Je, Mungu ameumba baadhi ya watu fulani kuwa masikini?

Je, Mungu ameumba baadhi ya watu fulani kuwa masikini?

Tajiri wa matajiri

Senior Member
Joined
Apr 17, 2024
Posts
166
Reaction score
649
Wakuu kuna swali hili mara zote linanitatiza aisee je kuna watu mungu ameumba kuwa maskini? Na kuna wengine ameumba kuwa matajiri? Na kama hivyo kwanini? Nchi nyingi za kiafrika watu wengi ni masikini kulinganisha na bara la ulaya,America na Asia?

Kwamba kuna watu wa rangi fulani l(afrika) na watu wa ngozi nyeupe ukilinganisha waAfrika wengi ni masikini pamoja na nchi zao lakini kuna maliasili za kutosha lakini raia wao ni maskini wa kutupwa Sana aisee

Je, kuna watu au bara fulani limeumbwa kuwa maskini milele je umasikini unaumbwa na mungu? Au watu tunajitakia?
 
Mbona jibu ni rahisi tu AKILI

Ila swali ninalojiuliza hivi Waafrika tumepewa akili kidogo au hatutumii akili?

Maana Mungu kama ameweka principles actions zako ndio zita determine destination yako
 
Wakuu kuna swali hili mara zote linanitatiza aisee je kuna watu mungu ameumba kuwa maskini? Na kuna wengine ameumba kuwa matajiri? Na kama hivyo kwanini? Nchi nyingi za kiafrika watu wengi ni masikini kulinganisha na bara la ulaya,America na Asia.....
Umasikini ni wa kujitakia, wala sio Mungu, jiulize katika nchi yako kuna mito na maziwa, kuna ardhi yenye rutuba, kuna madini, kuna misitu, wanyama wa kila aina ambao Mungu amewaumba, hali ya hewa nzuri hivyo umevitumiaje katika kukutajirisha?

umasikini unatengenezwa na unyonyaji, upatikanaji hafifu wa maarifa ya kumuwezesha mtu kutumia rasilimali zilizomzunguka. Mungu akamweka Admu katika bustani akamwambia ailime na kuitunza, muda mwingine umasikini inaletwa na uvivu
 
Upo sahihi Kbsa mkuu
 
Mungu aliumba
Kichwa na mkia
Slave na master
Mkombozi na mkombolewa
Kiongozi wa dini na muumini
So kwa maana iyo maskini na tajiri ni moja ya uumbaji wake

Ata ukifuatilia ktk bible kuna mitume na manabii waliokua
Maskini na kuna mitume na manabii walokua matajiri
 
Mbona jibu ni rahisi tu AKILI

Ila swali ninalojiuliza hivi Waafrika tumepewa akili kidogo au hatutumii akili?

Maana Mungu kama ameweka principles actions zako ndio zita determine destination yako

Nani anayetoa/gawa akili hata akampimia mwafrika nusu kikombe? Na kwa nini?
 
Umasikini ni wa kujitakia, wala sio Mungu, jiulize katika nchi yako kuna mito na maziwa, kuna ardhi yenye rutuba, kuna madini, kuna misitu, wanyama wa kila aina ambao Mungu amewaumba, hali ya hewa nzuri hivyo umevitumiaje katika kukutajirisha?

umasikini unatengenezwa na unyonyaji, upatikanaji hafifu wa maarifa ya kumuwezesha mtu kutumia rasilimali zilizomzunguka. Mungu akamweka Admu katika bustani akamwambia ailime na kuitunza, muda mwingine umasikini inaletwa na uvivu

Upatikanaji hafifu wa maarifa ya kumuwezesha mtu kutumia rasilimali kutoka wapi? Kuzaliwa nayo? Chuo? Mapokeo? Miujiza? Maono? Na kwa nini ni hafifu kwa mwafrika tu?
 
