Je! Mungu ni yule yule?

pole ndugu yangu kwa kudanganywa wito wangu kwako soma biblia vizuri utaufahamu hukweli, wacha kuambiwa hadithi ambazo hazina ukweli ndani yake.

Ukisoma biblia utagundua ugomvi wa Yesu na mafarisayo ni mafarisayo kumwabudu Mungu kwa unafiki wa midomo yao, huku Mioyo yao ikiwa mbali na Mungu.

Ndiyo maana nakwambia someni maandiko mfahamu kweli na kweli iwaweke huru, acheni kusikiliza uzushi.
 
UHURU JR said:
Nyie mngeweza kuthibitisha kuwa hakuna mungu basi kusingekuwa na haja ya mabishano hapa,ila kwa kuwa mnakubalia kuwa hamuwezi kuthibitisha hilo ndiyo maana inakuwa ngumu kukubali maneno yenu tu.
Asante chief kama na wewe umeliona hili.

Jana niliomba wathibitishe kuwa Mungu hayupo,wakaja na illogical excuse

Wanaomba sisi ndio tuthibitishe.

Hii ni sawa na mtu anayetoa tuhuma,halafu anaomba wengine ndio wamtafutie ushaidi

Tutakuwa tunaimba wimbo wa Thibitisha,thibitisha,thibitisha....
 
Kama angekuwepo, asingeumba dunia yenye kuruhusu mabaya kama hii.

mkuu kuna kitu hapo hakipo sawa katika kujua nini hasa sababu ya kuwepo hapa duniani, kwajinsi nijuayvo mimi nikwamba kila mtu ana sababu yake ya kuwepo na kuishi hapa dunian, sasa kupata shida au raha intokana nakiwango cha maarifa cha mtu husika, mungu alisha maliza kazi yake ya uumbaji, the rest ni kazi kwetu. cha kuhangaikia hapo ni kuishi maisha yako na kutojifananisha na mtu yeyote aliye kuwa maarufu hapa duniani,kwa kufanya hivo ni kujipoteza katika dira ya vile amboyvo ungetakiwa uwe ,, be who you are, be the greatest version, we don't suppose to be the copy of any version. coz naamini dunia ime stack bado ipo pale pale walipo ishia watu maarufu walio jitambua kalne nyingi zilizo pita,

kutupia lawama kwa mungu kwa matatitzo yetu binafsi au kusema hayupo pia kiwango cha maarifa kina husika.

NB: nendeni katika masinagogi ili muweze kupata mwanzo wa kuanzia safari na wala msiogope kutoa pale mnapo takiwa kutoa kile kinacho itwa sadaka maana kila kitu katika dunia hii kina price yake hakuna kitu cha bure hiyo ni elimu kama elimu zingine sema utoaji wake wa ada uko tofauti kidogo,,,,
 
Hapo ndipo walipowapumbaza wavivu wa kujiongeza kama nyie. Hebu nijibu haka kaswali. Je, uwepo wa shetani ilikua ni mipango ya mungu au yupo kwa sababu mungu alifeli?

elewa kwamba mungu ni nani au jiongeze kwa kujitafakari wewe binafsi utajua kwamba mungu alikuumba kwa mfano wake yeye sasa who are you? unapo tamka shetani katika fikra zako una pata picha gani? je unahisi ndio yule tunao abiwa kuwa anajicho moja au ni yule mwenye kucha ndefu na mampembe kichwani mwake? hebu jiongezeni hapo tuone katika uhalisia lipo je hili
 
Bahati mbaya mm siamini kama kuna mdudu anaitwa mungu
 
Kwa mfano wako huo ina maana mwenye nyumba endapo atasema nyumba yake haina madawa (kisichokuwepo) je,kauli yake hiyo ndiyo itakuwa ukweli wenyewe kisa tu hawezi kuthibitisha kisichokuwepo?
Maana kuna tofauti ya kusema kitu fulani hakipo na kusema huna uhakika kuwa hicho kitu kipo au hakipo.
 
Kiranga ni mtu ambaye anajitahidi sana kujua uwepo wa Mungu, ila hajapata mtu sahihi wa kumdhibitishia hilo kwa namna ambayo angeielewa au kuipendelea zaidi
 
Hapo ndipo walipowapumbaza wavivu wa kujiongeza kama nyie. Hebu nijibu haka kaswali. Je, uwepo wa shetani ilikua ni mipango ya mungu au yupo kwa sababu mungu alifeli?
Kama unataka majibu hayo sali sana utayapata.

unapomwita mtu usiemfahamu mvivu wakujiongeza wewe ndio unaeonekana huna la maana.
huwezi kutoa point yako bila kutusu watu halafu we ndie ulie elimika. tutolee uvivu hapa.

Usiniulize maswali ya Mungu . Yeye ndio mwenye majibu . kama unayataka sana sali utayapata.
Kama humwamini basi fuata njia zako nyingine usilazimishe watu kukujibu. Unataka majibu ya nini
Kwa kitu ambacho hukiamini ? au unatafuta kujibishana tu na watu .?
 
Kiranga ni mtu ambaye anajitahidi sana kujua uwepo wa Mungu, ila hajapata mtu sahihi wa kumdhibitishia hilo kwa namna ambayo angeielewa au kuipendelea zaidi
We unaamini kuwa mwenye kutaka kujua uwepo wa mungu ndiyo atakuja huku kweli?
 
Yaani kabisa unauwezo wa kutamba kuwa unafikiria kwa kuamini upumbavu. Uwezo wako wa kufikiria ni mdogo sana. Utatawaliwa milele hizo fikra zako.
 
Hilo swali ni gumu huwezi kulijibu
 
sijawah kuwa na comment juu ya hz mada, mana maswala ya uwepo wa Mungu sijayafatilia wala kutokuwepo kwake bdo cjachunguza, na sijui ntaanzia wapi? nyie endeleeni.
 
Ndio hivyo mkuu, halafu anakuja kutafuta majibu kwa kina Kiranga... dah! Aisee
Naona watu wako na mzee wa ligi hapa na naona mmoja mmoja anamuacha maana hata ukijibu unakuwa unafanya kazi bure tu maana atakuja kuuliza swali lile lile tena huko mbeleni......

Kaazi kweli kweli.....
 
Mzee wa ligi yupo na wimbo wake "thibitisha" hiyo ndio chorus ya wimbo wake ni kama kasuku...

Lazima umuache wimbo wake wa " bado hujathibitisha" hiyo ndio default position yake mtaenda baadae anarudi default position yake...
 
Hujaelewa hoja yangu.

Unaamini kwamba mungu yupo, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?
 
Mzee wa ligi yupo na wimbo wake "thibitisha" hiyo ndio chorus ya wimbo wake ni kama kasuku...

Lazima umuache wimbo wake wa " bado hujathibitisha" hiyo ndio default position yake mtaenda baadae anarudi default position yake...
Hujathibitisha bado.

Pia hujaeleza kwa nini mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.
 
Naona watu wako na mzee wa ligi hapa na naona mmoja mmoja anamuacha maana hata ukijibu unakuwa unafanya kazi bure tu maana atakuja kuuliza swali lile lile tena huko mbeleni......

Kaazi kweli kweli.....
Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?
 
Yaani kabisa unauwezo wa kutamba kuwa unafikiria kwa kuamini upumbavu. Uwezo wako wa kufikiria ni mdogo sana. Utatawaliwa milele hizo fikra zako.

Kwa nini unaendelea kuni Quote ?
Unadai naamini upumbavu , basi na wewe ni mpumbavu kujibishana na mpumbavu.
Karibu ususahau Kusali sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…