye hoja,achana na vipungufu vidogo vidogo sijui vya nukta nundu, mradi ujumbe unaeleweka basi mpe tu ushauri Kama unao, Mambo ya sijui yeye ni kondakta au dereva wa Daladala yanaingiaje hapa!!? Jibu hoja achaa Viroja Mkuu!!
 
Kwa kuwa huyo Shemeji keshaonesha muelekeo wa kipigaji.

Mkienda kisheria mtihani niuonao hapo ni namna ya kuthibitisha kwamba hiyo nyumba ni kati ya mali za ndoa, maana hapa nyaraka ndio muhimu.
Hivi mke akinikuta na mali alafu baadae labda nikatangulia hizi mali hazimuhusu?

Na je nimemkuta yeye na mali alafu akatangulia hizi mali hazinihusu mimi?
 
Kwa picha la haraka haraka,
Mkeo alikukamata ukakamatika haswa haswa Kias Cha hao shemej na wake zako kukudharau kiasi Cha kuoana wewe na familia yenu nzima hamuwezi kusimamia wala kujisimamia kwny mirathi ya familia yako.

Huenda washaona hujiwezi kiuchumi Wala kifedha Kias Cha kusimamia Mali zile.
Na hili Probably linasababishwa una uchumi mdg kuliko wake zako au ushalishwa limbwata. Wanakumudu.

Bila kukaza na kuonyesha makucha halisi ya kiume.

Trust me,
utapoteza kila kitu na kufurushwa Kama mbwa kwenye familia yako mbele ya wanao.
Tena anaweza aambiwa kua hata hao Watoto si wa kwake, na akaletwa Mwanaume mwingine kua ndiyo Baba halisi wa hao Watoto!!
 
Wewe jamaa inaonekana hauko sawasawa.
Kesi ya usimamizi wa mirathi inafunguliwa mahakamani , na tangazo linawekwa ili kama kuna pingamizi basi upate muda wa kushughulikia.
Sasa wewe unakuja na habari zako hapa eti hukuwa na taarifa.

Kuna shida mahali..
Hujanielewa mkuu,nimesema siku hiyo ya mazishi ambayo ndiyo kikao kilikaa sikuwa sawa kiakili,hivyo sikuzingatia kuhusu habari ya mirathi
 
Tena anaweza aambiwa kua hata hao Watoto si wa kwake, na akaletwa Mwanaume mwingine kua ndiyo Baba halisi wa hao Watoto!!
Ugh!! Umeenda mbali sana mkuu,kiufupi,mimi nina Mali nyingine ambazo hata wao hawazijui,nyumba ninayoishi ni ya kwangu,na mke wangu aliikuta na nyingine kadhaa,kinachomsukuma huyo shemeji yangu nafikiri ni njaa,alizoea kulelewa na dada yake(mke wangu)sasa hivi hana pakuchuma,nitajaribu Kuwaita ndugu zake tuongee kwa mara ya mwisho,then nitaamua,sasa hivi nina muda wa kutosha,asante kwa mchango wako ndugu.
 
Shemeji bado hajawa msimamizi wa Mirathi officially, maana kuna Vielelezo Kama vile cheti Cha kifo kiko kwa Mume hajampa kwenda nacho Mahakamani kufunguwa Mirathi,au labda Shemeji kaamua kugushi hiyo Mirathi ya Dada yake bila Shemeji yake kua na taarifa!!
Ndo maana tukamshauri aende mahakamani akajue yote
 
Haya mambo ya usimamizi wa mirathi yapo kisheria na yana utaratibu wake hata kama wengine hatuyapendi.
Kama hamukufuata utaratibu katika hatua ya mwanzo ya uteuzi basi huyo shemeji yako wala hajawa msimamizi wa mirathi na yote aliyoyafanya kwa hizo mali yanaweza yakamwingiza pabaya kisheria. Unachotakiwa kufanaya sana ni kuteua msimamizi rasmi na haraka lifunguliwe sharuri mahakamani. Itakubidi ujieleze kwa shemeji zako wengine na watu wengine wenye hekima mpaka ieleweke alichokifanya huyo mgomvi wake.Hii itakusaidia kumtenga kwanza ili asije akaleta usumbufu mwengine.
 
Back
Top Bottom