SoC01 Je, muda ni nini, na jinsi mtu anavyo weza kuwa huru na muda

SoC01 Je, muda ni nini, na jinsi mtu anavyo weza kuwa huru na muda

Stories of Change - 2021 Competition

Mulokozi GG

Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
34
Reaction score
44
Kwenye uzi huu wa mabadiliko nimetumia njia tofauti kidogo, kwani uzi huu hauja lenga kuibadilisha jamii moja kwa moja bali umelenga kubadisha au kuboresha kiunzi cha jamii(wewe msomaji), ili kiunzi cha jamii ndicho kiibadilishe jamii. Kwani moja ya zawadi na kazi kubwa mtu anayoweza kuifanya jamii au watu wanao mzunguka ni kubadilisha au kuboresha mtazamo wake kiasi cha matukio yote ya nje kutokuwa na madhara kwenye hali yake ya ndani, hivyo kuto athiri jinsi anavyo husiana na jamii inayo mzunguka. Tuanze;-

Muda(time), moja kati ya misingi ya uwepo. Kipindi cha miaka ya mwanzo mwanzo ya uwepo wa kizazi cha binaadamu, katika kutafuta njia za kumudu kwa ubora zaidi majukumu na katika uwiano sawa baadhi ya vipimo vilianza kutengenezwa. Moja kati ya vipimo hivyo ni njia ya kuhesabu na kutambua muda kwenye shughuli zilizo kuwa zinafanyika.

Kwa mjibu wa kikundi cha Mathematical Association of America kwenye makala iliyo andikwa na Keith Devlin na kuchapishwa December 1999, upimaji wa muda katika mahesabu ulianzia Misiri kwa njia za kitamaduni. Hivyo kadiri uhitaji na uelewa ulivyo ongezeka ndivyo maboresho yalivyo kuwa yakifanyika hadi kufikia hatua tuliyo ifikia sasahivi, ambapo duniani ikijizungusha mara moja tunasema ni siku, mwezi(moon) ukiizunguka dunia tunasema ni mwezi(month) na dunia ikilizunguka jua mara moja tunasema ni mwaka. Mizunguko hii tumeigawanya katika vipande vidogo vidogo zaidi kama saa, dakika na sekunde ili kutumika katika viwango vya chini zaidi.

Maendeleo ya sayanyi na tekinolojia yametusaidia zaidi sasahivi tunao uwezo wa kufanya hesabu za muda hata ulio nje ya kipindi chetu cha maisha kama binaadamu, mfano miaka ya mwanga. Mwaka mmoja wa mwanga ni sawa na kilometa trillion 9.5(ukurasa wa space.com, may 2019). Tofauti na hesabu za miaka ya kawaida ambayo ni matokeo ya mzunguko wa dunia, mwaka wa mwanga ni kipimo cha umbali ambao mwanga unasafiri ndani ya mzunguko mmoja wa dunia kulizunguka jua.

Mfano tukichukulia kuwa mwanga hauta pindishwa, kuzuiliwa au kubadilishwa; mtu akisimama juu ya soko la kariakoo akawasha tochi kwa dakika moja akaizima, ndani ya saa moja mwanga huo wa tochi utakuwa umesafiri kilometa 1,079,252,849 na ndani ya mwaka mmoja mwanga ule ule utakuwa umesafiri umbali wa kilometa trillion 9.5. Hivyo katika hali kama ile ile mwanga ulio tokana na ajari ya moto kwenye soko kuu la kariakoo wiki 10 zilizopita (mda huu nikiwa naandika uzi huu) mpaka sasahivi mwanga huo umeisha safiri takribani kilometa trillion 2.

Lakini kadiri maboresho ya jinsi ya kuhesabu muda yanavyo fanyika ndivyo watu wengi wanavyo zidi kukwama(trapped) ndani ya mahesabu hayo ya muda kiasi cha kupoteza kabisa uhalisia wa muda wenyewe. Hali hii imefanya mitazamo ya watu juu ya namba kwenye saa, siku, mwezi au mwaka kwenye kalenda kupewa uhalisia zaidi pamoja na nguvu kubwa kwenye akili na tafasiri za watu zaidi ya uhalisia wenyewe.

Mkanganyiko huu licha ya kuonekana mdogo unawafanya watu au mtu kuyapa maisha tafusiri ngumu kuziishi na unapoteza na kudumaza kwa kiasi kikubwa uwezo halisi wa mtu bila yeye kujua. Tofauti na baadhi ya falsafa na mitazamo kuwa muda ni uongo au mauzauza (illusion), kwa chochote kilicho katika mwili(physical) muda ni halisi kama uhalisia mwingine. Kwa maneno mengine muda ni katika vitu vilivyo katika mwili au vinavyo weza kuonekana(formless/form and physical).

"Kwasababu Kuna muda nafasi na muonekano(space) inawezekana, sababu kuna muda uwezekano wa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine upo hivyo kuna nafasi. Kusingekuwa na muda pasingekuwa na namna ya kusafiri."(Adiyogi: time and space explained, YouTube na Sadhguru, 18 may 2018. dakika ya 5 ).