Upatikanaji hafifu wa maarifa ya kumuwezesha mtu kutumia rasilimali kutoka wapi? Kuzaliwa nayo? Chuo? Mapokeo? Miujiza? Maono? Na kwa nini ni hafifu kwa mwafrika tu?
Kwani hayo maarifa Mungu ndio anatoa?, Maono Mungu anatoa? Mungu alimwambia Adamu utailima ardhi nayo itakupa mazao, sasa kama huilimi unataka mazao yatoke wapi? hutaki kuvua samaki unataka Mungu akuletee nyavu? maarifa yapo ni jukumu lako kutafuta. Ndio maana wengine wako Bize kufanya utafiti juu ya upatikanaji wa madini, mafuta ambavyo vyote viko chini ya ardhi, tena katika ardhi zetu
 
Ok sawa kumbe ni Mungu basi sawa, so aliwabagua weusi akawanyima hayo maarifa akawapa wazungu? I rest my case.

Then utafiti na Mungu wapi na wapi?
 
Cha msingi omba Mungu upate riziki ya kutosha, hayo mengine ni majaaliwa
 
Ok sawa kumbe ni Mungu basi sawa, so aliwabagua weusi akawanyima hayo maarifa akawapa wazungu? I rest my case.

Then utafiti na Mungu wapi na wapi?
Maarifa yanatafutwa, kwa mfano Tanzania ilitoa wanafunzi wakajifunza mambo ya petrol na gesi, huo ujuzi walioupata huko umetumika wapi? huwa kuna Watu wanaenda India na nchi zingine kupata ujuzi wakirudi wanafanya nini au wanakuwa machawa?
 
Kwa hiyo sio kutoka kwa mungu? "Yanatafutwa" na matumizi yake ni subject ya uelewa, maana wapo wengi wamepewa maarifa na hawana hata uwezo wa kuyatumia. Watu weusi tuna shida ya kuyatafuta maarifa na kuyaamini kwanza, ukishaamini una maarifa ndio unapata confidence na uwezo wa kuyatumia. Sio ajabu kabisa kwa mtu mweusi kufanya utafiti wake na baadaye akaukana, yani haamini andiko lake mwenyewe so hapo ndio shida inapoanzia. Msomi aliyefanya tafiti hadi zikampa Phd bado haziamini kama zinafanya kazi then anarudi kufanya biashara ya kiosk cha stationery kwa kuwa mmachinga anauza, so anaamini kwenye mauzo ya kimachinga kuliko high level business research aliyofanya mwenyewe.

Wenzetu maarifa wanayapata vyuoni kwa kusoma sana, kupractice na kufanya tafiti na wanafanya implementation ya tafiti zao hadi zinaunda biashara/taasisi, body of knowledge ambayo wanatumia kubadilisha maisha yao, sio kwa kusubiri maarifa wapewe na mungu (wa kufikirika) ingekua maarifa yanatoka kwake, leo hii kwa idadi na makanisa, vituo vya maombi, waombaji, misikiti, mikesha nk iliyopo Africa tungekua tunaongoza kwa maarifa na kila aina ya maendeleo badala yake tunaomba sana na kusubiri miujiza ishuke toka kwa tuliyemuomba! Hii ni moja ya sababu kubwa ya weusi (sio waafrika tu) kuwa masikini sehemu zote za dunia. Marekani makanisa yamejaa ZAIDI kwenye mitaa ya watu weusi pamoja na utajiri wake wote, kama ambavyo sehemu zote za dunia
 
Kwa hiyo sio kutoka kwa mungu? "Yanatafutwa" na matumizi yake ni subject ya uelewa, maana wapo wengi wamepewa maarifa na hawana hata uwezo wa kuyatumia. Watu weusi tuna shida ya kuyatafuta maarifa na kuyaamini kwanza, ukishaamini una maarifa ndio unapata confidence na uwezo wa kuyatumia. Sio ajabu kabisa kwa mtu mweusi kufanya utafiti wake na baadaye akaukana, yani haamini andiko lake mwenyewe so hapo ndio shida inapoanzia. Msomi aliyefanya tafiti hadi zikampa Phd bado haziamini kama zinafanya kazi then anarudi kufanya biashara ya kiosk cha stationery kwa kuwa mmachinga anauza, so anaamini kwnye mauzo ya kimachinga kuliko high level business reserach aliyofanya mwenyewe.

