Je, Mungu anajua utakwenda motoni au mbinguni?

Na kwa nini aumbe mgaidi wanakata vichwa watu wasiomkubala Alla!!?
 
Ah unafaa ukutane live umuulize hayo Maswal
Mimi sitaki kusikia tena kuhusu Mungu kama wazo.

Kama yupo kweli, kwanza thibitisha uwepo wake — kisha nielekeze yuko wapi nikamfuate, nimuulize uso kwa uso.
 
Kwa hiyo Mungu anaumba watu halafu aje awachome tu basi ndio furaha yake!! Mungu gani huyu!!?
Wewe hapo ukiambiwa chagua umaskini au utajiri utachagua nini...?

Jibu kwa ufasaha nataka kukufundisha kitu
 
Kama Mungu anajua Future yako
Je Anajua utaenda Mbinguni au Motoni?

Na Future inaweza ikabadilika?
Kumbukumbu la Torati 30:19-20
Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.
 
Amen
 
Mkuu kama anajua nitaenda motoni kwanini aniletee manabii??

Na hapo umeongelea kujiua, vipi kuuawa?
Mfano huko Israel, Palestine, Iran watu wanakufa tu, wanauawa hata ambao sio wapiganaji!! Ina maana walioangiwa watakufa kwa kulipuliwa na mabomu?
Huyo mlipua mabomu anakua na hatia ilhali yeye ni mfanikisha lengo la muondoa uhai??
 
Mungu ndiye aliamua kutuumba sisi, na alituumba Kwa Mapenzi yake kwetu, Mungu alipotuumba alitaka tuishi vizuri, na ili tuishi Vizuri akatuwekea taratibu na Sheria....! Pia akasema tumuabudu yeye pekee Kwa sababu ndiyo muumba wetu.

Mungu ilibidi aachilie Shetani aje kutawala hapa Duniani ili Tumuabudu yeye, hata sisi Wachache tunaomuabudu, tunamuabudu ili tuwe huru Toka Vifungo vya Shetani, kama Shetani asingekuepo means Jehanamu isingekuepo coz Jehanamu aliumbiwa Shetani, hivyo hakuna Binadamu ambaye angemwabudu Mungu, So pale Shetani akitubana kwenye Kona ndipo tunamwendea Mungu Sasa, na pale tunapomwendea yeye ndipo hapo akaweka Kanuni. (Mungu anazo kanuni na Shetani anayo Masharti)

Kanuni za Kuomba, kanuni za kupigana Vita vya kiroho, kanuni za kusinda n.k.... Na ili umshinde Shetani lazima ufate kanuni hizo, ufate Sheria zake.

Dunia hii ilipoumbwa haikuanza tu na Vita, haikuanza tu Magonjwa, haikuanza na Ajari, mabaya yote yaliyokua yanatokea ni Kwa sababu Binadamu hataki kufata Sheria na Kanuni ambazo Mungu alituwekea.

Mfano tunazo Amri za Mungu, Mungu anasema USIUE, kwani wewe Binadamu usipoua kama Mungu alivyosema, Mungu anapata faida Gani, ama unadhani Ukiua Mungu anapata Hasara Gani, ila usipoua ni wewe ndiyo unapata faida, coz ukiua na wewe utauwawa, ama utafungwa Maisha Jela.

Alisema Usizini, usipozini wewe unadhani Mungu anapata faida yoyote..!? Ila ukizini ni wewe utapata hasara, utakamatwa Ugoni, utapigwa faini, utavuruga familia na Watoto utapata Ukimwi n.k.
Hivyo utaona yote aliyotukataza ni Kwa faida yetu wenyewe, ili tuishi Kwa raha na Upendo sawa na maono yake.

Sisi Binadamu hatutaki kufata Sheria Wala Kanuni, na alisema msipofata Sheria na Kanuni mtakutana na Shetani, ana Hasira kama Simba....! Mabalaa yakitukuta hatutaki kurudi kwenye Sheria zake na Kanuni zake, tunataka Mungu atuokoe huku tuliendelea na njia zetu mbaya.

Kama wewe ni Mama ama Baba nyumbani Watoto wako umewapa Sheria zako, na wanafata, na wasipofata unawaadhibu, Tena kama Baba tutasema Baba hakosei, akisema kasema...!

Dunia hii Haina maana yoyote ya sisi kuwepo bila kumwabudu Mungu, nje ya hapo Haina Maana yoyote, ni muhimu kuacha lDhambi na kumrudia Mungu.

The Creator is Coming.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…