Je! Mungu ni yule yule?


Hapana.

Wajibu wa kuthibitisha ni wa yule anayesema madawa yapo. Ndiyo maana polisi wanaosema madawa yapo wanafanya msako. Wakishindwa kuthibitisha kwamba madawa yapo hawana haki ya kusema madawa yapo.

Other than abstracts logical constructs, kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo. Kwa sababu hakipo. Kinachothibitishwa ni kilichopo. Kwa hiyo suala zima la kumtaka anayesema kitu hakipo athibitishe -out of logical constructs- kwamba hakipo ni kutoelewa dhana ya kuthibitisha.

Nimeeleza kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote ambaye ameumba ulimwengu huu hayupo.

Kwa sababu ulimwengu huu kuruhusu mabaya kutokea kunam contradict huyo mungu kuwepo.

Kama vile pembetatu isivyoweza kuwa duara ndivyo mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote asivyoweza kuwa kaumba ulimwengu huu.

Unaweza ku reconcile hii contradiction?

Imekuwaje mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?
 
Mkuu kati ya siku nimekuelewa basi ni leo kwenye hili bandiko lako.
Kwamba huwezi kuthibitisha kitu kisichokuwepo ila unathibitisha kilichopo hii imenikaa akilini haswaa.
Asante sana
 
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Alitaka kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya ila hakuweza?

Kama hakuweza, ni muweza yote kweli?

Au aliweza kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya ila hakutaka tu?

Kama aliweza ila hakutaka tu, ni kweli ana upendo wote?

Mungu huyu yupo kweli au ni hadithi tu?

Mbona idea yenyewe tu inaji contradict?
 
gambada ynwa said:
Mkuu kati ya siku nimekuelewa basi ni leo kwenye hili bandiko lako.
Hapana chief,bado hujaelewa alichosema

Ungeelewa,usingekikubali
Kwamba huwezi kuthibitisha kitu kisichokuwepo
Hapo ndio tatizo lilipo

Umejuaje kuwa hakipo in the first place,mpaka useme hakina sifa ya kuthibitishwa?

Lengo kuu la kuthibitisha,ni kujua kuwa kitu kipo au hakipo

Sasa unaposema hiki hakiwezi kuthibitishwa kwasababu hakipo,umejuaje kuwa hakipo bila kuthibitisha?

hujaona tatizo kwenye hio hoja?

His excuse is simply flawed

ila unathibitisha kilichopo hii imenikaa akilini haswaa.
Asante sana
Kitu ambacho unajua kipo hakiitaji uthibitisho,maana kipo

Tunaitaji uthibitisho kwenye kitu ambacho hatuna uhakika kama kipo au hakipo.
 
Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?

je, unajua kama Kila ushahidi una namna yake yaku uwakilisha ? kwamfano wewe ukiwa unaumwa malaria ukaenda kwa doctor anakuthibitishia vip kama kweli homa yako ni ya malaria? so kila unapo taka kuthibitisha kitu au jambo lolote kunaaina ya kuwakilisha kwanza utambue hilo, sio lazima ukione kwa macho au kusikia sauti tu basi... ni lazima ujue kutumia vizuri milango yako yote mi 5 ya fahamu na yaziada,

Mungu ni jina tu ambalo lina wakilisha nguvu ya uweza ambayo ndio chanzo cha kila kiumbe hai una cho kiona katika ulimwengu huu,, by the way kwakifupi katika kuthibisha uwepo wamungu ya kupasa uelewe uwepo wa nafsi na roho na hivi vitu ni kitu gani kama utakua hujui ni nini hivi vitu mkuu kiranga itabidi niishie hapo,, na kama unajua hivi vitu vitatu yaani nafsi, roho na mwili nambie ili niendelee maana isije nikawa nime muingiza chuo kikuu mwanafunzi wa chekechea(vidudu) itakuwa vigumu kunielewa....
 
Wapi umethibitisha mungu yupo?

Umesema "Mungu ni jina tu ambalo linawakilisha nguvu na uweza ambayo ndio chanzo cha kila kiumbe hai" ukiambiwa chanzo cha viumbe kuwa hai ni nguvu ya uvutano utasema nguvu ya uvutano ni mungu?
 