Wenzetu maarifa wanayapata vyuoni kwa kusoma sana, kupractice na kufanya tafiti na wanafanya impelementation ya tafiti zao hadi zinaunda biashara/taasisi, body of knowledge ambayo wanatumia kubadilisha maisha yao, sio kwa kusubiri maarifa wapewe na mungu (wa kufikirika) ingakua maarifa yanatoka kwake, leo hii kwa idadi na makanisha, vituo vya maombi, waombaji, misikiti, nk iliyopo Africa tungekua tunaongoza kwa maarifa na kila aina ya maendeleo badala yake tunaomba sana na kusubiri miujiza ishuke toka kwa tuliyemuomba! Hii ni moja ya sababu kubwa ya weusi (sio waafrika tu) kuwa masikini sehemu zote za dunia.
Nadhani tumeelewana, sisi waafrika ni wazembe kwenye kutafuta maarifa na kuyatumia hayo maarifa yatupe matokeo, Kama ni raslimali tunazo za kutosha, madini, mafuta, mito,maziwa na bahari, ardhi nzuri zenye rutuba, wanyama wa kutosha lakini sisi ndio masikini vitu vingine tunanunua kutoka kwenye nchi za jangwani. Hapo utasema Mungu ana ubaguzi? basi kama Mungu anaupendeleo basi katupendelea sisi waafrika, yaani tunaweza kujiita mbeleko Fc lakini tumeshindwa kubebeka
 
Yes tunavunja na kuua viwanda tulivyoachiwa na mkoloni na kugeuza makanisa then tunafanya maombi ndani ya hayo makanisa tupate ajira! Serikali zinaua kila private sector inapoanza kukua halafu inataka watu wake wapate ajira, na haina uwezo wa kuajiri watu wote, weusi tunawachukia matajiri na kuwafanyia fitna muda wote na sabotage ya taasisi zao zinazotuajiri wakati ndio wanaotuajiri kwa wingi kuliko serikali, yani muda wote tupo vice versa.

Akina Galileo, Newton, Archimedes, Faraday n.k. hawakufanya maombi wala hawakuenda vyuo vikuu vyenye majina makubwa kufanya inventions walizofanya walikua kwenye mazingira yao tu including chini ya miti au mashambani na wakatumia maarifa yao kwa kufikiria sawasawa tu na wakagundua makubwa ambayo tunayaishi na michango yao kwa maendeleo ya dunia yanaishi hadi leo! Weusi tumechangia nini hadi sasa kusukuma dunia mbele? So shida ni mentality kabla ya mengine yote
 
Yes tunavunja na kuua viwanda tulivyoachiwa na mkoloni na kugeuza makanisa then tunafanya maombi ndani ya hayo makanisa tupate ajira! Serikali zinaua kila private sector inapoanza kukua halafu inataka watu wake wapate ajira, na haina uwezo wa kuajiri watu wote, weusi tunawachukia matajiri na kuwafanyia fitna muda wote na sabotage ya taasisi zinazotuajiri wakati ndio wanaotuajiri kwa wingi kuliko serikali, yani muda wote tupo vice versa.

Akina Galileo, Newton, Archimedes, Faraday n.k. hawakufanya maombi wala hawakuenda vyuo vikuu vyenye majina makubwa kufanya inventions walizofanya na michango yao kwa maendeleo ya dunia yanaishi hadi leo! Weusi tumechangia nini hadi sasa kusukuma dunia mbele? So shida ni mentality kabla ya mengine yote
Ubarikiwe sana
 
Mungu aliumba
Kichwa na mkia
Slave na master
Mkombozi na mkombolewa
Kiongozi wa dini na muumini
So kwa maana iyo maskini na tajiri ni moja ya uumbaji wake

Ata ukifuatilia ktk bible kuna mitume na manabii waliokua
Maskini na kuna mitume na manabii walokua matajiri
Chai HIYO.

Mungu alimuumba adamu na vitu vingine ikiwemo wanyama na maliasili zilizopo dunianii
 
Maskini ni mvivu wa kufanya kazi na kufikiri
 
Back
Top Bottom