Ufahamu wetu kama binadamu hauna muda bali kila kinachotokea kinatokea(experienced) muda kinao tokea. Hivyo hatuna njia ya kukutana na chochote kilicho pita au kijacho bali tupo au tunakutana na kile kilichopo sasahivi tu. Nje ya kile kilichopo sasahivi ni kumbukumbu (memories) pamoja na picha anazo jenga mtu (imagination) anazodhani zipo muda husika.

Hatua aliyo ifikia mtu na uwezo wake kuifunza akili yake kufanya kazi na kuwa katika hali iliyopo bila muingiliano mkubwa wa kumbukumbu au picha za mambo yajayo ni chanzo cha ufanisi mkubwa sana, ni tiba na kinga ya milele ya hisia hasi kama msongo wa mawazo, woga au hofu, hasira n.k. Kwani hali nyingi walizo na wanazo ishi nazo watu siyo matokeo ya kile kilichopo bali kile wanacho kikumbuka na kile wanacho dhani kitatokea.

Mtu yeyote aliye ifunza akili yake kufanya na kuwa katika hali iliyopo, falsafa kama usimamizi au matumizi ya muda(time management) kwake hazina nafasi sababu akili yake inakuwa katika mtiririko maalumu na ufanisi wa hali ya juu. Kwani katika uhalisia hakuna hali au kitu kama kusimamia au kutumia muda(time management) bali mtu anaweza kuboresha na kuwa bora jinsi anavyo tumia mwili wake, akili yake na nguvu zake, hivyo kuendana na mizunguko inayo uongoza mwili wake.

Zipo njia nyingi anazo weza kuzitumia mtu kuifunza akili yake kuwa katika hali iliyopo na kuwa huru na hesabu za muda, moja ya njia inayoweza kutumiwa kwa wepesi na katika mazingira ya aina yoyote ni; mtu kuzitazama fikra zake muda wote. Ifahamike kuwa mtu siyo mwili wake, mtu siyo hisia zake, mtu siyo nyumba au mali zake wala mtu siyo akili yake bali mtu ana mwili, mtu ana hisia, mtu ana mali na mtu ana akili pia. Kwa maneno mengine mtu ni mmiliki na mtumiaji wa vyote alivyo navyo lakini yeye siyo chochote kati ya vyote alivyo navyo.

Hivyo hapa mtu asijilazimishe kutofikiria bali atazame(observe) kile akili yake inacho kifikiria, yaani awe tu mtazamaji wa fikira zake. Ikitokea akasahau kwa kipindi fulani siyo tatizo bali akikumbuka tu aendelee na utazamaji wa mawazo na fikira za akili yake, hadi pale akili yake itakapo zoea na kuwa katika hali hiyo ya utazamaji yenyewe.

Itamuchukua muda au kipindi gani mtu kuwa huru na kuacha kuendeshwa na muda katika sura ya kumbukumbu na picha anazo jenga.? Hili halina dhamana(guarantee) bali ni undani(intensity) wa jinsi anavyo fanya zoezi hili utakao msaidia mhusika. Pia zoezi na njia hii siyo ya kujaribi na kuacha au nyepesi kama inavyo tamkika lakini maumivu yake na juhudi za mtu zote ni ndogo sana kulinganisha na matokeo au jinsi atakavyo nufaika na uhuru atakao upata muhusika.

Hivyo tusisitize na tufanye mabadiliko yatakayo tengeneza na kuleta uhuru kati ya mtu na vile alivyo navyo au vilivyopo. Tukifanikiwa katika hatua hii ya mabadiliko ya ndani, mabadiliko ya nje/kwenye jamii tunayo yataka itakuwa ni rahisi sana kuyafikia.
 
Upvote 3
Ni ngumu na ilikuwa ngumu kuandika baadhi ya mawazo katika lugha ya kiswahili. Sababu maneno mengi ya kiswahili yanabeba maana zaidi ya moja katika lugha nyingine, pamoja na picha zilizo nyuma ya baadhi ya maneno kwenye jamii ndani ya akili za wanajamii.

Kwa sababu kiswahili ndiyo lugha yetu na inabidi tukikuze nimejitahidi kadiri nilivyo weza kuwasilisha nguvu hii ya mabadiliko kwa lugha ya jamii yetu.

Kwa maelezo, swali na mifano ya ziada karibu sana. Jamiiforums ndo uwanja wake, to learn, reason and questioning everything in logical parameters.

Cosmic force

🙏🏾🌳🌳...
 
Ukiwa kwenye sayari hii huruhusiwi kusema hakuna muda,Mungu alipoumba vitu dunian kila baada ya kuumba akaumba na muda, means aliweka limits

Nukuu ya Biblia kitabu cha mwanzo 1
" ...ikawa jion ikawa asubuhi siku ya kwanza... siku ya pili... n.k"

Hivyo mwanadamu akiwa duniani huwezi kumtenganisha na muda na hawez kuishi nje ya muda

Ila ukitoka nje ya dunia hakuna kitu kinachoitwa muda, no morning na evening... you just live. Ndomaana Mungu hana muda..we unaona anachelewa kukujibu yeye anaona vitu viko palepale...an he's like what is he saying..[emoji848]
 
Back
Top Bottom