Wapi umethibitisha mungu yupo?

Umesema "Mungu ni jina tu ambalo linawakilisha nguvu na uweza ambayo ndio chanzo cha kila kiumbe hai" ukiambiwa chanzo cha viumbe kuwa hai ni nguvu ya uvutano utasema nguvu ya uvutano ni mungu?

nimekuuliza unajua nafsi,roho na mwili? au hujaona kama ni swali hilo kiranga..
 
Suala la polisi kufanya msako katika hiyo nyumba ni kutaka kuthibitisha kuwa madawa yapo au hayapo,ila kauli ya mwenye nyumba kusema nyumba haina madawa(kisichokuwepo) kama ulivyokubali kuwa haiwezi kuwa ndiyo ukweli na ni kwa sababu hakuna uthibitisho wa kufanya ijulikane ni kweli yapo madawa au hakuna.

Hivyo nanyi mnaosema hakuna mungu,kauli yenu hiyo haiwezi kuwa ndiyo ukweli kama ilivyo kwa mwenye nyumba kwa sababu hakuna uthibitisho huo. Kwa maana hiyo hata kama sie hatuja thibitisha(kama msemavyo)bado kusema kwenu kuwa hakuna mungu haiwezekani kuwa ndio ukweli,na suala la mungu si suala la kawaida kwa maana kwamba kuna tofauti endapo utasema mungu yupo au hayupo. Kumbuka sijazungumzia ni nani mwenye wajibu wa kuthibitisha hivyo nitashangaa kama utaanza kuzungumzia mwenye wajibu wa kuthibitisha.
 
Ukiacha kwanza hilo suala la jinsi ulimwengu kuwa na maovu,hivi katika sifa zote zilizo elezwa kuhusu mungu wewe umeziona zinaendana kabisa kwa maana hazina tatizo kwa jinsi zilivyoelezwa?
 
Kama mungu hayupo, swali zima la kuuliza mungu ni yule yule ama la linakosa maana.Maana msingi wake, kwamba kuna mungu, unakuwa potofu.

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
 
Wewe unaweza kuthibitisha nini?

Unajua maana ya kuthibitisha?
Unaweza kuthibitisha logically kwamba mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote kuumba ulimwengu mwenye mabaya ni contradiction.

Kuthibitisha ni kuondoa shaka yoyote.

Hujajibu swali.

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
 
Unaweza kuthibitisha logically kwamba mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote kuumba ulimwengu mwenye mabaya ni contradiction.
Jibu la swali langu liko wapi?

Mwanzo uliuliza swali la kilevi kuwa "unaweza kuthibitisha kuna Mungu"?

Sasa umebadili swali,na kuuliza kitu kingine tena...

Yaani hujui kuuliza "Unaweza kuthibitisha kuna Mungu" na kuuliza "Unaweza kuthibitisha logically kwamba Mungu muweza yote,mjuzi wa yote na mwenye upendo wote kuumba ulimwengu wenye mabaya ni contradiction" bayo ni maswali yanayohusu vitu viwili tofauti kabisa,yaani wewe unajiona tu unauliza kitu kile kile

Kama ungelkuwa unajua tofauti iliyoko hapo usingerukia kwenye hilo bila kumaliza la kwanza kwanza....
Kuthibitisha ni kuondoa shaka yoyote.
Kuondoa shaka ya kitu gani?

Unaweza kunipa mfano mmoja wa hili suala lako?
Hujajibu swali.

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
Inaonekana kuna unachotumia na kinaharibu uwezo wako wa kufikiri...

Nilikuuliza wewe umeweza kuthibitisha nini?

Sijaona jibu la swali lako hili....
 
Hujaona jibu la swali langu?

Unategemea kuona jibu la swali langu wapi?

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
 
Hujajibu nilichokuuliza.....
Huwezi kutaka nikujibu wewe tu, hata baada ya kukujibu mara lukuki.

Utaonekana unatumia mbinu tu ya kukataa kujibu.

Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?

Kama hakuna kinachoweza kuthibitishwa, that is an even worse indictment to the idea that god exists. It is not a vindication.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…